Hivi kwanini binadamu wana roho mbaya sana juu ya wanyama?

ntuchake

Member
Apr 17, 2024
49
110
Watanzania wana roho mbaya sana juu ya wanyama. Wakimuona paka ata kama hajafanya kitu wanaanza kumporomoshea mawe wanamfukuza na matusi juu. Halikadhalika mbwa na ndege kama vile kunguru na ndege wengine. Ni nini hasa inachangia Watanzania kuwa na roho mbaya juu ya wanyama ambao ni viumbe visivyokuwa na hatia?
 
Kutokumpenda Mungu! Kama wangekuwa wanamjua Mungu na kumpenda Mungu, wangevipenda na kuvijali viumbe Vyake.

Wewe hushangai mtu anamtumikisha punda kwa manufaa yake binafsi na bado anampiga bila kosa!
 
Huu ni utamaduni uliojijenga kwa siku nyingi pengine kwa sababu ya mazingira tunayoishi. Siyo wanyama na ndege tu hata binadamu wenyewe kwa wenyewe hupenda kushambuliana.
 
Ni kitu cha kustaajabu sana. Yani mpaka mbwa akimuona binadamu anakimbia anajua ni adui.

Baadhi ya nchi mbwa anatembea tu hamna wa kumbugudhi.
Hatupendi wanyama wenzetu.
 
Stress na Uchawi.
Hizi ni sababu nazoweza kuzikubali. Hata kuangalia picha za watu waliojeruhiwa au kufariki nalo ni tatizo. Unakuta mtu akisikia kuna ajali mbaya imetokea mahali anakimbilia mbio. Akikuta hakuna majeruhi anarudi huku anatukana eti amepoteza muda wake na hakuna lolote. Akikuta majeruhi na vifo anaumia lakini hapo hapo roho yake inaridhika.
 
Hapo kwenye kunguru hapo, acha wale majabali tu wana tabia chafu sana.
 
Hizi ni sababu nazoweza kuzikubali. Hata kuangalia picha za watu waliojeruhiwa au kufariki nalo ni tatizo. Unakuta mtu akisikia kuna ajali mbaya imetokea mahali anakimbilia mbili. Akikuta hakuna majeruhi anarudi huku anatukana eti amepoteza muda wake na hakuna lolote. Akikuta majeruhi na vifo anaumia lakini hapo hapo roho yake inaridhika.
Ajabu sana
 
Kutokumpenda Mungu! Kama wangekuwa wanamjua Mungu na kumpenda Mungu, wangevipenda na kuvijali viumbe Vyake.

Wewe hushangai mtu anamtumikisha punda kwa manufaa yake binafsi na bado anampiga bila kosa!
Mungu watamjuaje wakati yeye mwenyewe hajulikani? Unataka wajue hewa inayoitwa Mungu?
 
Kunguru tabia zake mbovu maana anaua vifaranga pia mwizi, paka naye mwizi sana wa kuku bata etc mbwa koko naye vilevile. Viumbe wastaarabu binadamu haangaiki nao
 
Watanzania wana roho mbaya sana juu ya wanyama. Wakimuona paka ata kama hajafanya kitu wanaanza kumporomoshea mawe wanamfukuza na matusi juu. Halikadhalika mbwa na ndege kama vile kunguru na ndege wengine. Ni nini hasa inachangia Watanzania kuwa na roho mbaya juu ya wanyama ambao ni viumbe visivyokuwa na hatia?
Una uhakika hawana hatia?

Mimi Kuna siku sina hili Wala lile, nakatiza zangu chini ya Mnazi, likunguru likaniparamia na kunikwaruza kichwani na makucha yake, ukizingatia nilikuwa nimenyoa Dongo.. Nilimmaind sana yule Fala.

Halafu unasema hana hatia?
 
Sio utamaduni Wala mazoea yetu kupenda wanyama hasa wanaozurura mitaani.

Wavietnam walipokuja kujenga minala ya Halotel walikula mbwa wa mitaani karibia wote hasa Dar es Salaam, waliwapunguza kwa kiwango cha juu sana
 
Watanzania wana roho mbaya sana juu ya wanyama. Wakimuona paka ata kama hajafanya kitu wanaanza kumporomoshea mawe wanamfukuza na matusi juu. Halikadhalika mbwa na ndege kama vile kunguru na ndege wengine. Ni nini hasa inachangia Watanzania kuwa na roho mbaya juu ya wanyama ambao ni viumbe visivyokuwa na hatia?
Umewahi fuga paka au wow tujue kweli unawapenda au laa au hata kunguru 🤔
 
Ni nadra kumuona mtu anamfukuza paka aliyemfuga na huenda kafanya kosa, hawa paka unakuta sijui katoka wapi yanakuja kulia dirishani alafu uache mlango wazi sasa utakuta jikoni mboga wamemaliza

Ukifanya wema uwe unawapa chakula pengine nje kidogo ya nyumba wanageuza inakuwa choo pale , hilo utaweza kulivumilia? Wakati yule uliyemfuga unaweza kukaa miezi 3 hujui anajisaidia wapi na mara ingine ukimuona ni kwenye Mataka taka ambako ni sehemu sahihi
 
Back
Top Bottom