Je, Makonda kuteuliwa kama mkuu wa mkoa kutoka kuwa katibu wa halmashauri kuu CCM taifa (itikadi na uenezi) amepanda cheo ama ameshuka?

Jan 28, 2024
97
133
jamiiforums-20240331-0001.jpg

Baada ya Makonda kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha leo hii, kumeibuka maswali na mijadala mbalimbali ikiwemo, Je amepanda cheo ama ameshuka?. Hapa nitajitahidi kieleza kadiri ya ninavyo fahamu.

Ipo hivi, katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na ana jukumu la kusimamia shughuli za serikali katika ngazi ya mkoa. Huyu yeye yupo kikatiba ya nnchi na ofisi yake imeanzishwa kupitia Ibara ya 61(1) ya katiba ya Jamuhuri ya wa Tanzania ,1977 (katiba) ambapo wakuu wa mikoa wa Tanzania bara huteuliwa na raisi wa nnchi baada ya kushauriana na waziri mkuu chini ya ibara ya 61(2) wakati wale wa Zanzibar wao huteuliwa na raisi wa Zanzibar baada ya kushauriana na raisi wa nnchi chini ya ibara ya 61(3) ya katiba.

Majukumu yake yake yapo katika ibara ya 61(4) ya katiba ambayo ni pamoja na kuhakikisha utulivu na usalama, kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, na kutoa mwelekeo wa juhudi za maendeleo katika mkoa. Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kiutawala na kisheria ambayo yanamwezesha kutekeleza majukumu haya.

Kwa upande mwingine, Katibu Mwenezi halmashauri kuu ccm ni kiongozi wa chama ambaye anahusika na kueneza itikadi na sera za chama na mmbo mengine kama yalivyo orodheshwa katika kifungu cha 108 (2) cha katiba ya CCM. Huyu yeye uteuliwa na halmashauri kuu ya CCM taifa kwakutumia katiba ya CCM. Hapa nitachambua kidogo.

Ni hivi,CCM kama ilivyo vyama vingine kinaendeshwa kwa vikao ambapo huanzia vikao vya chini kabisa (shina) mpaka taifa kama ilivyoelekezwa katika SEHEMU YA TATU ya katiba ya CCM. Na, maamuzi makuu (makubwa) kuhusu CCM hufanywa katika vikao vya taifa kama vilivyoonyeshwa katika kifungu cha 99 cha katiba ya CCM. Nikikao cha Halmashauri kuu CCM taifa ndio kikao muhimu zaidi kutokana na kazi zake zilizowekwa kupitia kifungu cha 103 cha katiba ya CCM ikiwemo kuandaa mkutano mkuu wa CCM taifa.

Hivyo basi, ni muhimu kuelewa kwamba Makonda alikua ameteuliwa na Halmashauri kuu CCM taifa na si raisi. Ingawa nafasi hii ni muhimu katika uendeshaji wa chama, haina mamlaka ya moja kwa moja katika utawala wa serikali kama ilivyo kwa Mkuu wa Mkoa. Kwaio ni vizuri kujua Makonda hakua kiongozi sa serikali bali wa chama. Na tukumbuke nnchi ina mihimiri mitatu ambayo ni Serikalini, Bunge na Mahakama, hivyo chama sio sehemu ya mihimiri ya nnchi.

Ukweli ni kwamba, Mwenezi ana nafasi muhimu na kubwa katika siasa za chama, Mkuu wa Mkoa ana wajibu mkubwa zaidi katika utawala wa umma na utekelezaji wa majukumu ya serikali.

Hata ivyo ni muhimu kuelewa tofauti hizi za kimamlaka na majukumu kati ya viongozi hawa wawili katika mfumo wa uongozi wa Tanzania. Ila tatizo la nnchi yetu ni kwamba chama tawala ndicho kinachounda serikali kuu.

Kwaio makonda kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa sikwamba amepanda cheo wala ameshuka bali amebadilishiwa majukumu, kutoka yale ya kichama na kuwa ya kiserikali, japo kwa jicho la siasa za Tanzania ni kama nguvu ya kimamlaka imeshuka.
 
Attachments

  • 2024-02-21 13_22_48_KATIBA YA CCM JAN 23 2023.pdf
    44.5 MB · Views: 3
  • KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SWAHILI VERSION[2000].pdf
    262.1 KB · Views: 5
Uenezi mawanda yake ni mapana pia ina ushawishi sana ndani ya chama... hapo habari za chama hasa wakati wa vikao muhimu nae atazisikia kwa wengine
 
Kupanda ama kushuka hiyo haijalishi kwa sisiem, kimsingi Makonda amepelekwa Arusha kimkakati na maandalishi ya 2025 ili akapambane na wapinzani kwa mtu wa kariba yake.
Lakini pia, hivyo ndivyo ameanza kurudishwa serikalini kupitia chama. Na ikiwezekana baada ya uchaguzi wa 2025 Makonda atateuliwa kua MB na kisha atalamba Uwaziri.
 
Uenezi mawanda yake ni mapana pia ina ushawishi sana ndani ya chama... hapo habari za chama hasa wakati wa vikao muhimu nae atazisikia kwa wengine
Ni kweli lakini uenezi ni uongozi wa chama wakati ukuu wa mkoa maana yake kaingia kwenye system ya uongozi wa serikalini
 
Kupanda ama kushuka hiyo haijalishi kwa sisiem, kimsingi Makonda amepelekwa Arusha kimkakati na maandalishi ya 2025 ili akapambane na wapinzani kwa mtu wa kariba yake.
Lakini pia, hivyo ndivyo ameanza kurudishwa serikalini kupitia chama. Na ikiwezekana baada ya uchaguzi wa 2025 Makonda atateuliwa kua MB na kisha atalamba Uwaziri.
😂😂Ni kama sisiemu wanacheza drafti, na ndo kashasogezwa selikarin
 
Kupanda ama kushuka hiyo haijalishi kwa sisiem, kimsingi Makonda amepelekwa Arusha kimkakati na maandalishi ya 2025 ili akapambane na wapinzani kwa mtu wa kariba yake.
Lakini pia, hivyo ndivyo ameanza kurudishwa serikalini kupitia chama. Na ikiwezekana baada ya uchaguzi wa 2025 Makonda atateuliwa kua MB na kisha atalamba Uwaziri.
Unahoja usikilizwe
 
Si ajabu akaletwa tena Dar!

Mapambio yote Yale ya mwenye nyumba, hawezi kuwa demoted kizembe hivyo!
 
Back
Top Bottom