Japo vita vya Gaza vinakaribia ukingoni, Israel itaingia kidogo Rafah kuwaridhisha wahafidhina wa kiyahudi kama ilivyofanya baada ya kipigo cha Iran

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,449
11,417
Makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza baada ya miezi sita ya mapigano makali yamekuwa magumu kufikiwa baina ya Hamas na Israel.

Hata hivyo kutokana na kuelemewa kwa Marekani na Israel na upinzani juu ya vita hivyo sasa kuna dalili za kutosha kuwa ukaidi wa Benjamin Netanyahu umefikia kikomo na huku Hamas wakitumia fursa hizo kuonesha nia za dhati kutilaiana saini na Israel.

Huku uchaguzi wa Marekani ukikaribia upinzani juu ya vita vya Israel na Hamas umeongezeka miongoni mwa wabunge na wanasiasa na sasa umeanza kusambaa mpaka kwenye vyuo vikuu na vyuo vyengine vya elimu ya juu.

Kwa upande wa ndani ya Israel maandamano ya kumpinga Benjamin Netanyahu na kutaka vita viishe na kurudishwa mateka yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

Hali hizo zote zimepelekea kiburi cha Benjamin Netanyahu nacho kushindwa kuendelea akiona mbele yake hakuna tena namna ya kushinda vita kwa malengo waliyojiwekea na huku kukiwa na kitisho cha kuachwa mkono na mfadhili wake mkuu,Marekani.

Upinzani dhidi ya vita hivyo kwa kuangalia vifo na mateso ya wapalestina umevuka mabara na kuingia nchi mbali mbali ambazo karibu zote zinawaunga mkono Palestina.

Lakini huko nyuma Benjamin Netanyahu alikwishaahidi kuwa lazima ataingiza vikosi vya miguu huko Rafah kumaliza bataliani zilizobaki za Hamas.Katika chama chake kuna wahafidhina kadhaa ambao wanataka hilo litokee wakidhani ndio watakuwa wamewashinda Hamas.

Wakati huo huo kuna washirika muhimu kwenye baraza la vita ambao hawataki vita viingie Rafah wakitilia maanani kupatikana kwa mateka waliobaki kuwa ndio muhimu zaidi.

Hali hizo kinzani zinampa wakati mgumu waziri mkuu kuamua kipi kifanyike na huku viongozi wa Hamas baada ya kulegeza masharti nao wakionekana kuwa tayari kuachia mateka hao mara moja ilimradi madai yao muhimu yazingatiwe.Kuachiwa mateka ni moja ya sehemu itakayompatia Netanyahu kifuta machozi cha vita baada ya kushindwa kufikiwa kwa malengo mengine.

Tayari Hamas imepeleka wajumbe wake Cairo nchini Misri wakiwa na maagizo maalumu kutoka kwa kiongozi wa kijeshi ,Yahya Sinwar pamoja na maelekezo kutoka viongozi wengine wa kisiasa walioko nje ya Gaza.

Ikumbukwe Israel ilikuwa imeweka msimamo mkali dhidi ya Iran siku yoyote nchi hiyo ingejaribu kurusha silaha ndani ya maeneo yake.Hilo lilifanya baadhi ya watu kuamini Iran isingeweza kufanya hivyo na kwamba ilikuwa ikitafutwa tu ijiingize kwenye ugomvi ili ipigwe na iwe mwisho wa utawala wa nchi hiyo.

Israel ilijiamini kuupiga ubalozi wa Iran nchini Syria jambo ambalo katika mahusiano ya nchi ni kuipiga nchi nyengine kikamilifu.Shambulio hilo liliua makamanda wakubwa wa Iran ambapo Ina ran nayo iliahidi kulipiza kisasi.
Bila kutarajiwa na kwa kujiamini kweli Iran ililipiza kisasi kwa kupiga maeneo muhimu liyojichagulia ndani ya Israel.Inaonekana hata Israel hawakuamini kwamba Iran ilikuw na uwezo wa kupiga maeneo hayo.

Pamoja na kwamba inajulikana Israel ina uwezo mkubwa wa kijeshi,kilichofuata ni Israel kuamua kutoishambulia Iran kwa nguvu kwani kufikia hapo walijua na wao wangeshambuliwa kwa kiwango hicho hicho.

Hata hivyo kulikuwa na shinikizo ndani ya Israel la kurudisha kipigo ili isionekane wameshindwa na ili kuwaridhisha baadhi ya wahafidhina.Hiivyo Israel ikapiga kidogo Iran kwa kutumia silaha hafifu ambazo zilidondoshwa na Iran na hua ukawa ndio mwisho kwa mduara ule wa uhasama.

Tukija upande wa Rafah, ni kuwa Israel imeelemewa na vita na haijaweza kufikia malengo yake na inajua kuwa kwa kuivamia Rafah muda huu kutatibua upinzani zaidi dhidi yake ndani na nje na hasa kuharibu hali ya utulivu ndani ya Marekani huku uchaguzi wao ukikaribia.

Katika hali hiyo kumalizika kwa vita ni jambo la muhimu sana kwa Israel.Ndio maana ili kuwaridhisha wahafidhina wa kiyahudi ndani ya Israel na kwa vile ahadi ilikwishatolewa,basi Israel itatiliana saini na Hamas kumaliza vita na wakati huo huo itaingiza jeshi kupiga kidogo ndani ya Rafah na baada ya hapo itakuwa ndio mwisho wa vita.
 
Makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza baada ya miezi sita ya mapigano makali yamekuwa magumu kufikiwa baina ya Hamas na Israel.
Hata hivyo kutokana na kuelemewa kwa Marekani na Israel na upinzani juu ya vita hivyo sasa kuna dalili za kutosha kuwa ukaidi wa Benjamin Netanyahu umefikia kikomo na huku Hamas wakitumia fursa hizo kuonesha nia za dhati kutilaiana saini na Israel.
Huku uchaguzi wa Marekani ukikaribia upinzani juu ya vita vya Israel na Hamas umeongezeka miongoni mwa wabunge na wanasiasa na sasa umeanza kusambaa mpaka kwenye vyuo vikuu na vyuo vyengine vya elimu ya juu.
Kwa upande wa ndani ya Israel maandamano ya kumpinga Benjamin Netanyahu na kutaka vita viishe na kurudishwa mateka yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.
Hali hizo zote zimepelekea kiburi cha Benjamin Netanyahu nacho kushindwa kuendelea akiona mbele yake hakuna tena namna ya kushinda vita kwa malengo waliyojiwekea na huku kukiwa na kitisho cha kuachwa mkono na mfadhili wake mkuu,Marekani.
Upinzani dhidi ya vita hivyo kwa kuangalia vifo na mateso ya wapalestina umevuka mabara na kuingia nchi mbali mbali ambazo karibu zote zinawaunga mkono Palestina.
Lakini huko nyuma Benjamin Netanyahu alikwishaahidi kuwa lazima ataingiza vikosi vya miguu huko Rafah kumaliza bataliani zilizobaki za Hamas.Katika chama chake kuna wahafidhina kadhaa ambao wanataka hilo litokee wakidhani ndio watakuwa wamewashinda Hamas.
Wakati huo huo kuna washirika muhimu kwenye baraza la vita ambao hawataki vita viingie Gaza wakitilia maanani kupatikana kwa mateka waliobaki kuwa ndio muhimu zaidi.
Hali hizo kinzani zinampa wakati mgumu waziri mkuu kuamua kipi kifanyike na huku viongozi wa Hamas baad ya kulegeza masharti nao wakionekana kuwa tayari kuachia mateka hao mara moja ilimradi madai yao muhimu yazingatiwe.Tayari Hamas imepeleka wajumbe wake Cairo nchini Misri wakiwa na maagizo maalumu kutoka kwa kiongozi wa kijeshi ,Yahya Sinwar pamoja na maelekezo kutoka viongozi wengine wa kisiasa walioko nje ya Gaza.
Ikumbukwe Israel ilikuwa imeweka msimamo mkali dhidi ya Iran siku yoyote nchi hiyo ingejaribu kurusha silaha ndani ya maeneo yake.Hilo lilifanya baadhi ya watu kuamini Iran isingeweza kufanya hivyo na kwamba ilikuwa ikitafutwa tu ijiingize kwenye ugomvi ili ipigwe na iwe mwisho wa utawala wa nchi hiyo.
Israel ilijiamini kuupiga ubalozi wa Iran nchini Syria na kuua makamanda wakubwa wa Iran ambapo Iran iliahidi kulipiza kisasi.Bila kutarajiwa kweli Iran ililipiza kisasi kwa kupiga maeneo muhimu liyojichagulia ndani ya Israel.Inaonekana hata Israel hawakuwamini kwamba Iran ilikuw na uwezo wa kupiga maeneo hayo.Kilichofuata ni Israel kuamua kutoishambulia Iran kwa nguvu kwani na wao wangeshambuliwa kwa kiwango hicho hicho.Hata hivyo kulikuwa na shinikizo la kurudisha kipigo ili isionekane imeshindwa na ili kuwaridhisha baadhi ya wahafidhina.
Tukija upande wa Rafah ni kuwa Israel imeelemewa na vita na haijaweza kufikia malengo yake na inajua kuwa kwa kuivamia Rafaha muda huu kutatibua upinzani zaidi dhidi yake ndani na nje na hasa kuharibu hali ya utulivu ndani ya Marekani huku uchaguzi wao ukikaribia.
Katika hali hiyo kumalizika kwa vita ni jambo la muhimu.Hata hivyo ili kuwaridhisha wahafidhina wa kiyahudi ndani ya Israel na kwa vile ahadi ilikwishatolewa,basi Israel itatiliana saini na Hamas kumaliza vita na wakati huo huo itaingiza jeshi kupiga kidogo ndani ya Gaza halafu baada ya hapo itakuwa ndio mwisho wa vita.
Kama umeandika kimemko na kishabiki upande wa wafia dini
 
Pole ila Israel kairudisha Palestine yote mikononi mwake....hivi sasa gaza ni Israel
 
.hivi sasa gaza ni Israel
Screenshot_20240502-211040.png
 
Kipi ungependa kuona maana naona uko upande wa "ukinipiga umenionea"ukiniacha umeniogopa"
 
Kwa sasa huko gaza kuna vilio vya kila namna
Hamas waliomba vita Netanyahu kawapa vita kwa sasa kilio chao kimesikika dunia nzima hakuna msaada wowote kutoka kwa allah wala mnyaanzi wanafunzi wa huko Amerika ndio wanaandama ili kipigo cha mbwa koko kisitishwe huko gaza
Wale mashabiki wa Hamas hapa jf wamepoteana baada ya Hamas kupewa haki za katiba ya Israel anae kuanza mmalize.
 
Wale jamaa wa Resistance wamemwambia Netanyahu " Enter Rafa at your own risk " sasa sijui yatajirudia ya Gaza IDF kufungasha virago ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom