Dębe tupu haliishi kufanya nini vile?Bado Miradi ilioanzishwa wakati tumepata Uhuru na kuendelea ni mingi sana nchi hii ukilinganisha na sasa hivi. Ila chakushangaza wakati huo wa utawala wa Baba wa Taifa hakuna hata project moja ilio itwa jina Nyerere.
Ni Juzi kati baada ya yeye kufariki ndio kidogo vitu vikaanza kuitwa majina yake.
Ila kuanzia awamu hasa ya Tano na hii ya sasa ni kila project wanataka iitwe majina yao, kila kitakacho anzishwa wanataka jina lao ndio litokelezee pale. Sasa je Nyerere alikuwa mashamba wa kiwango cha juu kabisa kuto kubali kutukuzwa? Kuto kubali vitu au mali za umma zipewe jina lake?
Kwa nini sasa hawa viongozi wa sasa wanataka kutukuzwa kupindikia na kuna chawa wanawachukulia kama ndio Mungu, viongozi wana sujudiwa kwa sasa.
Wanataka kujienzi wakiwa madarakani? waonekane kana kwamba walio tangulia hawakufanya chochote kile au walikuwa washamba sana?