Hoja ya nchi kujitenga si ya leo ni ya muda mrefu huko nyuma

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

Kwa kuwajulisha tuu kiufupi haya yote yanayo tokea sasa ni matokeo ya Uongozi wetu tokea huko nyuma hadi hapa tulipo fika kama uongozi ungekuwa bora , siasa zinge kuwa safi haya mambo yange kuwa ni tofauti.

Nakuja kwa hoja yangu, Mnamo miaka ya mwisho wa 1980's kuja kwa mwanzoni mwa 1990's kulikuwa na kundi kubwa la vigogo toka kanda ya ziwa na walikuwa kwa system mean ndani ya serikali na ni walikuwa wana CCM wazito haswa walikuwa na mpango wao kabambe ambao ulikuwa umekamilika wa kujitenga kwa kanda ya ziwa Bukoba, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara. na kwa bahati mbaya hiyo issue ikawa leaked. waka potezea. Kwa hali ile nchi ilitaka kujitenga ni kwa ajili ya haya haya mambo ya serikali kutojali na kuwa makini na kuwajibika kwa wananchi wao.(Kanda ya ziwa ilikuwa inajua inajitosheleza kwa kila kitu kiuchumi na idadi ya watu wengi wange support mapinduzi yale) leo hii nasari kusema kujimegea aridhi yao ati viongozi wama kuja juuu ivi migogoro ya Aridhi huko Meru Mashariki serikali ni mpaka ijiridhishe vipi? kusikia kilio cha watu wa arumeru.

Tuongee ukweli tuuu hivi wananchi wa Arumeru Mashariki kwanini wakavamia mashamba wao ni wenda wazimuu?? Kwanini Mkapa alisema tutawarudishia aridhi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki inamaana serikali kwanini haikumwoji Mkapa kwanini ulisema kuwarudishia Aridhi watu wa Arumeru Mashari? na Aridhi ilikwenda wapi muda wote huo?

My Take;

Matukio haya ni juu ya serikali kutojari wananchi wake esp katika maeneo hayo kama kanda ya ziwa,Kaskazini wana resource za kutosha lakini maisha yao ni duni duni mpaya na hii yote ni serikali yetu kutojipanga na kuwa legelege. Tukisema mengi tunakuwa maadui wabaya kabisa ila wale vigogo wanao uza nchi yetu wao ni wema kuliko sisi rai wa kawaida.

 
Kwani nini kipya mbona kuna mbunge mmja wa Mtwara aliwahi kutamka bungeni kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ijietenge na kujiunga Mozambique!
 
Mbeya ni nchi na Rais ni Sugu!

Source: Mabango ya wamachinga mjini Mbeya
 
Wakuu hizi propaganda tuachane nazo kunya naye kuku,bata anaharisha.Nani anakumbuka lile tamko la waislamu lililofadhiliwa na Makamba pale diamond kati wa waliyoyasema ni kwamba nchi itengwe kati ya waislam na wakristo hawa hawakupewa shutuma za uhaini hapana ila Nassari ndio mhaini
 
The law is an invention of the strong to CHAIN and RULE the WEAK_Rousseau
Tafakari,Chukua Hatua
 
Wazee waliotaka Pemba ijitenge kesi yao iliishia wapi?

Hawa waliandamana hadi ofisi za UN Dar es salaam kupeleka barua ya kuomba Pemba ijitenge.
 
Jumuiya ya Uamsho Zanzibar inayotaka kuvunja Muungano ambayo ni sawa na kuimega nchi vipande viwili iko wapi, imeendesha mikutano mfululizo mwezi ulipita huko zanzibar kuhamasisha wananchi wa zanzibar wavunje Muungano
 
Hoja hii inaweza kumtia matatani Nassari kama mchezo wa kuigiza.

Mbowe alielewa mapema hatari ya kauli ya Nassari ndio sababu akawahi kukanusha.

Kijana anasherehekea ushindi wa Arumeru kwa mbinu ya kutangaza uhaini!!!!!!!!!
 
Hoja hii inaweza kumtia matatani Nassari kama mchezo wa kuigiza.

Mbowe alielewa mapema hatari ya kauli ya Nassari ndio sababu akawahi kukanusha.

Kijana anasherehekea ushindi wa Arumeru kwa mbinu ya kutangaza uhaini!!!!!!!!!
hapo juu watu wameweka hoja za similar magnitude ambazo serikali ilikaa kimya............
 
Usipotoshe. Historia huo ni uongo. Tena wa. Kutunga ili kupoteza leng o la mjadala wa Hoja ya Nassari .
 
Jumuiya ya Uamsho Zanzibar inayotaka kuvunja Muungano ambayo ni sawa na kuimega nchi vipande viwili iko wapi, imeendesha mikutano mfululizo mwezi ulipita huko zanzibar kuhamasisha wananchi wa zanzibar wavunje Muungano

Pengine kuipa hoja nguvu,wazo la kuanzisha nchi kanda ya kaskazini ni la siku nyingi sana na muhimu kwa ustawi wa ukanda huo.ni nchi inayoundwa na Tanga,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Mara........,kutokana na rasilimali zilizopo,bandari(Tanga)Mbuga za wanyama,madini,mlima Klmanjaro,mipaka na nchi jirani(Kenya) na uongozi thabiti wa kizalendo tungekuwa mbali sana.Nassari kutamka aliyotamka isiwe nongwa,kila siku wabunge wa pembezoni(Mtwara,Ruvuma,Kigoma rukwa n.k)wanatamka hayo,mbona hawaitwi wahaini!!!!
 
Hoja hii inaweza kumtia matatani Nassari kama mchezo wa kuigiza.

Mbowe alielewa mapema hatari ya kauli ya Nassari ndio sababu akawahi kukanusha.

Kijana anasherehekea ushindi wa Arumeru kwa mbinu ya kutangaza uhaini!!!!!!!!!

Uhaiini kivipi inchi hii ina wahaiini wangapi, Hawa wanao kula nchi si wahaiini kweli?????
Nadhani sasa tutumie haya maneno kwa wale wana hujumu inchi yetu mafisadi wote ni wahaini maana ni watu wanao iangamiza nchi huku twacheka tuu na haya magazeti yetu ya unafiki kila kukicha hawajui ni kipi cha kuelimisha wananchi


 


Uhaiini kivipi inchi hii ina wahaiini wangapi, Hawa wanao kula nchi si wahaiini kweli?????
Nadhani sasa tutumie haya maneno kwa wale wana hujumu inchi yetu mafisadi wote ni wahaini maana ni watu wanao iangamiza nchi huku twacheka tuu na haya magazeti yetu ya unafiki kila kukicha hawajui ni kipi cha kuelimisha wananchi



Uhujumu uchumi nafikili una maana Prof. Mahalu?
 
Ndugu zangu mawazo kama haya tusiyachukulie kisiasa na kisheria zaidi maana sheria za Tanzania zimeegemea kwa wenye nafasi. Jambo la msingi tutambue kuwa watu tumechoka na ufedhuli unao fanywa na watawala wetu tulio wapa dhamana ya kutuongoza (ila wao wanatutawala). Maeneo yate ambayo watu wanalalamika siyo wapuuzi au wahaini kama ambavyo watawala wanataka watuaminishe, maeneo haya yana rasilimali nyingi ambazo kwa akili ya kawaida tu ambayo haihitaji uwe msomi wa degree ulitambue hilo. Maisha ambayo watu wanaishi pembezoni mwa rasilimali hizi yanatisha na kama hujui basi fika maeneo haya utaona na utakubaliana na mawazo ya watu kujitenga ili wapate kile wanacho amini ni haki yao na hawakipati kwani walafi ni wengi wanaozitolea macho rasilimali hizo. Mie natoka kanda ya Ziwa lakini maisha tunayo ishi hayalingani na rasilimali tulizo jaaliwa na maanani. Tutafute suluhisho la matatizo ya wananchi kwani maeneo yetu tunakila aina ya rasilimali ambazo zinanufaisha maeneo mengine na kutuacha tukitaabika. Tunalima pamba, almasi, dhahabu, ziwa, ng'ombe ambavyo vinaliingizia taifa hili pesa za kigeni, lakini siye ndo wenye taabu na miundo mbinu (barabara,reli) zinajengwa sehemu watokazo viongozi.Tatizo letu ni elimu na natumai tukipata elimu ya kutosha kwa watu wa huku PATACHIMBIKA
 


Tulijaribu kwa hawa mafisadi wetu kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi lakini watawala wetu kwa kujua kitakacho jiri kama wakifunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi wanakuja na politic zao MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA. Kama mchwa hawa wanadiriki kuiba BOT bado unadai ni matumizi mabaya ya madaraka!!!!!!!!!!! BOT ndo uchumi wa taifa letu unako angalia
 
Back
Top Bottom