James Mbatia kumtuhumu Rais Magufuli kwa Ukanda: Anamlinganisha na nani?

Wiki hii wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Maliasili na Utalii, Mbunge wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro, James Mbatia, ambaye ni Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, alimtuhumu Rais John Pombe Magufuli kwa tamko lake kuwa, "Watu wa Kaskazini wasubiri kwanza."

Katika kujenga arguments zake, Mbatia alijaribu kuonyesha jinsi kodi zilivyo nyingi katika sekta ya utalii (57) na kwamba fedha za utalii zinazorudi kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kitalii ni ndogo na siyo 7% iliyopo kisheria. Mbatia alisifia juu ya mapato makubwa ya utalii kwenye TANAPA yatokanayo na Hifadhi tano zilizoko Kaskazini - Kilimanjaro, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na Serengeti.

Hakutaja maeneo mengine ya kiutalii ndani ya Nchi bali alitetea na kusifia ubora wa Ukanda wa Kaskazini kiutalii. Bahati mbaya hakumpa Rais Magufuli, the benefit of doubt, ukizingatia kuwa, Rais aliyasema hayo akiwa katika Ukanda wa pili kwa Utalii nchini - Iringa.

Kwa kuwa, CHADEMA ndio wamekuwa mstari wa mbele kumuita Rais Magufuli kuwa anapendelea watu wa Kanda ya Ziwa, nimelazimika kufuatilia Wizara Kivuli 18 za Kambi ya Upinzani Bungeni kuona jinsi Wabunge kutoka Kanda zote nchini wamezigawana. Majibu yalikuwa ifuatavyo:
  • Kanda ya Kaskazini - 15, ambapo Wenyeviti wa Kamati wana Wizara - 08.
  • Kanda ya Ziwa - 07, ambapo Wenyeviti wa Kamati ni - 03.
  • Nyanda za Juu Kusini - 05, Wenyeviti wa Kamati ni - 02.
  • Kanda ya Mashariki - 04, Wenyeviti wa Kamati - 00.
  • Kanda ya Zanzibar - 02, Wenyeviti wa Kamati - 02
  • Kanda ya Kati - 01, Wenyeviti wa Kamati - 01.
  • Kanda ya Kusini - 01, Wenyeviti wa Kamati - 00.
  • Kanda ya Magharibi - 01. Mwenyekiti wa Kamati - 01.
Ndipo hapo nimekuwa najiuliza: Hivi Magufuli kuitwa mukanda, mudini na mukabila, wanamlinganisha dhidi ya nani?




Naona umesahau hesabu za propotionality!!!
 
Mbona Chama Chenu cha CHADEMA ndo cha kikabila na kikanda miaka nenda rudi:
  • Mwenyekiti -Freeman Mbowe,
  • Katibu Mkuu - Dr. Slaa (hamkumuondoa bali alijiondoa mwenyewe)
  • Katibu Mwenezi (Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi) - John Mrema.
  • Mweka Hazina - Anthony Komu.
Wote hao wanataka Kaskazini na nafasi zao ndio hasa definition ya Chama, wengine kama Makamu Mwenyekiti nafasi zao hazina effects yoyote ya maana kwenye usimamizi wa rasilimali na uendeshaji wa operesheni za Chama. So ndio wanaokula hela.

kISHAKUWA CHANGU AU NDIO YALE YALE ASIYE UPANDE WAKO BASI YUKO UPANDE MWINGINE?
 
..Mh.Mbatia anadai Mlima Kilimanjaro umechangia serekalini zaidi ya 400 billion.

..halafu vijiji themanini na moja vinavyozunguka hifadhi ya mlima huo vimepewa 2.8 billion.

..kiwango hicho ni chini ya asilimia 0.48%.

..Jambo hilo siyo sawa. Halipaswi kutokea Kilimanjaro, Serengeti, Mikumi, Katavi, Gombe, Saadani, Ruaha, au popote pale Tanzania.

..nina wasiwasi mtoa mada hajasikiliza hoja ya Mh.Mbatia.
 
Mikoa iliyopo kaskazini mwa Tanzania ni Kagera, Simiyu, Mwanza, Mara, Arusha, kilimanjaro na Tanga
 
Kaskazini kwa sasa mtapumua maana alisema msubiri kwanza.

Nenda kwa amani Mh. Magufuli
 
Back
Top Bottom