ITV/EATV/Channel TEN & STAR TV HAZIPO HEWANI KTK DISH

AljuniorTz

JF-Expert Member
Jan 6, 2009
544
17
Nawataka radhi km nimerudia post

Naomba kama mtu anafahamu hizo chaneli tajwa hapo juu iwapo wahusika wamebadilisha Frequency zao kwa wale wanotumia Satellite Dish.
Ilianza kupotea channel TEN, ikafuata Star TV na kuanzia last week ITV/Capital na EATV(wote wapo pamoja), hazipo hewani. Sina hakika km wamehamia ktk digital broadcasting ama ni vipi; nimetembelea website zao hamna lolote la maana zaidi ya habari za siku nyingi zilizopita...
Nitashukuru kwa yeyote mwenye taarifa
 
kuna thread iliyokuwa inasema hili ndilo jibu walonipa mafundi wa ITV, inasemekana kuwa wamehamia intel sat na kuwapata unatakiwa uwe na dish la ft 8, kama vp fuatilia maana wataalamu walitoa michango mingi.
 
hizi channel hazija badilika tatizo kubwa tunauziwa madish feki madishi mengi ya futi sita ni feki yanafanya kazi kipindi cha mwaka mmoja mwaka wa pili yanaanza kukata channel moja moja tuwe makini sana tunapo nunua haya madish ya futi sita kuna feki na original na siku hizi ukienda dukani wanakwambia bei tofauti ya feki na original kama unataka kujua frequency za ITV,TBC, na nyenginezo ingia hapa Intelsat 906 @ 64° East Intelsat 906 @ 64° East - frequencies - freq - channels - packages :: TrackSat.com
 
Nawataka radhi km nimerudia post

Naomba kama mtu anafahamu hizo chaneli tajwa hapo juu iwapo wahusika wamebadilisha Frequency zao kwa wale wanotumia Satellite Dish.
Ilianza kupotea channel TEN, ikafuata Star TV na kuanzia last week ITV/Capital na EATV(wote wapo pamoja), hazipo hewani. Sina hakika km wamehamia ktk digital broadcasting ama ni vipi; nimetembelea website zao hamna lolote la maana zaidi ya habari za siku nyingi zilizopita...
Nitashukuru kwa yeyote mwenye taarifa

Mkuu hili ni tatizo hasa kwa wale watumiao dish la futi 6. Mimi ni mmoja wa wahanga, niliamua kubadili dishi na kuweka la futi 8, kwa kweli sasa home amani tele, maana sehemu kubwa ya familia ni wapenzi wa itv,eatv,capital na star. Pamoja na hayo, ukuaji huu wa teknolojia(toka mfumo wa analogue kwenda mfumo wa digital) utatuacha solemba,maana nimesikia watu wanasema haya madishi makubwa hayatakua tena na nafasi (sina uthibitisho katika hili).
 
achaneni na madish bana.pata digital box ya Easy TV Local channel zote unapata crystal clear.madish tuwaachie wanaokaa mikoani
 
We inkos unadhani easy tv wako nchi nzima? hapa tunaongelea watu wa mikoani wanaozipata chaneli hizi kwa njia ya satelite.
 
thanx xana fatma,the web imenitoa sana leo,nimejizolea maujiko kwa watu leo,,,,,,,,thnx once again
 
achaneni na madish bana.pata digital box ya Easy TV Local channel zote unapata crystal clear.madish tuwaachie wanaokaa mikoani
Hongera zako unayekaa Jijini! Mikoani hatuishi kwa chips za mihogo wala juice za ukwaju!
 
Usikate tamaa wakati mwingine ni deflection ya dish tu. Jaribu kufanya hivi:Washa TV yako, weka channel isiyoonekana,kisha nenda kurekebisha dish lako kwa kulegeza ile screw iliyo nyuma ya dish na kupandisha kidogo sana, labda kwa milimita huku mtu mwingine akikujulisha kuhusu maendeleo(hata fundi si lazima). Channel zikirudi kaza hiyo screw, endelea na maisha. Ikishindikana basi kuna tatizo kubwa. Lakini naamini kwa 100% kuwa utafanikiwa.
 
Ni kwambie? Wewe ni miongoni mwa viumbe wachache kwenye hii dunia waliozaliwa kwa faida!! Asante kwa MSAADA mkubwa Fatma.
 
Back
Top Bottom