Hiyo Kodi itakayotozwa pindi nitakapokuwa naingiza vocha ni tofauti na hii ambayo anakatwa mtoa huduma (VAT)?

Mbogo nyeusi

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
233
540
Mh waziri ukweli ni kwamba Mh Zungu anakudanganya utarudisha huo uwaziri kwa mama siku zinahesabika.

Hivi wewe Mwingulu na PhD yako ni wa kuokota mawazo ya kijinga ya Zungu? Uzalendo haupimwi kwa kulipa tozo za kuumizana,

Mh waziri ivi hiyo Kodi itakayo tozwa pindi nitakapokuwa naingiza vocha ni tofauti na hii ambayo anakatwa mtoa huduma? (VAT)

Hebu tafakari mtu ana buku akanunua vocha ya buku na kifurushi kinauzwa buku,alivyo ingiza tu kwenye simu yake Mara paaaap ikakatwa sh 10 na kubakiwa na sh 990, je huyu mtu atawezaje kujiunga na kifurushi ikiwa kasha pelewa sh 10?

Mh unatakiwa ujue kuwa hata Kodi tuliyo zoea kukatwa kupitia mtoa huduma ile ni pesa yangu mimi mtumia huduma,,mfano nimenunua vocha ya buku nilivyo ingiza kwenye simu na kununua kifurushi ikakatwa VAT sh 50, je hiyo sh 50 ni ya mtoa huduma au ni ile pesa yangu imekatwa, huo uzalendo mnaoutaka nyie ni upi?

Kweli mmetuona sisi watanzania ni mambumbumbu kweli, nalipa VAT kila ninapo nunua salio na kufanya miamala haitoshi mnataka kutukamua mpaka itoke hewa, huwezi ukaijenga nchi kwa hiyo miradi mikubwa ikaonekana ikiwa hata mlo wa siku kwetu ni shida na watu tuna makazi duni, watu wakiwa na kipato cha kuridhisha maendeleo yanajileta yenyewe.

Utakapo ongeza hiyo Kodi ya uzalendo tayari umeathiri budget ya mtu kwa kuwa hataweza tena kununua vocha ya buku atalazimika kununua vocha ya buku jero ili akatwa hiyo sh 20 apate buku ya kuunga kifurushi.

Nyie wabunge kwa kuwa mna posho nyingi na mishahara mikubwa mnatudharau na kutuona mambulula,mishahara yenu na posho hazikatwi Kodi Sasa tuanzie hapo kukata Kodi ndio tuone huo uzalendo wenu unao hubiriwa na Zungu,kiinua mgongo chenu zaidi ya milioni mia mbili hakikatwi kodi na nikiinua mgongo cha ajabu mnafanya kazi miaka mitano na mnapata kiinua mgonga kinamzidi mtumishi wa uma aliye fanya kazi miaka 40.

Wabunge muone aibu mnatufedhehesha inakuwaje mtu akatwe Kodi Mara mbili? VAT tunakatwa kila tunapo nunua salio au kifurushi,Sasa mnatuongezea na uzalendo, huo uzalendo anzeni nao nyie kwa kukataa sitting allowance zote kwa kuwa kituo chako Cha kazi ni bungeni inakuwaje upo ofisini kwako unajilipa posho ya kwenda ofisi? Mnaonaje wafanyakazi wote wa serikali nao wakaanza kujilipa posho kila suku wakiwa wanafanya majukumu yao ya kiofisi?

Mh Zungu anza kutuonesha uzalendo wako utangaze kwamba kuanza mwezi wa saba ukatwe Kodi kwenye miposho yako na mishahara yako.

La sivyo Mh waziri kama mtashindwa kujikata Kodi kwenye mishahara yenu ondoa hiyo tozo Mara moja, maumivu mnayo pata pale mnapo sikia kuwa posho zenu zinataka kupunguzwa kwa kukatwa Kodi ndivyo hivyo tunavyo sikia maumivu mkipitisha hoja ya Zungu ya sisi raia wanyonge kukatwa shilingi 10 zetu ili hali tunakatwa VAT.

Mh waziri kwa kuwa mna maisha mazuri mnatuona labda na sisi huku mtaani tunafanana na nyie, siye tuna maisha magumu na zaidi mnataka kumkwamisha mama, mama anataka kuongeza mzunguko wa pesa mtaani wewe na Zungu mnataka mzikusanye mzirundike huko hazina.
 
Hawa viongozi wameshatoa sie ni zumbukuku ulimwengu uko huku, washazoea kelele zetu za chura, kupiga kelele mitandaoni baada ya siku mbili 3 yataisha wajinga wengi wataanza kuongelea "video mpya ya diamond" sijui chupi ya Nandy.

Ilitakiwa ifike kipindi tuwajambishe, tuhashimiane kidogo, hawa wanatuona sisi ni mafala kiwango cha lami, pesa wanazopeana bungeni aisee, ukisoma moyo unanyong'onyea, ndio maana ubunge(siasa) umekuwa ni ajira pendwa kwa watu wa kada zoote, mwl, eng, Dr, n.k woote wanautamani ubunge.

Wakat mwingine nasemaga inahitajika katiba mpya lakini je katiba mpya ndio itaponya huu uzembe weetu, hii hii ya zamani inavunjwa nasi kimya tu.
 
ELIMU
Nafikiri maendeleo ya nchi hii yanapaswa kuanzia chini huko kwa kutoa elimu bora zaidi.
Mtaala ubadilishe tutoke kwenye elimu ya vyeti twende kwenye elimu ya kuhoji.

Siku moja nchi irudi kwa wenye nchi na sio kwa wanasiasa. Pesa wanayoipata hawa jamaa watz 70% ikiwauma na wao wanachokipata ndio mapinduzi ya kiutawala yatakapoanzia.

Umaskini mbaya sana ni wa fikra kuliko umaskini wa mali.
 
Tz ni shida kodi juu ya kodi ,naunga mkono hoja
Yaani hao wabunge kwanza hawana tija ,wanaunga mkono na kutuambia kwa kejeli ' nyie watz lipeni kodi' utafikiri tulikuwa hatulipi siku zote, kwa kukatwa hiyo VAT ktk kila tulipokuwa tunaunga kifurushi! Hayo ni mambo ya dharau za aliyeshiba, hamjui mwenye njaa... serikali na wabunge jamani tuwahurumie na kuwafikiria wananchi walio na vipato vya chini kwa kuzidi kuwakamua... kaaazi kwelikweli.
 
Wanakamua beberu wakidhani ana maziwa kumbe zile @&%$
 
Dr. Mwigulu tafadhali ongeza na kodi ya umiliki wa Kisimbuzi na TV. Kodi hii itakuwa inakatwa kila mwezi katika malipo ya vifurushi.
 
Tumeipenda wenyewe chaguo letu milele.. ndindiii wacha waisome namba eeeh ccm mbele kwa mbelee
 
Back
Top Bottom