Itakuwaje wafuasi wa CHADEMA wakijipeleka polisi ili watiwe maabusu baada ya maandamano?

Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
808
704
Nimewahi kusimuliwa kisa kimoja nikiwa kijana ambacho kilitokea maeneo ya Tukuyu enzi za Nyerere wakati wa mfumo wa ujamaa (Wanaokifahamu watanisahihisha). Kipindi hicho hakukuwa na maduka ya watu binafsi na watu walipata mahitaji yao kupitia maduka ya ushirika.

Kisa chenyewe ni kwamba kulikuwa na uhaba wa bidhaa katika madukaya ushirika na baadaye makamu wa raisi Abdul Jumbe alipanga kutembelea Tukuyu.Kabla ya ziara hiyo vitu vikafurika madukani. Jumbe alipofika watu walighadhabika sana mbele ya mkutano na kutukana kwa jinsi wanavyopata shida ya bidhaa na baadaye walipoona yeye anatembelea huko vitu vikaletwa madukani.Ikatokea fujo na ikabidi FFU waitwe na kuwakamata baadhi ya watu na kuwapeleka gereza la Ruanda Mbeya mjini. Wananchi waliobaki waliamua kupanda mabasi na kujipeleka wenyewe gereza la Ruanda na kuwaeleza kuwa tufungeni na sisi kwani si hao tu mliowakamata (tulikuwa pamoja).

Kwa kweli ni kisa cha ajabu kwani wananchi walionesha mshikamano wao kwa jambo lililokuwa linawagusa na kuwaumiza. sielewi kama watanzania wa leo wenye kuridhika na familia zao pasipo kuitazama jamii nzima wanaweza kufanya hivyo.

Swali langu ni Je CHADEMA wakiamua kuandamana kwa amani kwa kushika matawi ya miti na baadaye baadhi wakakamatwa (Let say viongozi na wengine), na baadaye wafuasi wote wa CHADEMA wakaondoa woga na wakajipeleka wenyewe polisi kwa makundi makubwa na kuwaeleza kuwa tulikuwa pamoja na mliowakamata kwa hiyo tufungeni na sisi, hizo mahabusu/magereza zitatosha? Ni swala kama la kufikirika lakini likitokea linaweza kusababisha "kitu cha ajabu" katika nchi kwani polisi na watawala watashikwa na butwaa na pengine polisi watajikuta kwamba ni wachache kuliko hao watu wanaotaka kufungwa.
 
Ndiyo maana tunasema suala hili ni la maridhiano tu na si ubabe. Mahabusu zetu haziwezi kutosheleza kufunga wafuasi wote wa CDM.
 
Hahaha,hii kali.
Unajua mahabusu wanapelekwa SEGEREA,sasa mambo ya kuliwa kiboga ndio issue.
Wakitoka tuwakague,kuna manyapara yamepinda kule.
 
Back
Top Bottom