Israeli SI taifa teule TENA. (Fact)

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,417
7,036
Habari za muda!

Kwa mujibu wa maandiko, Mungu alilichagua taifa la Israeli kama taifa lake teule, akilipa amri zake kwa njia ya maagano, ili wazifuate na wasiziasi.

Pamoja na hayo, Israeli waliasi mara nyingi. Bado Mungu alikuwa na imani nao, akawapelekea agano tena kupitia Yesu Kristo, bado wakamkataa.

Hapo Mungu hakuwa na budi ila kuuhamisha ufalme na kuupeleka taifa jingine. Uteule wa taifa la Israeli uliondoka punde baada ya kumkataa Yesu na kumtoa ili asulibishwe na Pilato.

Israeli ya kimwili ilishaisha, kwa sasa, Mungu anamuhesabu ni Myahudi mtu yeyote anayeamini Yesu ni BWANA kwa kukiri kwa kinywa. Hii ndiyo Israeli ya kiroho, ambayo Mungu yupo nayo.

Israeli ya kimwili imekufa ni taifa kama mataifa mengine tu, si wateule TENA wa Mungu.

Regards!
 
Ni kweli kabisa, Katika mwaka wa 33 W.K., taifa la asili la Israeli liliacha kuwa taifa teule la Mungu wakati lilipomkataa Masihi, ambaye ni Mwana wa Mungu.

Masihi mwenyewe alisema hivi: “Yerusalemu, Yerusalemu, muuaji wa manabii na ambaye huwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwake . . . Tazama! Nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” (Mathayo 23:37, 38).

Maneno ya Yesu yalitimizwa mwaka wa 70 W.K., wakati majeshi ya Roma yalipoharibu Yerusalemu pamoja na hekalu na ukuhani wake.

Ndiyo maana Yesu aliwahimiza wanafunzi wake kuhubiri habari njema Sehemu mbalimbali mbali na Pale Israelna "Basi, nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu" Mathayo 28:19

"Hii habari njema ya ufalme itahubiriwa katika dunia yote inayokaliwa ili kuwa ushahidi kwa mataifa yote; na ndipo ule mwisho utakapokuja.”—MATHAYO 24:14.
 
Kama ni fact basi ni proved Mungu wa wanaisreal anasapot ushoga
Hapo unaitukana mpaka dini yako... maana ukristo na uislamu vyote vimetokea kwenye uyahudi.. kina Musa na wengine wote wa design hizo dini yao ni JUDAISM
 
Mungu mnasema aliteketeza sodoma kwa ushaga , mbona hao wanaufanya hawapati adhabu?
Watapata tu, sheria inasema tusimuhukumu mtu kwakosa ambalo halikuwepo wakati linatendeka,hivyo kama wanafanya sasa na sheria inawakataa , wataadhibiwa tu
 
Ukweli ni kwamba zama hizi hakuna miujuzi wala hukumu za hapo kwa hapo .
 
Kama ni fact basi ni proved Mungu wa wanaisreal anasapot ushoga
Sasa ushoga na Mungu na kusupport Israel mbona hakuna connection kiongozi.

Aya,Zanzibar kuna mapapai kibao ambao sehemu kubwa ni waumini wa dini ile ya mtume(kwahiyo tuseme pia naye Mungu wao anafavor upimbi sio?).Hii sio nzuri unaweza kuweka hoja zako bila kuwa hivi na ukaeleweka.

Mapapai yamejaa karibia kila nchi(si nchi zenye misimamo ya kidini au zisizo tambua dini au Mungu).Mtu kuwa papai ni jambo la malezi.Kikubwa mtunze mwanao wa kiume na muombe Mungu amkinge na hiki kikombe basi
 
Habari za muda!

Kwa mujibu wa maandiko, Mungu alilichagua taifa la Israeli kama taifa lake teule, akilipa amri zake kwa njia ya maagano, ili wazifuate na wasiziasi.

Pamoja na hayo, Israeli waliasi mara nyingi. Bado Mungu alikuwa na imani nao, akawapelekea agano tena kupitia Yesu Kristo, bado wakamkataa.

Hapo Mungu hakuwa na budi ila kuuhamisha ufalme na kuupeleka taifa jingine. Uteule wa taifa la Israeli uliondoka punde baada ya kumkataa Yesu na kumtoa ili asulibishwe na Pilato.

Israeli ya kimwili ilishaisha, kwa sasa, Mungu anamuhesabu ni Myahudi mtu yeyote anayeamini Yesu ni BWANA kwa kukiri kwa kinywa. Hii ndiyo Israeli ya kiroho, ambayo Mungu yupo nayo.

Israeli ya kimwili imekufa ni taifa kama mataifa mengine tu, si wateule TENA wa Mungu.

Regards!
unataka kumchokoza aya-tollah
 
Back
Top Bottom