Inonga anaiheshimisha NBC Premier League

Gwele

JF-Expert Member
Jun 7, 2016
2,298
2,857
Ukweli uwekwe wazi tu kuwa uwepo wa Inonga kwenye ligi yetu ya NBC premier League kunaipa heshima sana ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa mchezaji wa ligi yetu kucheza nusu fainali ya Afcon toka kuanzishwa kwake

Kwa hili nipeleke sifa za moja kwa moja kwa kamati ya usajili ya klabu ya Simba kwa kukileta hiki chuma kwenye ligi yetu, ni fahari kuwa nae na kila mtanzania mpenda soka ni vyema kujivunia uwepo wake kabla hajaondoka kwenye hii ligi

Inonga kwa sasa amekuwa nembo na kielelezo cha ubora wa ligi yetu, hivyo kama mtanzanzania mpenda soka popote ulipo bila kujali timu unayoshabikia unaweza kutembea kifua mbele kwamba tuna mtu kwenye nusu fainali za Afcon na probably anaweza kurudi nchini akiwa mshindi wa michuano hiyo

Ikumbukwe vipo vilabu vingi tu nchini vilivyojaza wacongo lakini hata tu kuitwa kukaa benchi kwenye kikosi cha Congo kama ilivyo kwa mchezaji wa Pyramid Fiston Kalala Mayele wameshindwa hiyo inaonyesha ni kwa namna gani ni wachezaji wa viwango duni.

Na hii pia ni somo kuwa quality ina matters zaidi kuliko wingi wa wachezaji zipo klabu zilizokuwa zikijisifu kuwa na wachezaji wengi kwenye michuano hii ya Afcon lakini mpaka muda huu hakuna hata mchezaji mmoja aliyesalia huko pamoja na wingi wao aliyejitahidi sana aliishia robo fainali na kilicho amua hayo yote ni quality zao tu.
FB_IMG_1707033041975.jpg
 
Inonga hatabakia Simba msimu ujao vinginevyo Simba ipasuke haswaa
 
Simba ina maono sana ila inakwamishwa na UTOPOLO kwà ulozi
Ukumbuke kuwa klabu ya Simba inatambuliwa na CAF kama klabu Kiongozi Katika maswala ya kishirikina barani Afrika.

Hii Ina thibitishwa na baadhi ya wachezji wa klabu iyo kulalamika kwa watu wao wa karibu kuwa vitendo vya kishirikina vime kithiri kiasi Cha wachezaji aki fua/Fanya usafi, ahakikishe analinda nguo au vifaa vyake mpaka vinapo kauka ili kuepuka wachezji wachawi ku kwapua na kwenda kuvifanyia ushirikina.

Uongozi wa klabu iyo umejipambanua zaidi baada ya hivi karibuni ku ukataa uwanja wa Azam complex kwa madai hawapati matokeo kwakua uwanja wa Azam una mazingira magumu kwao kupata ushindi kupitia njia za kishirikina.

Lakini Ime fahamika kua Azam hawataki uwanjawao uchimbwe na kufukiwa makafara na klabu iyo ya msimbazi kama ilivyo fanikiwa ku uharibu uwanja wa Benjamin Mkapa na kupelekea nyasi za uwanjauo kukauka na kuonekana kama zilizo pigwa na radi.
Hali iyo inafanya viongozi wa Simba kuona wananyimwa haki Yao ya msingi katika vitendo hivyo vya kitamaduni.
 
Mnataka sana tutumie Chamanzi kuna nini metuwekea ndugu zetu wananchi?
 
Simba ina maono sana ila inakwamishwa na UTOPOLO kwà ulozi
Hili ni kweli kabisa Ulozi na mipango mipango ya nje ya uwanja ndio inawapa uto jeuri ya kukaribiana na Simba ila vingnevyo ni timu mbili tofauti kabisa, Simba ina viongozi wenye maono ya mpira
 
Na hapo ndipo mnapolikosea heshima mchezo wa mpira wa miguu, mna matatizo kwa wachezaji wenu, scouting na viongozi wenu ila lawama wanapewa Yanga kwa kuwalogea uwanja.
Simba imecheza michezo nane ya kimataifa msimu huu lakini imeshinda mechi moja pekee.
Imecheza michezo minne away na haijashinda mechi hata moja, je hao uto waliwafiata hadi huko nje ya mipaka ya Tanzania kuloga viwanja?

Mechi mlizoshinda za ligi, uchawi wa uto uwanjani ulikuwa wapi hadi mshinde?
 
Simba walivyo mapimbi wanauza mchezaji kama huyu, unapotaka kuwa timu nzuri, bakiza wachezaji wako bora inapotokea kuuza uza kwa timu ambayo ni bora zaidi yaani hadhi ya timu inakufanya usiweze mzuia mchezaji.
Kwa miaka ya karibuni far rabat na simba, simba ni kubwa. Simba ilipofikia inabidi iporwe mchezaji na mamelodi, wydad, al ahly huko. Kibaya zaidi wameuza bei ya kawaida tu.
 
Na hapo ndipo mnapolikosea heshima mchezo wa mpira wa miguu, mna matatizo kwa wachezaji wenu, scouting na viongozi wenu ila lawama wanapewa Yanga kwa kuwalogea uwanja.
Simba imecheza michezo nane ya kimataifa msimu huu lakini imeshinda mechi moja pekee.
Imecheza michezo minne away na haijashinda mechi hata moja, je hao uto waliwafiata hadi huko nje ya mipaka ya Tanzania kuloga viwanja?

Mechi mlizoshinda za ligi, uchawi wa uto uwanjani ulikuwa wapi hadi mshinde?
Yaani timu inayosajili Inonga na Che Malone ina scout mbovu ila inayosajili Gift Fred na Doumbia hao ndio hawana shida kwenye scouting?
Ndio maana nikasema ni ulozi tu na mipango ya nje ya uwanja hivi mchezaji kama Mzize,Musonda au Max wana uwezo gani kiuhalisia wakumsumbua beki kama Inonga au Zimbwe Jr we unadhani ni kawaida ile

Hao Yanga unaosema wanafanya vizuri kimataifa wapo makundi hapo wamecheza michezo minne sawa na Simba nikuulize wamekusanya point kumi na ngapi?
 
Dah Mzee umemchana mbaya mbovu .........
 
Kwahiyo Inonga na Che Melone ndio wachezaji pekee uliowaona mmesajili? Unataka tuanze kufungua makaburi yenu humu mkiwa mnalalamika kuhusu kusajili magarasa?

Kama uchawi unafanya kazi, timu zisingekuwa zinasajili wachezaji bali waganga wa kienyeji. Ni taifa gani au timu ipi iliyofanikiwa kuchukua kombe kwa uchawi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom