Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,770
- 41,630
Usiku wa Jumamosi, tarehe13 April 2024, Iran iliishambulia Israel kwa makombora mbalimbali na drones 300, huku mitambo ya Israel, Marekani, Uingereza na Jordan, ikidaka zaidi ya 99% ya makombora yote, na karibia yote yakitunguliwa kabla ya kuingia anga la Israel. Machache yaliyofanikiwa kutua Israel yalileta uharibifu mdogo ikiwemo kumjeruhi binti wa umri wa miaka 14 ambaye alijeruhiwa na vipande vya drones iliyotunguliwa akiwa angani.
Shambulio hilo linafuatia shambulia la Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Iran lililoua makamanda wawili wa ngazi ya juu kabisa wa jeshi la Iran, pamoja na maafisa wengine 11. Israel ilidai kuwa jengo hilo halikuwa ubalozi mdogo bali linatumiwa na makundi ya wapiganaji wanaoishambulia Israel wanaosaidiwa na Iran.
Kufuatia shambulio la jana, mataifa mengi yamelaani shambulio hilo na kuomba utulivu, huku mataifa karibia yote tajiri Duniani, yakisema kuwa yanasimama na Israel, yakiilaani Iran kuwa ndiyo chanzo cha migogoro Mashariki ya kati likiwemo shambulio la tarehe 7 October 2023 dhidi ya Israel lililozaa maafa makubwa yanayoendelea dhidi ya Wapalestina. Mataifa yenye uchumi mkubwa Duniani yamekutana jana juu ya hatua za kuchukua dhidi ya Iran, huku Israel ikiendelea na vikao kuamua hatua za kuchukua dhidi ya Iran. Waziri Mkuu wa Israel amesema kuwa Jeshi la Israel ni imara, wananchi wa Israel ni imara, na wanaishi kwa falsafa moja kuwa anayetishia usalama wao watamwangamiza.
Mara baada ya shambulio hilo, sarafu ya Iran imeporomoka ghafla kwa speed ya ajabu, ambapo sasa dollar moja inabadilishwa kwa rial 660,000, huku wananchi wengi wakihangaika kubafilisha pesa zao ili wazitunze katika sarafu za kigeni.
$1 = 660,000 Rial!!!
Tunasema shilingi yetu ni dhaifu, sijui hii ya Rial ya Iran, itaitwaje!!
Iran's Rial Dips to All-time Low Against US Dollar
The Iranian Rial continued its downward spiral on Saturday amidst escalating tensions with Israel and concerns of a potential war.
The US dollar surpassed the 660,000-rial mark for the first time on the open market.
With an annual inflation rate reaching about 50 percent, Iranians have been scrambling to convert their savings into hard currencies or gold.
The Rial's decline intensified following the recent Israeli attack on Iran's consulate in Syria and subsequent tensions between the two nations.
The Iranian government has yet to offer a public explanation for the sharp decline of the Rial.