Huwa hukuna mvurugano kwenye kuwa makini bali utafsiri wake

Nov 2, 2023
61
61
Siku hizi kila mtu anatafuta njia tofauti tofauti na wengi wanafundisha unawezaje kuwa makini. Ina onekana kuna tatizo kubwa la watu kushindwa kuwa makini kwenye wanachofanya na kupata mvurugiko kwenye akili zao. Tunashindwa kuwa na akili iliyotulia kwakuwa muda wote tupo kwenye mkanganyiko wa mapigano ndani ya akili zetu wenyewe bila chanzo chochote kutoka nnje.

Embu tujiulize ni kweli kuna vizuizi vinavyoleta mvurugano na kushindwa kuwa makini akilini mwetu. Au kuna kitu kingine tofauti tusichojua kinachotufanya tuone tatizo tunalo litengeneza wenyewe kwa tafsiri zetu. Kutokuwa makini ina maana gani kwetu, akili kushindwa kufuata unachohisi unataka na kuona unalazimika kujilazimisha kutaka unacho pingana nacho, na kwanini hilo litafsirike tatizo la kuwa makini.

Kuna muda unajiona huwezi kuwa makini lakini ghafla ukapata kitu kinachokusisimua ukajikuta umekuwa makini bila kutegemea, hii ina onyesha kuwa makini si jambo la kulazimisha kwa ufahamu wako bali inatokana na ubora na utulivu wa uelewa wa akili yako. Tumekuwa na mabadiliko mengi ya kihisia na mawazo ya ghafla bila kuwa na ufahamu nayo na hatuliwekei uzito swala hilo kulijua kwa undani.

Kwanza tujiulize umakini ni upi? Ni kuweza kutenda kila kitu kwakutaka kwa kulazimisha tuwepo kwenye wakati wa tukio huku ukitumia nguvu ya kufahamu. Umakini haupo kwenye katakwa yetu na hatujui hilo kwa kulamisha kuwepo kwenye wakati ndio hua kizuizi kinacholeta mvurugiko tunao uona ni kutokuwa makini.

Muda wote akili yetu ipo kwenye mwenendo wa mawazo na hisia bila hiari wala matakwa yetu na pakiwa na chakutuweka makini huwa moja kwa moja tunakuwa makini ila kutoelewa kwetu ndio huleta mvurugano kwa kutaka kudhibiti wakati wa tukio na kuleta shida ya kutokuwa makini.

Kwenye uhalisia hakuna mvurugano unao sababisha kushindwa kuwa makini ila ni tafsiri zetu za kuona mwenendo wa mawazo umenda pengine na sisi tukafikiri ni tatizo na kuanza kupingana nalo hapo ndio tunatengeneza kutokuwa makini. Ila ukiweza kuangalia mwenendo wa mawazo na hisia bila kutafsiri kwa kutaka kudhibiti kuwa ni tatizo utaona hakuna tatizo lolote kwenye mwenendo wa umakini wako na akili itabaki tulivu muda wote.

Nb: Tufufue ufahamu wetu na tuanze kuona uhalisia wa mambo ndani ya akili yetu jinsi tunavyo ya tafsiri tofauti na kutudhuru. Utulivu na umakini wetu ni wa muhimu sana katika akili yetu kuweza kutosababisha mivirugano na upotofu wa kushindwa kuona uhalisia wa maisha.
 
Sijaelewa hapa mkuu kwamba huwezi kukontrol umakini sio kweli!!!!

Ukweli ni kwamba mind zetu zinapenda sana vitu vya kustarehesha

Ndio maana mtu anaweza kuwa makini kufuatilia season yenye vipande 500
Ila hawezi kuvumilia lecture ya 1 hour

Inawezekana kujitrain kuwa makini ila sio suala la siku moja ni Kama unapotengeneza tabia mpya
Inaweza kuchukua miezi tatu au Zaidi
 
Umakini ni suala la maamuzi tu....
Ukiamua kuwa makini utaweza kuwa makini na hakuna cha kukufanya usiwe makini..kila kikwazo cha kuzuia umakini una uwezo wa kukidhibiti kwa asilimia nyingi sana hata uwe kwenye pressure namna gani...

Kwa mfano mwepesi tu...una jambo la muhimu sana linaendelea linahitaji umakini sana halafu linatokea jingine nalo linahitaji umakini..hapo unacheza na % tu..lipi niweke umakini kiasi gani? Na hili niweke kiasi gani..halafu unaacha % ya distraction kwa hiyo unakuta mambo yote yanaenda na vizuizi pia unakua navyo makini...
Tatizo kubwa la umakini ni muda (Time Limit) kama muda ni mdogo sana na jambo ni gumu sana( complicated) hapo sasa uwezo wa akili yako,na hisia mdio zitakusaidia zaidi...ndio maana nasistiza tujitahidi kuongeza hivi vitu ( IQ and EQ)

MP
 
Kuwa makini inawezekana lakini pia ni ngumu sana kwa maisha ya binadamu wa kawaida, kwasababu matendo mengi ya binadamu yanaongozwa na hisia kwanza halafu fikira zinakuja baadae, kwahiyo kama utashindwa kutuliza hisia zako huwezi kuwa makini hata siku moja.
Ndo mana dini zote zimejikita kujenga watu kwenye hisia ili kuweza kuwa makini.
Na ndio mana tunashauriwa kuswali,kusali,kufanya meditation zote hizo ni njia za kupunguza mihemko ya akili(hisia) ili akili iweze kufikiria vizuri bila distraction nyingi.
Jambo la kusikitisha ni kwamba matendo yote ya binadamu yanaongozwa na hisia ndo mana watu wasio na dini,au wasiifanya meditation wanaongoza kwa ulevi,umalaya, kujinyonga,kujiuwa,kwakuwa hawana kitu ambacho kinawasadia ku deal na hisia kali zinapotokea kama kusali,au kufanya meditation.
 
Self control is an illusion
Screenshot_20240331-230014_Moon%2B%20Reader.jpg
 
Sijaelewa hapa mkuu kwamba huwezi kukontrol umakini sio kweli!!!!

Ukweli ni kwamba mind zetu zinapenda sana vitu vya kustarehesha

Ndio maana mtu anaweza kuwa makini kufuatilia season yenye vipande 500
Ila hawezi kuvumilia lecture ya 1 hour

Inawezekana kujitrain kuwa makini ila sio suala la siku moja ni Kama unapotengeneza tabia mpya
Inaweza kuchukua miezi tatu au Zaidi
Huwezi kucontrol umakini kwakuwa hakuna controller
 
Umakini ni suala la maamuzi tu....
Ukiamua kuwa makini utaweza kuwa makini na hakuna cha kukufanya usiwe makini..kila kikwazo cha kuzuia umakini una uwezo wa kukidhibiti kwa asilimia nyingi sana hata uwe kwenye pressure namna gani...

Kwa mfano mwepesi tu...una jambo la muhimu sana linaendelea linahitaji umakini sana halafu linatokea jingine nalo linahitaji umakini..hapo unacheza na % tu..lipi niweke umakini kiasi gani? Na hili niweke kiasi gani..halafu unaacha % ya distraction kwa hiyo unakuta mambo yote yanaenda na vizuizi pia unakua navyo makini...
Tatizo kubwa la umakini ni muda (Time Limit) kama muda ni mdogo sana na jambo ni gumu sana( complicated) hapo sasa uwezo wa akili yako,na hisia mdio zitakusaidia zaidi...ndio maana nasistiza tujitahidi kuongeza hivi vitu ( IQ and EQ)

MP
Huwezi kucontrol umakini kwakuwa hakuna kikwazo kati yako na umakini ni kutoelewa tu
 
Kikwazo kati yako na umakini ni uwezo wako wa kuact under pressure...hapa kuna time limit,Iq..Eq na mazingira....siku hz kuna technology so unaezaje kucontrol kila kitu on a limited time? Hilo gape lipo na ndio linatutofautisha sisi na ile 1%....wakati mwingine na supreme beings!
 
Siku hizi kila mtu anatafuta njia tofauti tofauti na wengi wanafundisha unawezaje kuwa makini. Ina onekana kuna tatizo kubwa la watu kushindwa kuwa makini kwenye wanachofanya na kupata mvurugiko kwenye akili zao. Tunashindwa kuwa na akili iliyotulia kwakuwa muda wote tupo kwenye mkanganyiko wa mapigano ndani ya akili zetu wenyewe bila chanzo chochote kutoka nnje.

Embu tujiulize ni kweli kuna vizuizi vinavyoleta mvurugano na kushindwa kuwa makini akilini mwetu. Au kuna kitu kingine tofauti tusichojua kinachotufanya tuone tatizo tunalo litengeneza wenyewe kwa tafsiri zetu. Kutokuwa makini ina maana gani kwetu, akili kushindwa kufuata unachohisi unataka na kuona unalazimika kujilazimisha kutaka unacho pingana nacho, na kwanini hilo litafsirike tatizo la kuwa makini.

Kuna muda unajiona huwezi kuwa makini lakini ghafla ukapata kitu kinachokusisimua ukajikuta umekuwa makini bila kutegemea, hii ina onyesha kuwa makini si jambo la kulazimisha kwa ufahamu wako bali inatokana na ubora na utulivu wa uelewa wa akili yako. Tumekuwa na mabadiliko mengi ya kihisia na mawazo ya ghafla bila kuwa na ufahamu nayo na hatuliwekei uzito swala hilo kulijua kwa undani.

Kwanza tujiulize umakini ni upi? Ni kuweza kutenda kila kitu kwakutaka kwa kulazimisha tuwepo kwenye wakati wa tukio huku ukitumia nguvu ya kufahamu. Umakini haupo kwenye katakwa yetu na hatujui hilo kwa kulamisha kuwepo kwenye wakati ndio hua kizuizi kinacholeta mvurugiko tunao uona ni kutokuwa makini.

Muda wote akili yetu ipo kwenye mwenendo wa mawazo na hisia bila hiari wala matakwa yetu na pakiwa na chakutuweka makini huwa moja kwa moja tunakuwa makini ila kutoelewa kwetu ndio huleta mvurugano kwa kutaka kudhibiti wakati wa tukio na kuleta shida ya kutokuwa makini.

Kwenye uhalisia hakuna mvurugano unao sababisha kushindwa kuwa makini ila ni tafsiri zetu za kuona mwenendo wa mawazo umenda pengine na sisi tukafikiri ni tatizo na kuanza kupingana nalo hapo ndio tunatengeneza kutokuwa makini. Ila ukiweza kuangalia mwenendo wa mawazo na hisia bila kutafsiri kwa kutaka kudhibiti kuwa ni tatizo utaona hakuna tatizo lolote kwenye mwenendo wa umakini wako na akili itabaki tulivu muda wote.

Nb: Tufufue ufahamu wetu na tuanze kuona uhalisia wa mambo ndani ya akili yetu jinsi tunavyo ya tafsiri tofauti na kutudhuru. Utulivu na umakini wetu ni wa muhimu sana katika akili yetu kuweza kutosababisha mivirugano na upotofu wa kushindwa kuona uhalisia wa maisha.
tatzo madeni😢
 
Back
Top Bottom