Intel wazindua generation ya 8 ya CPU zao

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,844
40,203
Intel leo wamezindua generation ya nane ya CPU zao itakayojulikana kama kabylake refresh, kwa sasa wamezindua CPU za laptop tu, uzinduzi wa desktop na tablets utafuatia baadae.

Kwa wale wanaofuatilia mambo ya CPU kuanzia generation ya 2 mpaka ya 7 cpu zote zilikuwa zikifanana mpangilio wa core, kwenye laptop kuanzia i3 mpaka i7 zilikuwa ni core 2 na thread 4, (mainstream laptop sio high perfomance zenye quad core).

Ila kwenye hii 8th generation mambo yamebadilika, kwa cpu za i5 na i7 ambazo zimezinduliwa zote zitakuwa na core 4 na thread 8, japo base clock zimeshuka lakini turbo clock zimeongezeka.

8th_gen_overview_near_final-page-017.jpg


Ukiangalia hio picha utaona kuna i7 yenye core 4 na thread 8 na inaboost hadi 4.2ghz kwa umeme wa 15w tu.

Hii itakuwa ni upgrade nzuri sana, laptop mpya zitakuwa na nguvu mara mbili au zaidi ya sasa, tutegemee software na games mpya zitakazotoka miaka ijayo kutocheza kwenye laptop zetu za sasa.

Kwa updates ya CPU nyingine nitazi-update baadae.
 
Technology inazidi kusonga mbele angalia mfano wa simu za miaka 4 iliyopita nyingi zinashindwa kurun baadhi ya games zenye GB 1 nakuendelea
 
Tia kipicha wengine huku tunaelewa kwa picha maana tu wakina Marxist..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom