Iringa: Ahukumiwa kunyongwa baada ya kumbaka na kumuua Mke wa Mtu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,482
8,336
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Mwanaume aitwaye Mohamed Njali kwa kosa la kumbaka na kumuua kwa kumkaba Atika Chesco Kivanule (24) September 25, 2022 saa saba usiku wakati Mumewe akiwa kwenye banda la video kutazama pambano la ngumi la Mandonga vs Salim Abeid lililofanyika Mkoani Mtwara.

Katika kesi hiyo ambayo ilisimamiwa na Mawakili wa Serikali WinFrida Mpiwa na Muzna Mfinanga na kutolewa hukumu na Jaji wa Mahakama Angaza Mwipopo, Mahakama imesema siku ya tukio hilo Mshtakiwa alivunja mlango na kuiba simu pamoja na suti na baadae kumbaka Atika na kumkaba shingoni.

Adeline Kileo ambaye ni Mume wa Marehemu ameishukuru Mahakama kwa adhabu iliyotolewa dhidi ya Kijana huyo Mohamed Njali.
 
Mume wake aliongea kwa uchungu sana,maana wakati wa purukushani za kubaka mpaka kumuua kuna mtoto wake mdogo alishuhudia,anasema hio ilimtesa sana mtoto mpaka kukaa sawa
 
Back
Top Bottom