Hivi bado kuna watu wanaoamini kuwa Lowassa alikuwa ni mtu mbaya?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,207
7,084
Lowassa alikuwa na madhaifu yake, lakini inawezekana hakuwa mbaya kiwango ambacho wanasiasa waliokuwa wana chuki naye walikuwa wakimtuhumu.

Pamoja na madhaifu yake, alikuwa kiongozi mzuri.
1. Utendaji wake alipokuwa waziri wa maji alidhihiriaha hilo.

2. Mbinu zake za kuweza kushawishi makundi mbalimbali ya watu haukuwa wa kutiliwa mashaka. Mtu asiseme alikuwa akitumia pesa kwa sababu si yeye peke yake aliyekuwa tajiri.

3. Matunda yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha Uwaziri
Mkuu wake yangali yakionekana hata sasa.

Alikuwa na madhaifu yake, kama ambavyo kila mtu ana yake, lakini alikuwa "kiongozi".

Lakini, kama ilivyosemekana kuwa mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe, ndivyo ilivyotukia kwa Lowassa.
1. Alizushiwa na wanasiasa
2. Alitukanwa na vijana
3. Alikejeliwa na wazee
4. Alizomewa na wasiokuwa wa hadhi yake.

Lakini pamoja na yote hayo, yeye alikaa kimya.

Mahasimu wake wa kisiasa walifurahia kuona mashambulizi yalizidi dhaidi yake. Hata viongozi waliodhamiwa kuwa na hekima nao walikaa kimya!

Ajabu! Alipofariki, wakasema "pengo lake halitazibika"

Kwa nini hawakutuambia hayo alipokuwa bado ana nguvu?

Kwa nini wamesubiria hadi amekata pumzi ndiyo wamsifie?
 
Kwa sasa kiongozi yoyote anayekiri/atakayekiri kuwa nchi yetu imekwama na inahitaji tukae pamoja tutafakari mfumo wa uongozi wetu, ni wapi tumekosea na tujaribu kufanya reset, huyo ndiye kiongozi mzuri kwangu. Hawa wanaogombania nafasi za uongozi huku wakijifanya hatuna matatizo wote ni waganga njaa. Lowassa alikuwa upande gani?
 
Back
Top Bottom