Hivi zile challenge kule TikTok huwa ni kweli?

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
10,414
16,268
Sijawahi kutumia TikTok hapo kabla, ni jana tu nimejiunga huko mjini TikTok. Hii ni baada ya mshikaji wangu mmoja mara kibao amekuwa akiniambia kuwa kule kuna vichekesho ambavyo kama huna mbavu huwezi kuhimili. Basi jana nikaamua kujiunga kwa lengo la kwenda kuangalia hivyo vichekesho.

Kwa kweli nimekutana na vichekesho na kama alivyo sema kama huna mbavu huwezi vumilia. Mimi huwa ni mpenzi wa vichekesho maana wakati mwingine unaondoa msongo wa mawazo. Katika kuendelea ku scroll nilikutana na account nyingi zikiwa na content (maudhui) mbalimbali, vijana wanajitahidi.

Maudhui yaliyo nifanya nije kuuliza hapa ni yale ya challenge za wapenzi, nimekutana na account nyingi zinazo endesha hizo challenge. Mfano jamaa anakuja anakufanyia challenge kwa mpenzi wako bila yeye kujua mwisho wa siku mambo yanakuwa hasi tofauti na ulivyo tarajia. Nimebaki nashangaa sana hiyo kitu, hivi ni kweli hayo mambo yapo?

Zile challenge nilikuwa nacheka sana, yaani watu wanaingizwa box na wanajaa. Challenge kama hizo binafsi hapana.
 
Y'all see me in pornhub doing my thang,but TikTok??hapana that's lame bro,..tuadithie na ya Snapchat
 
Mkuu unataka wote tutafute pesa TikTok? Kila mmoja ana namna yake ya kuingiza pesa, na kingine kila mmoja ana namna yake ya kujiburudisha. Mimi najiburudisha kwenye hivyo vichekesho, sio mbaya ata kama anaingiza pesa maana huko ndio kwenye hustle zake. Starehe ni gharama lazima tuilipie
Watu wanatafta pesa wewe, unacheka!
 
Mkuu unataka wote tutafute pesa TikTok? Kila mmoja ana namna yake ya kuingiza pesa, na kingine kila mmoja ana namna yake ya kujiburudisha. Mimi najiburudisha kwenye hivyo vichekesho, sio mbaya ata kama anaingiza pesa maana huko ndio kwenye hustle zake. Starehe ni gharama lazima tuilipie
Endelea kustarehe mkuu, sio kesi
 
Back
Top Bottom