Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,598
- 215,331
Utamaduni wa kutengeneza vitenge kutumia wax ulianzia Indonesia katika kisiwa cha Java. Vitenge vilitengenezwa kwa kutumia kitambaa cha batiki. Wax ya nyuki ilipochanganywa na rangi za nguo iliimarisha ubora na haikutoka kirahisi hata iliponyeshewa na mvua.
Uzalishaji ulikuwa ni mdogo tu na vitenge vilitengenezwa kwaajili ya viongozi wa makabila na machifu.
Nerthalands ilipoichukua Indonesia kama koloni lake waliona utaratibu huu na kuchukua ufundi huu kuupeleka Holland katika miaka ya 1850. Makampuni yaliyoanzisha uzalishaji kwa mashine ni pamoja na Jean_Baptiste_Theodore_Prévinaire na Peter Fentener_van_Vlissingen. Wafanyabiashara hawa walikuwa na mategemeo ya kuwa uzalishaji wa mashine utatoa mali nyingi itakayoteka soko la Indonesia. Matokeo yalikuwa kinyume na matarajio yao. Walikosa soko kabisa.
Wakati huo huo Nerthalands ilichukua Pwani ya Dhahabu Afrika (The Gold Cost today’s Ghana). Na katika bidhaa ilizipeleka Ghana ni batiki wax print. Bidhaa hii ilipokelewa kwa kasi mno na Africa ilianza kutumia batiki wax kama vazi la kila siku.
Wakati huo Ghana walifuma nguo zao aina ya kente lakini hizi zilifumwa kwa mkono na zilikuwa ni alama ya ma machifu na viongozi wa jadi.
Mwaka 1854 mfalme Willem wa Nerthalands alianzisha kiwanda cha pamba katika mji wa Haarlem katika jitihada za kuokoa idadi ya raia wasio na kazi. Kiwanda hiki kilizalisha Hollandeise wax kwa wingi mno.
Mafanikio ya Wax Hollandeise yaliwavutia wafanyabiashara wengine. Ilikuja Scotish print jina lingine iliitwa English wax na Swiss wax.
Biashara iliposhamiri meli za Nertherland na Scotland zilipeleka vitenge Ghana miaka ya 1870-1930 kipindi hiki Netherland iliajiri watu kutoka Afrika Magharibi kwa wingi katika jeshi lake ili kupigania koloni la Indonesia. Askari hawa walijulikana kama Belanda Hitam. Wachache waliobahatika kurudi kutoka vitani walikuwa na fahari kuvaa suruali na shati la Wax Hollandeise. Belanda Hitam waliongeza umaarufu wa bidhaa hii.
Kitenge kizima ni yadi 12 lakini mauzo ya nusu kitenge yadi 6 hufanyika pia. Yadi sita ndiyo vipande vitabu. Afrika sasa wana viwanda vya kuzalisha vitenge vya wax. Mpaka sasa hivi majina maarufu ya vitenge vya wax ni imiwax, java print, roller print, na Le fancy. Uzalishaji wa kitenge kisicho na wax ni rahisi zaidi.
Vlisco ambayo ilikuwa Vlissingen ndiye mzalishaji mkubwa wa Wax Hollandeise aliyebaki na soko lake kubwa ni Afrika pamoja na Waafrika wanaoishi Ulaya na Marekani. Mwaka 2014 peke yake Vlisco ametengeneza faida ya €million 300.