Je, umeshawai Kuota ndoto upo shule unafanya mtihani ilihali shule ulimaliza kitambo?

Los santos

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,085
2,376
Nimekuta wadau mtandaoni wanalia kuwa Huwa wanaota ndoto wanafanya mitiani either necta form 4,shule ya msingi ,chuo au 6 ilihali hiyo hatua waliivuka kitambo sana ,hizi ni baadhi ya comments zao

1.Hiyo ni taarifa kuwa Kuna eneo kwenye maisha yako bado haujafaulu na hauja kamilisha kujifunza...na kukosa maandalizi maana yake Kuna jambo linakuja kwenye maisha yako na haujajiandaa...au Kuna nafasi inakuja kwenye maisha yako ambayo unahitaji kujiandaa kiakili kiroho na kifikra Ili uweze kuimudu

2. Hata sio mashetan, ubongo unatabia ya kurewind. Kuna siku utaota umebanwa na mkojo unahangaika ukojoe kama ile ya utotoni lakini ukiwa mkubwa huwezi kukojoa kweli kitandani, ila utotoni ilikuwa unakojoa kweli. Ko ukiona ubongo umerudisha cha nyuma mfano unafanya mtihani shuleni yatatokea yafuatayo
1. Ukakuta unafanya somo hukulipenda, huna cha kuandika ila wenzako waanaandika balaa
2. Ukiandika inakuwa ni kidogo tu hata haumalizi mtihani kabisa
3. Utaota umechelewa kufanya mtihani
4. Ukimaliza mara inatokea hujakusanya
5. Litatokea lolote la kuzuga zuga ili tu mtihani uonekane kama ni mazingaombwe tu ila unakuta unajiuliza mbona ni mtihan wa taifa huu au akili inakuja kujiuliza kuwa mbona huu mtihani niliufanya??

3. Hapo awali nilisumbuliwa saana na hii ndoto...lkn nikaja kupata tafsiri yake kutoka kwa mtumishi wa Mungu...akanitafsiria kuwa..hizo inakuwa ni nguvu za giza...ambazo mara nyingi...zinakuvuta kukurudisha nyuma ktk mafanikio yako...kuzuia maendeleo..ktk nyanja zote kiuchumi,kijamii na hata kisiasa

4. Nilimaliza chuo 2011 lkn mpaka sasa naota nipo chuo tena nafanya mtihani, cha ajabu sijawahi kukusanya wala kumaliza mtihani na ajabu kabisa wahuni ninaofanya nao mtihani sio wale niliokuwa nao chuo ni tofauti kabisa na wengine ni wahuni wa kitaa tu, wengine ni watu waliofanikiwa tayari lkn nipo nao paper.
Dah, haya maisha sio fare kabisa

5. Ubongo unafanya kazi yake ya kukumbuka mambo uliyofanya zamani ila kwakuwa ni muda mrefu uliopita inakuwa ni vipandevipande, ni kawaida ubongo kukumbuka mambo yaliyopita.

6. Haya mandonto sijui kwa Nini yanatokea, hata Mimi ilinitokea ndoto ya namna hiyo nilihangaika sana, yaani nilikuwa nahangaika kwenye mtihani huo, ilikuwa ni kuruka maswali halafu msimamizi Yuko nyuma yangu nikashindwa hata kupiga chabo kwa wenzangu. Watafiti wafanye tafiti za ndoto za namna hii, zinatutesa sana hadi tunakosa usingizi vizuri.

7. Hizo ndoto zipo ni kweli. Zinamaanisha unaishi nje ya mpango wa Mungu, hivyo kuna roho za kishetani zinaharibu mafanikio yako na mema yanayokuja mbele yako. Huwa inakubidi kutengeneza maisha yako na kumuomba Mungu ndio huja ndoto za mafanikio na matokeo huonekana ni kweli kabisa.

FB_IMG_1713700674037.jpg
 
Nimekuwa nikiota sana ndoto za namna hii, au mara nyingine nimekuwa nikiota tumefungua shule (boarding) ila muda wa kujiandaa kwenda darasani nagundua either suruali ama shati la shule halionekani au chafu.

Nimeona sababu nyingi ila hii hapa chini naona inamake sense hivi.

1.Hiyo ni taarifa kuwa Kuna eneo kwenye maisha yako bado haujafaulu na hauja kamilisha kujifunza...na kukosa maandalizi maana yake Kuna jambo linakuja kwenye maisha yako na haujajiandaa...au Kuna nafasi inakuja kwenye maisha yako ambayo unahitaji kujiandaa kiakili kiroho na kifikra Ili uweze kuimudu
 
Nafikiri ni kwa sababu pengine ni vitu ambavyo vilikaa kwa muda mrefu kwenye akili kwa kuwa necta ilikuwa ni mtihani wa kukuvusha kwenda sehemu nyingine... So zile moments za maandalizi yake pengine hufanya ubongo kuzirejea, Pia ukichunguza sana za mitihani zinakuwaga za ule mtihani wa mwisho kabisa uliomalizia level ya msomo, Kama uliishia class seven utaota necta ya class seven, kama ni form 4, utaota ya necta ya form 4.....
 
Africa Kuna vitimbwi vingi sana ,ila wengine wanasema ni ubongo kuchakata mambo ya zamani
Na mie nilijuaga hivyo ila baadae nikaja kushtuka maana ikitokea tu hio ndoto lazima kuna hali inabadirika na pia kuna upepo wa mambo unakua hauendi sawa ,nilipolipatia ufumbuzi hilo jambo hizo ndoto zikakata ila sasa zikawa zinakuja za aina nyingine
 
Nimekuwa nikiota sana ndoto za namna hii, au mara nyingine nimekuwa nikiota tumefungua shule (boarding) ila muda wa kujiandaa kwenda darasani nagundua either suruali ama shati la shule halionekani au chafu.

Nimeona sababu nyingi ila hii hapa chini naona inamake sense hivi.

1.Hiyo ni taarifa kuwa Kuna eneo kwenye maisha yako bado haujafaulu na hauja kamilisha kujifunza...na kukosa maandalizi maana yake Kuna jambo linakuja kwenye maisha yako na haujajiandaa...au Kuna nafasi inakuja kwenye maisha yako ambayo unahitaji kujiandaa kiakili kiroho na kifikra Ili uweze kuimudu
Mkuu hata mim hii point nimeikubali sana na inawezekana vijana tuna fursa sana ila hatujajiandaa kukabiliana nazo na mfano mzuri ni wanaozipata fursa tunaonaga vituko wanavyofanya mitandaoni ,mitaani etc kwaiyo kifupi watz wengi Wana baraka sema hatujui namna ya kuzihandle
 
Back
Top Bottom