Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,638
113,873
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali tuu, sio thread ya udini au ukabila.
  1. Je, kuna uhusiano wowote kati ya dini/kabila la mtu na ukakamavu ndani ya majeshi yetu nchini Tanzania?
  2. Je, kuna uhusiano wowote wa kati ya kabila la mtu na ukakamavu wa majeshini?
  3. Je, watu wa dini fulani au makabila fulani ni wazuri zaidi jeshini kuliko watu wa dini zingine au makabila mengine?.
Maswali haya ni kufuatia Mkuu wetu wa Majeshi wa sasa kufanya kazi nzuri iliyotukuka Jeshini kuliko wakuu wengine wote wa majeshi waliotangulia, ukiondoa wakuu wa jeshi walioongoza vita vya Kagera Tanzania tukashinda inawezekana huu uchapa kazi wa Mkuu wa sasa wa Jeshi letu unatokana na kutoka katika kabila la wachapakazi?

Katika kuwadurufu wakuu wetu wa majeshi waliotangulia, kuna kitu very strange nimeki observers na kukinote...

Wakuu hawa ni
  1. Jenerali Mirisho Sarakikya,
  2. Jenerali Abdalah Twalipo,
  3. Jenerali David Musuguri,
  4. Jenerali Ernest Mwita Kiaro,
  5. Jenerali Robert Mboma,
  6. Jenerali George Waitara,
  7. Jenerali Davis Mwamunyange,
  8. Na mkuu wa sasa wa majeshi yetu Jenerali Venance Mabeyo.
Majenerali karibu wote majina yao yana kiashiria ni majina ya dini fulani au ni watu wa dini fulani!. Kati ya majenerali hao wote 8, majenerali 7 wana majina ya Kikristo isipokuwa Jenerali mmoja tu, Generali Abdalah Twalipo ndio mwenye jina la mwanzo la Kiislamu. Tena huyu Generali Twalipo, nilisoma darasa moja na binti yake akiitwa Flora Twalipo ambapo jina la Flora pia ni jina la kishiria cha dini ya Kikristo, usikute hata jina la Abdallah ni jina tuu, na hayo ni majina mengine yote ni majina tu na haya uhusiano wowote na dini zao kama jina la Jaji Mkuu Saidi, Jaji Mkuu Ramadhani, ni majina tuu lakini wenyewe ni Wakristo, hivyo inawezekana ile Abdalah ni kama kwenye Anna Abdallah ni jina tuu la Kiislamu lakini mwenyewe ni Mkristo, au Jaji Ramadhani ni jina tuu la Kiislamu lakini mwenyewe ni Mkiristo au Rose Migiro ni jina tuu la Kikristu lakini mwenyewe ni Muislamu?.

Swali ni kwa muktadha wa nchi yetu Tanzania, ni secular state, haina dini, sasa kwanini majenerali karibu wote ni watu wa dini moja?. Je kuna uwezekano watu wa dini fulani ndio wazuri zaidi na wakakamavu zaidi jeshini kuliko watu wa dini nyingine ndio maana huko majeshini wengi huko majeshini ni watu wa dini fulani?, na ni kufuatia ukakamavu huo, hivyo ni watu wa dini hiyo ndio pekee kufikia kuwa majenerali?.

Kama jeshini tuna watu wa dini zote, na wote wana ukakamavu sawa, inamaana wanaopanda kufikia majenerali wangekuwa watu wa dini zote, lakini hali halisi ya wanao panda hadi kufikia top rank ya majenerali, kwa nini wengi wawe wa dini fulani hiyo hiyo?, kwani hao wa dini nyingine kwa nini hawawi majenerali?

Jee kuna uwezekano hao wanajeshi wa vyeo vya juu kutoka dini zote wapo lakini hawana sifa za ujenerali?. Au pia kuna uwezekano hao wanajeshi wa vyeo vya juu kutoka dini nyingine wapo na wanasifa zote za kuwa majenerali ila wanabaguliwa tuu kutokana na dini zao hivyo majenerali wengi kuwa watu wa dini moja?.

Na kwenye hii sampling ya majenerali wetu 8, tukija kwenye sampling ya wanatoka makabila gani, jee pia kuna uwezekano kuna makabila wachapakazi wanaoweza mitulinga ya Jeshini, na makabila mengine sio makabila ya watu wa kazi za mitulinga hivyo kwao kazi za Jeshini ni kituo cha polisi?.

Kwa nini watu wa makabila fulani fulani yuu ndio wajazane majeshini na kupata vyeo hadi kuwa majenerali? na wanajeshi wa makabila mengine wasiwe?.

Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya Muungano yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, sasa iweje Majenerali wote 8 ni watu wa kutoka upande mmoja tuu wa muungano, ina maana hakuna watu kutoka upande ule wa muungano wetu wenye sifa za kupanda hadi kuwa majenerali?. Yaani majenerali wote ni wa makabila ya bara tuu, yaani watu wa Pwani na visiwani hawawezi kupanda na kuwa majenerali?. NB. Hapa nazungumzia Jeshi, JWTZ na sio Polisi, kule polisi kuna ubaguzi wa urefu, watu wa makabila ya wafupi walikuwa hawaajiriwi polisi zamani.

Nauliza hivi makusudi ili baadae huko mbele ya safari, tusije kulaumiana, kati ya majenerali wote 8 wa jeshi letu, tangu tumepata uhuru, kuna majenerali watatu, sio tuu waliotoka mkoa mmoja, bali ni watu wa kabila moja!. Tanzania tuna makabila zaidi ya 120, kwanini majenerali watatu wajirudie kabila moja?

Kwa vile majenerali kuteuliwa na CinC, sasa ikitokea CinC ni mtu wa kabila fulani mfano mimi ndio nikibahatika kuwa CinC wa majeshi yetu, nami nikanote hakujawahi kutokea generalI wa kabila langu, jee kuna ubaya wowote nikafanya kiji affirmative action nikatafuta angalau kagenerali kamoja ka kabila langu?, hata kama rank ya huyo mtu wa kabila langu ilikuwa bado ni rank ya chini, kufikia kuwa generalI, nikamuongezea muda kidogo wa kustaafu jenerali aliyepo ambaye muda wake umekwisha, kisha nikampandisha vyeo chap chap jererali wa kabila langu, ili angalau na makabila mengine yatoe majenerali?

Na baada ya kumpata jenerali wa kabila langu, kiukweli kabisa hakuniangusha, amepiga mtulinga haswa na kufuatia good track record ya utekelezaji wake wa mambo makubwa, je kuna ubaya wowote ikiamuliwa kuanzia sasa, tuwe tunawajaribisha watu wa dini zote kwenye ujenerali na watu wa makabila yote kwenye ujenerali, ili kuupima uchapaji kazi wao, tukiisha jiridhisha kuna makabila ni wachapa kazi, then tunaamua kuanzia sasa, majenerali wote wa jeshi letu ni lazima wawe kutoka makabila fulani tuu ya wachapa kazi, angalau hata wafikie wawili, watatu kama lile kabila jingine, ndipo tuanze affirmative action jeshini kwa kuwajengea uwezo kwa kuwapandisha vyeo chap chap watu wa dini nyingine ambao hawajapata majenerali wa kutosha na kuwajaribisha watu wa makabila mengine kwenye vyeo vya juu, ili Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania, liwe ni jeshi la wananchi wote wa Tanzania, na wa dini zote na makabila yote kuweza kuwa majenerali?.

Nawatakia Jumapili njema ya matawi.

Paskali
 
Swali ni je kuna uwezekano watu wa dini fulani ni wakakamavu zaidi kuliko dini nyingine ndio maana wengi huko majeshini ni watu wa dini fulani?
No , historia ni mwalimu mzuri! Wakurya ni wezi wa ngombe na hivyo ni wakakamavu. Rais wa kwanza alitoka kwao/upande ule na hivyo kuwa influenced na ukakamavu wao kuwaweka jeshini! Dini inategemea nani alikwenda huko. Pwani Mwarabu/islamu ilitawala. Bara Yesu affiliantes walitawala.
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali
Jee Kuna Uhusiano Wowote Kati ya Dini na Majeshi?. Jee Kuna Watu wa Dini Fulani ni Wazuri Zaidi Jeshini Kuliko Dini Nyingine?.

Kufuatia Mkuu wetu wa Majeshi wa sasa kufanya kazi nzuri iliyotukuka Jeshini kuliko wakuu wengine wote waliotangulia, inawezekana huu uchapa kazi wake unatokana na kutoka kabila la wachapakazi?.

Katika kuwadurufu Wakuu wa Majeshi waliotangulia, kuna kitu strange nimekinote.

Wakuu hawa ni Jenerali Mirisho Sarakikya, Jenerali Abdalah Twalipo, Jenerali David Musuguri, Jenerali Ernest Mwita Kiaro, Jenerali Robert Mboma, Jenerali George Waitara, Jenerali Davis Mwamunyange, wa sasa Jenerali Venance Mabeyo.

Wote wana majina ya kiashiria ni watu wa dini fulani, isipokuwa mmoja tuu, Generali Abdalah Twalipo. Tena huyu Twalipo, mimi nilisoma darasa moja na binti yake akiitwa Flora Twalipo ambalo pia jina la kishiria cha dini fulani, usikute hilo jina la Abdalah ni jina tuu kama Anna Abdalah, au Jaji Ramadhani?.

Swali ni je kuna uwezekano watu wa dini fulani ni wakakamavu zaidi kuliko dini nyingine ndio maana wengi huko majeshini ni watu wa dini fulani?.

Jee ukakamavu nao una uhusiano na dini ya mtu.
Na jee pia kuna makabila wachapakazi wanaoweza mitulinga ya Jeshini, na makabila mengine kazi za Jeshini ni kituo cha polisi?.

Nawatakia Jumapili njema ya matawi.


P
Mkuu hebu jaribu kulinganisha watu wa dar na mwanza wapi wanafaa tuwatangulize mstari wa mbele kwenye vita utagundua watu wa mwanza ni wajasiri zaidi
 
Paskali una hoja,ila tutegemee mvua kubwa na matope punde tu!!

Nahisi chimbuko lilianzia kwa Nyerere kwa tukio hili......"Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi" ila muktadha wa wananchi huo ndio umejaa hao anaojaribu kuhoji Paskali,jumlisha na historia ya Mwlm kuingia TAA hadi TANU na waliomkaribisha!!!
 
Hakuna uhusiano kati ya dini na ukakamavu bali ulichokionesha ni namna gani dini inazingatiwa katika kuchagua hao mageneral katika jeshi, mfano mzuri watazame alshabab ni watu wa dini gani na tazama impact yao Somalia.
Hii haiwezi kutoa justification yoyote kwa sababu hata hilo jeshi la serikali linalotolewa jasho na Al shaabab ni wa dini ile ile kama ya hao Al shaabab
 
Back
Top Bottom