Jenista Mhagama na gharama za kuhamia Dodoma

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,034
Huyu Jenista Mhagama anadhani hizo posho za Mawaziri za miezi mitano ndiyo zitatosha kugharamia Serikali kuhamia Dodoma? Duh!

Gharama za kuhamia Dodoma ni kati ya 1.5 trillion mpaka 2 Trillioni halafu yeye anakuja na posho za miezi mitano za Mawaziri na anashindwa kuweka wazi hata hizo posho zake anazostahili kupata kwa hiyo miezi mitano.

========

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amesema suala la bajeti ya kuhamishia makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam litatatuliwa kwa kutumia posho za safari za mawaziri.

Akizungumza katika kipindi cha Safari ya Dodoma kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mhagama amesema suala la bajeti wanalijua wenyewe serikalini.

“Bajeti tulizopanga, hasa ya 2016/17 sisi tunajua tulipanga nini, tunafahamu mapato yaliyopitishwa na Bunge yakoje. Kwa mfano mimi Jenista (waziri) kwa mwaka huu mzima wa fedha nina mikutano minne Dodoma. Kwenye ile mikutano yote natakiwa kulipwa posho, maana yake ni kuwa napaswa nipate posho ya miezi mitano, sasa fedha hiyo ndiyo itakayoingizwa kwenye gharama za kuihamishia Serikali Dodoma,” amesema.


Chanzo: Mwananchi
 
nilimsikia na mimi kwenye Interview ya TBC kipindi cha Safari ya Dodoma anadai maandalizi ya ofisi za serikali dodoma yamekamili kwa asilimia 75 na makazi kwa watumishi asilimia 70 hivyo wanaweza kuhamia kwa awamu awamu ikabidi nizime TV nikalale
Ungeivunja kabisa
 
Hao mawaziri wasipojitoa muhanga na kumwambia ukweli huyo kiongozi wao hakika wataishia kujichekesha, kuongea uwongo, kutafuta na maneno mazuri ya kumfurahisha boss wao lakini mwisho wa siku ukweli utatamalaki na wao wataishia kukumbwa na aibu isiyo na mfano.

Kwa suala la kuhamia Dodoma tumesikia CDA na TBA wameshaanza kuwatimua wapangaji wao ili kupisha watendaji wa Serikali watakaohamia Dodoma. Hivi kwa nini watawala wanakuwa waongo na waoga kusimama katika ukweli. Ilani ya CCM kwa mwaka 2015 -2020 imesema wazi kipi kinatakiwa kufanywa kwa sasa katika mpango wa Serikali wa kuhamia Dodoma; Nanukuu,

''Kuhamia Makao Makuu Dodoma

151. Chama Cha Mapinduzi kinatambua jitihada zilizofanywa na Serikali za
kuunganisha mji wa Dodoma na mikoa mingine kwa njia ya barabara za
lami. Aidha, baadhi ya majengo ya Serikali yameendelea kujengwa
Dodoma likiwemo jengo la Bunge, Benki Kuu, Hazina, Chuo Kikuu cha
Dodoma na Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba kwa ajili ya
makazi ya wananchi. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015-
2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo:-

(a) Kutunga Sheria itakayoutambua mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi;
(b) Kusimamia azma ya Serikali ya kuhakikisha majengo yote ya Wizara za Serikali
yanajengwa Dodoma badala ya Dar es Salaam; na
(c) Kuongeza kasi ya kupima viwanja kwa ajili ya makazi, viwanda na taasisi na
kuendelea kuiweka miundombinu ikiwemo maji, umeme na barabara.''

Kwa kuzingatia hilo, kwa nini viongozi wanashindwa kuwa wakweli na kuendelea kuaminisha umma wa Watanzania kwa mambo ambayo siyo kweli. Kimsingi hata sheria ya kutambua Dodoma kama Makao Makuu ya nchi haipo.

Nachelea kusema siku itakapofika kibao kitawageukia na hakika watatumbuliwa mchana kweupe
 
Huyu akamilishe kwanza barabara za jimboni kwake mana pesa alilamba mwenyekiti wake wa sasa alimwambia vipi nikutumbue mana fungu lilitoka afu sioni kilichofanyika,mama wa watu jasho likamtoka ndomana siku hizi anacheza kila step ambayo mwenyekiti anaitaka ilimradi amfurahishe ila huyu mama kiutendaji hana kitu kabisa ni mweupe
 
Nahisi ndio mmoja wa Mawaziri wakulupukaji na wanaopenda kujionesha kwa mkuu kuwa wapo pamoja nae na wanafanya kazi.
 
Back
Top Bottom