Huwa Rais anafikiria nini katika uteuzi wake?

Tongue blister

JF-Expert Member
Jun 19, 2009
362
11
Nimejaribu kujiuliza lihi swali kila wakati bila kupata majibu yaliyo sahihi , Huwa najiuliza Rais wetu aliwaza nini au huwa anawaza nini pale ambapo huwa teuwa wana jeshi wastaafu kuwa wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ?

Labda kwa ufahamu wangu mdogo mnaweza kunisaidia katika kupata majibu yaliyo sahihi.Tukizingatia pia kwamba wapo pia Vijana wengi wasomi wenye kuijua siasa na wenye uwezo wa kuongoza nchi ndani ya Tanzania wanaishio bila ajira .

Je ni yapi basi mafanikio ambayo tumeyaona yameletwa na viongozi hao shupavu kutoka majeshini ? Na je kuna ukaribu gani ktk ya waheshimiwa hao na wananchi wa kawaida wa kule Geita ama wa Kule Newala mkoani Mtwara ?

Nimejaribu kutazama baadhi ya posts ambazo zimekuwa zikizungumzia maeneo mbali mbali yenye matatizo ya kimaendeleo nikagundua kwamba ukiyafuatilia kwa ukaribu maeneo hayo utaambiwa mbunge wao ni mwana jeshi au mkuu wa wilaya pale ni mwana jeshi au hata Mkuu wa mkoa.

Swali langu ni Je …Rais huwa ana jaribu kufikiri nini katika kuwa Teuwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wana jeshi ?
 
Swala hili halijaanza na JK hii ni toka miaka ya Mwalimu!! Kuna ishu nilisikia (ila sina uhakika) kua hii ni njia moja inayosaidia wapiganaji wetu wasije wakaanzisha Vikundi vya Rebels kama nchi Jirani!!
 
Moja hiyo mkuu...!! Chukua five !!! Nasubiri majibu mengine ! Kisha tunakuja kufanya summary..!
 
Mbili ni kwamba Kwa system ya jeshini, watu hustaafu sometimes na umri mdogo sana, yaani hata kabla ya kufikisha 55 au60 yrs, hivyo kuwaacha benchi hivihivi itawasababishia msongo wa mawazo.

Lakini pia ni kwamba proffession ya uaskari haina kuajiriwa pengine nje ya majeshi, labda mgambo!
 
Swala hili halijaanza na JK hii ni toka miaka ya Mwalimu!! Kuna ishu nilisikia (ila sina uhakika) kua hii ni njia moja inayosaidia wapiganaji wetu wasije wakaanzisha Vikundi vya Rebels kama nchi Jirani!!

Huenda kuna ukweli ndani yake lakini pia JK alikuwa kamanda na kama ilivyo ada ya Tanzania kulindana! inambidi afanye hivyo ili kesho Jk ilikifika nao watamlinda kwa kutoa fadhira.
Nafikiri uteuzi kama huu wakati mwingine huenda ukaweka watendaji wasioweza kuwajibika kwa jamii.
 
Wetu huyu wa sasa nathani ni utashi wake wa kutaka mambumbu haswa kwa uchaguzi wake wa Wanawake hakuwakomboa bali kuwakomoa kwa kuchukua incompetent leaders kama wakina Sofia Simba, Shamsha Mwanguna na Aisha Kigoda (akijiita Dr wakatu ni nurse)! ukiacha hawa, hao wengine sijaskia hata m1 aliyefanya la maana! This is too discouraging hivi wakina Tibaijuka wako wangapi humu Tanzania zaidi ya kutuletea hawa ma-bogus?
 
Swala hili halijaanza na JK hii ni toka miaka ya Mwalimu!! Kuna ishu nilisikia (ila sina uhakika) kua hii ni njia moja inayosaidia wapiganaji wetu wasije wakaanzisha Vikundi vya Rebels kama nchi Jirani!!

I wish u had cofirmation maana linafana sana na ukweli!! nadhani ni bora wangetafutiwa ulaji mwingine kuliko huu maana sasa wanatupa shida sisi wananchi wanaotuongoza kwa kuboronga wanapogaiwa hizo nyadhifa muhimu za kuongoza mikoa na wilaya.
 
Wale madada maDC duh....yule wa mvomero aliniacha hoi last week akifuatialia mafuriko na majangili misistu....wako wengi halafu....
 
sometimes kuwaweka wanajeshi pembezoni mwa mikoa iliyo mpakani ilikuwa ni kuimarisha zaidi usalama, wapo walioweza lakini wengine waliboronga na kuliletea jesi letu sifa mbaya!
 
I wish u had cofirmation maana linafana sana na ukweli!! nadhani ni bora wangetafutiwa ulaji mwingine kuliko huu maana sasa wanatupa shida sisi wananchi wanaotuongoza kwa kuboronga wanapogaiwa hizo nyadhifa muhimu za kuongoza mikoa na wilaya.

Nilihisi lazima mtu mwenye upeo wa kufuatilia mambo kama wewe ,angeliona hilo kama ulivyoliona.
Kawa Rais ana hisi kwamba nchi inaweza kuletewa matata kiusalama basi angejaribu kutafuta njia mbadala kwa kuwatawanya wanajeshi kwa kuwapa shughuli zingine za kimaendeleo, kuliko kuwapatia nyadhifa hizo muhimu ambazo si tu kwamba wanaboronga bali wana haribu kabisa..!
 
Mkuu wameharibu wapi? Kwenye A Golden Opportunity?
 
Mkuu wameharibu wapi? Kwenye A Golden Opportunity?

jishughulishe kidogo tu wa huhitaji kuchosha akili, anagalia mikoa/wilay azinazoongozwa na hao wageshi wastaafu afu ufanye tathmini...
 
Uteuzi wa wanajeshi kama ni ishara tosha kwamba hata wanajeshi nao wanajihusisha kwa namna moja au nyingine kwenye siasa
 
Mimi ninavoona labda wanajeshi wao ni watu wa kufata AMRI tu na si vinginevyo. Yeye Mh kama mkuu akitoa amri wao wanatekeleza.

Tukumbuke kuwa wanajeshi wana nidhamu ya hali ya juu sana katika kutekeleza maagizo na kufata Time hakuna lele mama.

Yote hao ni kichocheo cha wao kuchaguliwa.
 
Mbona hizo sifa mnazotaja hazitoshi na hazina vigezo vya huyu mheshimiwa kuwapa huo uongozi
 
Back
Top Bottom