Ijue minara kumi ya kuvutia mirefu zaidi duniani

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,539
Kwa nchi za Kiafrika suala la kujenga minara kama utambulisho wa jiji na kivutio cha utalii au kurushia matangazo ya redio na televisheni halipewi kipaumbele .
Pia inaonekana kama matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
Dikteta Mobutu Sese Seko alwahi kuanzisha ujenzi wa mnara huko nchini Zaire(DRC) lakini hadi anaondolewa madarakani haukukamilika na kuishia kutelekezwa tu na kuwa makazi ya bundi
Kwa Wakristo kuna Mnara wa Babeli ila sijajua ni mnara wa kiimani tu au upo kweli duniani

Tuangalie minara 10 mirefu zaidi duniani
......................................................... .......

10/Zhongyuan Tower
0fb881ded16ffde2e7199cef283aa1a2.jpg
ea9ff670dd138ad32cd8954e61ac38d6.jpg

Unapatikana Zhengzhou katika jimbo la Henan nchini China
Unaaminika kuwa ndio mnara mrefu zaidi duniani uliotegenezwa kwa vyuma.....ikumukwe hata ElfeltTtower huko jijini Paris Ufaransa umetengenezwa kwa vyuma na ndo chanzo cha jamaa fkani hivi aitwaye Victor Lustig kuwatapeli wafanyabiashara wakubwa wa chuma kwa kuwadanganya kuwauzia ili wapate vyuma

Sasa tuendelee.....mnara huu ujenzi wake ulikamilika mwaka 2011 na ndo ukawa mnara mrefu zaidi wa chuma hadi pale mwingine ulipojengwa Tokyo Japan
Mnara huu una migahawa takribani 200 ya kuhudumia wageni/watalii
Hutumika pia kurushia matangazo ya luninga

Una urefu wa futi 1,273
 
Last edited:
please wait............
sawa mkuu
Ila usijali mkuu nipo likizo now nitakuwa napisti hapa intelligence kuhusu "10 kubwa" hivyo uwe unachungulia mara moja moja ila nitakuwa nadondosha kidogokidogo
 
9/China Central Radio & TV Tower
802dfedbcfa8532c307e54fca8f1a7b2.jpg
e761b8da9384ea010640677466b18cf0.jpg

Zamani wakati TBC ya bongo ikiitwa TVT wenyewe ulijulikana kama CCTV Tower kisha baadaye kidogo ukaitwa Beijing Tv Tower
Ndio mnara mrefu zaidi jijini Beijing yaani ukipanda juu unajioneea mandhari ya jiji lote vizuri kabisa bila kwere
Ulianza kujengwa mwaka 1987 na ujenzi kukamilika mnamo mwaka 1992
Huu ni mnara maalumu kwa ajili ya mawasiliano na kurushia matangazo ya luninga na Radio nchiniChina

Una urefu wa futi 1,329
 
9/China Central Radio & TV Tower
802dfedbcfa8532c307e54fca8f1a7b2.jpg
e761b8da9384ea010640677466b18cf0.jpg

Zamani wakati TBC ya bongo ikiitwa TVT wenyewe ulijulikana kama CCTV Tower kisha baadaye kidogo ukaitwa Beijing Tv Tower
Ndio mnara mrefu zaidi jijini Beijing yaani ukipanda juu unajioneea mandhari ya jiji lote vizuri kabisa bila kwere
Ulianza kujengwa mwaka 1987 na ujenzi kukamilika mnamo mwaka 1992
Huu ni mnara maalumu kwa ajili ya mawasiliano na kurushia matangazo ya luninga na Radio nchiniChina

Una urefu wa futi 1,329
mkuu ni vyema ukaweka kwa mtiririko hata kama utarusha mmoja mmoja ili iwe rahisi kusoma kuliko kupost kama post humu ndani
 
Kuna mnara mmoja huo kila sehemu upo aisee ukisimama huo habari yake inakuwa nyingine kabisa.

Ahsante Sana.
 
mkuu ni vyema ukaweka kwa mtiririko hata kama utarusha mmoja mmoja ili iwe rahisi kusoma kuliko kupost kama post humu ndani
Jf ndio tatizo hawaruhusu kuedit post inayoazisha uzi hivyo ni vigumu kuziendelezea pake pale ukishapost
Samahani kwa usumbufu ila kuwa mvumilivu # 8 & 7 zinakuja muda huu
 
Hii ni moja kati ya post chache nzuri na zenye kuvutia sana.
Lakini kwasababu ilio nje ya uwezo wako, naona kama tayari umeifanya imekosa mvuto na honestly it's boring
Mkuu nuda umebana
Pia hii sio rahisi kupost yote
Mvuto haupotei kwa kupost nusu nusu bali kile mtu anachoandika
Nakuhakikishia naimalizia yote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom