Je, umewahi kukutana na jini? Ilikuwaje? Njoo tusimuliane simulizi za kweli

Airmanula

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
3,527
5,756
Wanajukwaa!

Je, umewahi kukutana na MAJINI au JINI? Je ulifanyaje? Je mlikua marafiki, au walikutisha na kukuogopesha, je mliishi pamoja? Je umeshawahi kuzungumza nao? Basi kama ndio karibu tuambie hapa ilikuaje? Na ulifanikiwa kujitenga nao au bado unaishi nao/nae!

Huu uzi ni kwa yoyote yule aliyewahi kutana au simuliwa visa na matukio ya kukutana na MAJINI au JINI.

Mimi nakumbuka wa kwanza nilikutana nae nje ya jengo la kanisa, alikua amejifunika baibui mwili mzima, alikua anakuja uelekeo wangu akitembea kwa haraka sana, ajabu ni kwamba miguu ilikua kinyume, ila yeye anatembea kwenda mbele, niliogofya sana nikajua leo ndio naondoka leo naenda baharini, alivyonikaribia ghafla akabadilisha mwelekeo, akatokomea kwenye kundi la watu

Mwingine nikiwa nimekaa ufukwe wa bahari mojawapo hapa Tanzania, ghafla nikasikia harufu kali sana ya marashi ya kiarabu, kushoto kulia sioni mtu, nikajikaza nikasema ngoja nitamke maneno, nikasema " wewe jini nmekusikia harufu yako, tamu sana na inavutia marashi yananukia vizuri, jitokeze nikuone" ghafla mwili ukasisimka na nikasikia kicheko, nikakimbia!

Nilikutana na mwingine kwenye soko moja maarufu, nilienda kununua bidhaa flani, ile natembea nikaona mdada anakuja uelekeo wangu wakati namuangalia machoni ghafla yalijeuka kua ya bluu, nikawa namtazama hadi tukapishana, ghafla nikapata maumivu makali ya kichwa, wakat nashika kichwa niangalie nyuma sikumuona.

Karibuni!
 
Enzi hizo mshamba ni mlokole

Nilienda kwenye huduma ya nabiii flani, nikakanyaga mafuta

Ule usiku nilishtuka muda flani, nikaona kuna mdada flani mweupe kasimama karibu na kabati langu, hana kichwa, damu zinaruka ruka

Wee nikakimbia nikaenda kulala na bibi

Nyingine nimeenda kununua mkate asubuhi saa 12 kasoro, kuna shamba kubwa la migomba mahali, niliona mtu kavaa kanzu nyeupee ana upara, anatembea tu

Afu sikuwa mwenyewe, niliyekuwa nae alimuona pia.... Nikapotezea tu
 
ila humu ndani bhn
 
Attachments

  • IMG_20240510_111957_626.jpg
    IMG_20240510_111957_626.jpg
    151.5 KB · Views: 12

hizi stori kamsimulie Lucas mwashambwa
 
Enzi hizo mshamba ni mlokole

Nilienda kwenye huduma ya nabiii flani, nikakanyaga mafuta

Ule usiku nilishtuka muda flani, nikaona kuna mdada flani mweupe kasimama karibu na kabati langu, hana kichwa, damu zinaruka ruka

Wee nikakimbia nikaenda kulala na bibi

Nyingine nimeenda kununua mkate asubuhi saa 12 kasoro, kuna shamba kubwa la migomba mahali, niliona mtu kavaa kanzu nyeupee ana upara, anatembea tu

Afu sikuwa mwenyewe, niliyekuwa nae alimuona pia.... Nikapotezea tu
acheni kuangalia horror movies.
 
Sumbawanga Moja

Kipindi Cha mbala mwezi nimetoka kuangalia mechi ambayo Makolo wakikandwa 5 nayanga

Nikiwa busy kutembea ...nikaona nigeuke nyuma .... ghafla nakuta kivuli changu nimekiacha MITA kadhaa nyuma ....Anza kukimbia mbele ...chenyewe kimeganda tu..then nikaona Cha nikifuate ....nakuta kinanikimbia ... daaah nilichomoka mbio hizo
 
Story kama hizi utazikuta Africa na uarabuni tu. Nadhani ni kwakuwa kuna vichaa wengi maana 1 kati ya watu 4 ni kichaa, sasa vichaa kuna muda wana imagine vitu ambavyo havipo na wanaamini vipo.

Africa, Africa, Africa.
Mkuu unataka kuniambia kwa wenzetu(ulaya, marekani, jamii za wachina,wajapan,korea) hakuna visanga kama hivi?

Mbona tunasoma hivi vitu mara kwa mara, kuna movie based on true story zinahusu haya mambo.
 
Nilikua siamini habari za majini mpaka siku moja karibu na barabara ya hospital mida ya saa 11 alfajir nilipoona mbele yangu mwanamke mwembamba mrefuu ka wale wanaotembeleaga magongo ya kufanya wawe warefu kwenye michezo.

Sasa nilikua na pkpk yangu nimetoka hospital, baada ya kuona nikajipa ujasiri katika Yesu kwamba hakuna baya litanifanya, nilipo likaribia maana lilikua pembezoni mwa barabara kama vile linasubir usafiri, niliendelea kuvuta moto ghafra akawa mtu amebeba ukuni mmoja mrefu sana, nikasema potelea mbali aliye ndani yangu mkuu kuliko wewe jini.! Kwanza wewe ni duni sana unapaswa unikimbie.!

Hatari sana.!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom