Jaji Warioba: Yaliyotokea Uchaguzi wa 2019 na 2020 yakitokea tena Uchaguzi wa 2025 itakuwa ni mwanzo wa Vurugu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,879
12,133
Kongamano la Wadau kuhusu Wajibu wa Vyombo vya Habari katika Kuhakikisha Uchaguzi wa Kuaminika (Agenda for Stakeholders’ Conference on the Role of the Media in Ensuring Credible Elections), linafanyika kwenye Ukumbi wa New Dodoma Hoteli, leo Aprili 30, 2024

Snapinsta.app_440760340_1286766542288628_2314021663418549535_n_1080.jpg

Snapinsta.app_440694833_1476867326559903_8840315725747724887_n_1080 (1).jpg

Snapinsta.app_440699037_1485184785409277_2861604533382033862_n_1080.jpg

Baadhi ya Washiriki na ambao wanatarajia kuchangia mada katika kongamano la leo Aprili 30, 2024 ni:
  • Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu
  • Dr. Joyce Bazira, Mjumbe wa Bodi ya Uongozi Baraza la Habari la Tanzania (MCT)
  • Ernest Sungura, Mkurugenzi Mtendaji MCT
  • Matinyi Mobhare, Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa MAELEZO
  • Rosemary S. Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
  • Dr. Michael Anthony Battle, Balozi wa Marekani
  • Jenerali Ulimwengu, Media Consultant
  • Edda Sanga, Media Consultant
  • Pili Mtambalike, Media consultant and trainer
  • Maxence Mello, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums
  • Ludovick Utouh, Director Wajibu Institute
  • Engineer Andrew Kisaka, Principal Broadcast Engineer (Tanzania Communication Regulatory Authority -TCRA)
  • Zitto Kabwe, ACT- Wazalendo
  • David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi
  • Thabit Idarous Faina, Director Zanzibar Election Commission
  • Hamad Masoud Hamad, CUF Secretary General
  • Jacob Nyukuri Nyongesa, Senior Officer Research Planning and Strategy - Media Council of Kenya
  • Jennifer Thomas, Associate Professor, Department of Media, Journalism and Film, Howard University
  • Absalom Kibanda, Senior Editor
DODOMA: Waandishi wa Habari wanakutana katika Kongamano kujadili kuhusu tasnia ya Habari kuelekea katika Uchaguzi Nchini

Kongamano hilo linafanyika wakati #Tanzania ikijiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025. Pia, linashirikisha Wadau kutoka Vyama vya Siasa, Taasisi za Kiserikali na zisizo za Kiserikali

1714463091816.jpeg

photo_2024-04-30_11-22-44.jpg

Ernest Sungura (Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT): Hali halisi ya Uandishi wa Habari Nchini #Tanzania wakati wa Uchaguzi, Vyombo vya Habari mara nyingi huwa havina Maandalizi ya pamoja kuanzia hatua za awali hadi kwenye Uchaguzi wenyewe na hadi wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi.

Ernest Sungura (Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT): Uzoefu wangu unaonesha wakati wa Uchaguzi Vyombo vya Habari vya Tanzania vinajikita katika vitu ambavyo havina umuhimu

Kwa Lugha ya Mtaani tunaweza kusema ni ‘Media’ zinaelekeza nguvu kwenye ‘blabla flani hivi’, wanaangalia Maisha binafsi ambayo hayana uhusiano na athari kwa Wananchi moja kwa moja

Vyombo vya Habari vinakuwa vinadili na Wagombea ambao ama wamewapa posho au kuna lolote linafanyika ili wapate kula.

Ernest Sungura (Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT): Tunatambua kukua kwa Demokrasia Tanzania kunaendana na Uchaguzi wa Viongozi Kidemokrasia na kwamba Uchaguzi huu unahitaji Mazingira ya Haki, Uwazi na Uwajibikaji, Vyombo vya Habari vikifanya kazi kwa Weledi vinachagiza kuwepo kwa Haki, Uwazi na Uwajibikaji

Ni kwa msingi huo MCT tunaamini katika kaulimbiu ya Kongamano ambayo ni: Uandishi wa Habari za Uchaguzi kwa Weledi hujenga Usawa, Haki na Uwajibikaji
GMZXlbIWIAALxXb.jpeg

GMZXlbJX0AAMjTH.jpeg
Ernest Sungura (Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT): Vyombo vya Habari vya Tanzania huwa havina uelewa mpana wa viwango vya Kimataifa vya masuala ya Uchaguzi, Sheria na Kanuni mbalimbali za Uchaguzi, Mifumo ya usimamizi wa Uchaguzi Tanzania, uelewa mpana wa Sera, itikadi ya Vyama vya Siasa na ilani zao za Uchaguzi.

Ernest Sungura (Mkurugenzi Mtendaji (MCT): Nini MCT imekusudia kufanya? Kuviandaa Vyombo vya Habari mapema kwa kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa unaolenga kuvisaidia kufanya kazi ya kihabari ya kutoa taarifa sahihi kwa wakati sahihi (Information role), kufichua uovu na kuwajibisha (Watchdog role) na kuibua masuala ili yajadiliwe (Agenda setting role)

Kuratibu utafutaji na ukusanyaji rasilimali na kuvisaidia Vyombo vya Habari viwe na Uhuru wa Uhariri wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025. Ni matamanio ya MCT vyombo vya Habari Tanzania viwe na usafiri na posho zao wakati wa Kampeni badala ya usafiri na posho kutoka kwa Wagombea

Ernest Sungura, Mkurugenzi Mtendaji (MCT): Haki, Uwazi na Uwajibikaji katika masuala ya Uchaguzi yataletwa na Uandishi wa Habari za Uchaguzi unaozingatia Weledi na Maadili ya Kitaaluma. Hii ndiyo Kaulimbiu yetu tunapoelekea Uchaguzi
photo_2024-04-30_12-35-20.jpg
Matinyi Mobhare (Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa MAELEZO): Vyombo vya Habari vina wajibu mkubwa katika Jamii yoyote ambayo inapenda Demokrasia kwa kuwa vina uwezo wa kuelimisha na kuratibu Mijadala kwenye Umma

Tunapokaribia Uchaguzi jukumu la Vyombo hivyo linakuwa ni muhimu kwa kuwa kupitia wao Wananchi wanapata Habari na kuelimishwa jinsi ya kushiriki Uchaguzi ili kufanya Maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura yenye manufaa kwao

Matinyi Mobhare (Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo): Majukumu ya MCT katika kuendeleza Weledi, Maadili na Uwajibikaji katika Tasnia ya Habari, majukumu hayo ni muhimu katika Demokrasia inayostawi kama Tanzania, hivyo inapaswa kupongezwa, kwa nafasi yangu naelewa na kuthamini michango ya Vyombo vya Habari

Vyombo vya Habari vina wajibu wa kuripoti usawa na kuhakiki Habari kabla, wakati na baada ya Uchaguzi, hivyo ni nguzo muhimu kwa Demokrasia yetu
photo_2024-04-30_12-59-34.jpg
Msemaji wa Ubalozi wa Marekani, Kalisha Holmes: Akiwa katika Kongamano la Kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani, Kalisha Holmes amesema "Mitandao ya Kijamii imefanya baadhi ya mambo kuwa na nguvu kuliko tulivyotarajia, yamekuwa yakisambaa kwa kasi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma"

Ameongeza "Tumeingia katika nyakati ambazo Wananchi wetu wanahitaji kuelewa umuhimu wa taarifa ambazo zimehakikiwa, kwani chombo cha Habari kikiwa huru kinakwepa kulaghaiwa"

Warioba.jpg
Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu: Akihudhuria Kongamano la Kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi, Jaji Joseph Warioba amesema "Mara nyingi katika mchakato wa #Uchaguzi ndipo ambapo kuna changamoto, unaanzia wakati wa uandikishaji, ukiharibu hapo basi unaharibu Uchaguzi wote"

Amesema "Baada ya hapo hatua inayofuata ni mpangilio wa Vituo vya Kupiga Kura, nia ni kurahisisha na kumwezesha Mwananchi kufika kwenye kituo akapiga kura kwa Usalama na haraka"

Ameongeza "Uandaaji wa vifaa pia ni muhimu, siku ya kupiga kura kukiwa na dosari ya vifaa inaweza kuharibu Uchaguzi, Mfano; Kusababisha baadhi ya Watu kutopiga kura kwa upungufu wa vifaa au kuchelewea kufikishwa kituoni"

Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu: "Tunaelekea kwenye #Uchaguzi wa 2024 na 2025, tuliona kilichotokea 2019 na 2020, yakijirudia inaweza kuwa mwanzo wa vurugu. Tunakumbuka yaliyotokea #Zanzibar pia miaka ya nyuma, yasije yakajitokeza tena"

Akiwa katika Kongamano la kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi amesema "Mwaka 2020 Wagombea tuliowapeleka hatuwezi kusema walikuwa ni chaguo la Wananchi, tujitahidi tutumie taratibu ili kuwapelekea Wananchi wagombea ambao wanatambulika"

Ameongeza "Tusipofanya hivyo #Demokrasia haitakuwa ya ukweli, Demokrasia isiyozingatia maoni ya Wananchi hiyo siyo Demokrasia, tutakuwa tunajidanganya. Tusiwe CAG wa Uchaguzi, kazi yetu iwe kuchambua makosa ya Uchaguzi, tujenge Demokrasi ya kweli"

JENERALI ULIMWENGU.jpg
Akishiriki Kongamano la Kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi, Mwanahabari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu amesema "Chombo cha Habari cha Umma kama TBC kinatakiwa kuwa cha Umma, hakitakiwi kuegemea upande mmoja wa Kisiasa. Pili, hakitakiwi kuchukua matangazo ya biashara, kikifanya hivyo inamaanisha chombo ambacho kinaendeshwa kwa Kodi za Mwananchi kinaingia kwenye ushindani na Vyombo Binafsi, sio haki hata kidogo"

Pia, amesema Wakati wa Uchaguzi ni bora kuweka wazi msimamo wa Taasisi (Chombo cha Habari) kuwa ipo upande gani kuliko kufanya mambo kimyakimya na mwisho wake ni kukiuka weledi wa kazi

Ameongeza "Pia, kuna vyombo vya Serikali mfano Daily News, TBC, Habari Leo nakadhalika vinavyoendeshwa kwa fedha za Wananchi, vinakuwa sio vya Wananchi tena badala yake vinakuwa vya Serikali na hatimaye vinakuwa ni vya Mwenyekiti wa CCM"
Uli.jpg
Mwanahabari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu amesema kuwa Tume ya Jaji Francis Nyalali iligusia kuondolewa kwa baadhi ya Sheria Kandamizi, badala ya kuondolewa au kupunguzwa zikaongeka

Amesema "Jaji Nyalali alishauri mali ambazo zilikuwa chini ya Chama Tawala na zilichangiwa na Wananchi wote zirejeshwe kwa Wananchi, hilo halikufanyika (Mfano viwanja vya Chama)"

Ameongeza "Pia, aligusia uwepo wa Wagombea Huru, hilo halijafanyika badala yake lazima uwe chini ya Chama ndio uruhusiwe kugombea"


MAXENCE MELO (Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums): Miaka ya nyuma kulikuwa na mabadiliko ya Habari, Mwaka 2020 kuna ‘Malaika’ walitokea wakazima Mtandao, tunaamini hilo halitajitokeza Mwaka 2025

Watanzania wanategemea Wanahabari kuwapa habari, wasipozipata kutoka kwa Wanahabari watatafuta kwa njia nyingine ya kuzipata na hiyo itamaanisha Vyombo vya Habari kupoteza tunu ya taaluma yao

JENERALI ULIMWENGU (Mwanahabari Mkongwe): Uchaguzi wa Mwaka 2020, Wanahabari waliandaa Mdahalo wa Wagombea kwa kushirikiana na JamiiForums, sote tulitarajia uwe mkubwa licha ya Sheria kadhaa kupitishwa kwa wakati huo kwa lengo la kudhibiti mambo kadhaa, kilichotokea Saa 48 kabla ya Mdahalo walishuka ‘Malaika’ fulani na Mdahalo ukafa

Wananchi hawakujua kwa kuwa tulikuwa hatujatangaza lakini ilitupa wakati mgumu kutokana na jitihada zilizotumika kuuandaa
MAXENCE MELO.jpg
MAXENCE MELO (Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums): Mwananchi ana nafasi ya kufanya maamuzi ya mabadiliko kwa kushiriki katika uchaguzi, hilo linawezekana kwa kupiga kura

Pia, kwa ambao wanahitaji kupaza sauti lakini hawataki kujulikana, JamiiForums imewapa nafasi ya kufanya hivyo kupitia Jukwaa la #FichuaUovu, hapo wanapata nafasi ya kueleza hoja na mitazamo yao kwa nia ya kujenga bila kujulikana na hilo linafanyika bure bila utambulisho wao kujulikana ndani ya Tovuti ya JamiiForums.com

NEEMA LUGANGIRA (Mbunge): Mara nyingi Wanawake hawajitokezi kwenye Uchaguzi, hiyo inatokea ili kukwepa ukatili wa Kijinsia. Wanahabari wanatakiwa kuhakikisha wanalipigania hilo kwa lengo la kuwawezesha Wanawake wajitokeze kushiriki

NEEMA LUGANGIRA (Mbunge): Kuna matukio ya Ukatili wa Kijinsia kwenye Mitandao ya Kijamii, wakati mwingine hata kurasa rasmi za Vyombo vya Habari zinaweka Picha au Video ambazo zinaruhusu maoni mengi ya kudhalilisha Wanawake

Komenti zinatakiwa kufutwa lakini zimekuwa zikiachwa, hilo ni jukumu la Chombo cha Habari, Mtu anatakiwa apingwe kwa hoja na sio jinsia yake

NEEMA LUGANGIRA (Mbunge): Kuna suala la false news’ na ‘misinformation’, Wanahabari mnatakiwa kujipanga kuhakikisha Habari haitoki pasipokuwa na uhakiki wa hizo taarifa kwa faida ya kufanya Jamii ipate taarifa sahihi

Misimee.jpg
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema Mwandishi anatakiwa kutambua kuwa Usalama unaanza na yeye mwenyewe. Mfano; Akienda kuchukua Habari kwenye tukio la Uchaguzi anatakiwa kuzingatia mazingira anayoyakuta hasa ya kiusalama kabla ya kuendelea na majukumu yake.

Akishiriki Kongamano la Kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi amesema "Ni jukumu la Vyombo vya Habari kuwapa Elimu Waandishi wake kuhusu Mazingira ya Usalama pamoja na kuwapa vitendea kazi vya kujilinda au utambulisho"

Ameongeza "Mfano anapokuwa katika majukumu kisha kukatokea vurugu, mavazi yenye utambulisho Mfano ya neno “PRESS” yanaweza kumsaidia na kutambulika kirahisi"

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema "Jeshi la Polisi linazingatia kuwa hakuna aliye juu ya Sheria, iwe ni Mwanasiasa, Askari Polisi au Mwandishi wa Habari. Pia, tunaheshimu Haki za Binadamu, mfano Watu wana Haki ya kukusanyika na kujieleza"

Akiongea katika Kongamano la kujadili Tasnia ya Habari kuelekea Uchaguzi, Misime amesema "Tunapotimiza majukumu yetu kwa mujibu wa Sheria, Jeshi la Polisi linakuwa linamhakikishia Mwandishi wa Habari kufanya kazi yake kwa Amani na Utulivu"
 
Back
Top Bottom