Elections 2015 Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,657
113,882
Wanabodi,

Habari za Jumapili.

Jumapili ya leo, naomba tutafakari kwa pamoja msemo huu wa lugha ya Kilatini kuwa "Vox Populi is Vox Dei"
ukimaanisha "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu!", au "Kauli ya wengi ni kauli ya Mungu", ikimaanisha "Chaguo la wengi ndilo Chaguo la Mungu!".

Kuna maandishi yamewahi kuandika kuwa "hakuna kipya chini ya jua", jambo lolote linalotokea duniani, liwe zuri au baya, liliisha pangwa siku nyingi kitambo kuwa litatokea na jinsi ile ile ambayo limetokea!, yaani hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya, coincidence neema, majanga, etc, everything is pre meditated events zilipangwa tangu kitambo, vivyo hivyo ile siku dunia iliumbwa iliishajulikana rais wa Tanzania kwa mwaka 2015 ni nani!.

Kuna msemo wa Waswahili usema "Lisemwalo lipo, na kama halipo linakuja!", October ndio hiyo inakuja, jee hili lisemwalo sana, litakuwepo?, na kama halipo jee litakuja?!.

Rais wa Tanzania kwa mwaka 2015 tayari yupo, ameishaandikiwa, ameisha pangwa, ameisha chaguliwa na sasa anasubiri tuu kuapishwa!, hizi harakati zote za kutaja taja majina ni process tuu ya kukamilisha kile kilichoshapangwa!, hivyo watu mseme msiseme, mpange msipange, rais ni yule tuu aliyeandikiwa kuwa ndie rais wetu wa 2015 na ni lazima awe yeye, nikimaanisha yule aliyepangiwa na Mungu kuwa ndiye yeye, then lazima awe yeye, na akitokea akawa ni yule yule wengi wanayemdhania, huo utakuwa ndio uthibitisho wa kazi ya Mungu haina makosa!. Ikitokea asiwe yule ambaye ni chaguo la wengi, na badala yake akawa mwingine yoyote, then huyu mwingine aliyekuwa rais wetu itakuwa ndio yeye aliyeandikiwa!, sometimes sio lazima lisemwalo ndilo liwalo, bali liandikwalo!.

Kwa vile chaguo la rais wetu wa 2015 ni kazi ya Mungu, then inawezekana kabisa akachaguliwa mtu asiyetarajiwa kabisa, kama vile Mungu alipombadili mvuvi wa samaki na kumfanya mvuvi wa watu!. Na Akamwambia "Wewe ni mwamba na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu!".

Ila pia kwenye mipango ya Mungu, kuna baadhi ya mambo ya ajabu ambayo Mungu huyapanga ili kuudhihirisha utukufu wake, mfano wakati wa kuwakomboa Wana wa Israel kutoka utumwani Misri, kwa kumtumia Nabii Musa, Mungu aliufanya moyo wa Firauni uwe mzito ili aweze kuudhihirisha utukufu wake kwao!.

Hiki ndicho kinachokuja kufanyika Tanzania katika uchaguzi huu mkuu ujao!, maadam kuna kuna watu wameishaandikiwa, Mungu ataifanya mioyo yetu iwe migumu, kwa kuliinua lile "Jiwe Walilolikataa waashi!, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Kuna mambo ukiyafikiri kibinaadamu utayaona kama hayawezekani, lakini "Lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu, linawezekana!" yaani "nothing is impossible under the sun!".

Hii topic ni kudiscuss ideas za rais wetu ajae na sio ku discuss people!. Great Minds discuss ideas, hivyo hawajaji taji majina na ndio maana mmeona kwenye uzi huu, sijataja jina lolote!. Hivyo nakuomba na wewe ujitahidi kuchangia bila kutaja taja majina!, ila ukijikuta unawashwa sana kutaja taja majina, wewe jijue ni simple mind!. Japo Jf was meant to be the home of great minds, but ordinary minds wanao discuss events wapo na simple minds wanao discuss people pia wapo!, na tunavumiliana!.

Namaliza kwa swali, jee hii "Vox Pupuli" tunayoisikia kweli ni sauti ya Mungu?! na huu muujiza wa Jiwe Walilolikataa Waashi, likafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni, unawezekana kwa Tanzania?!.

Kwa vile mimi nafahamika msimamo wangu humu kumhusu "jamaa yetu", hivyo wale mtakaoniadhania namzungumzia yeye, nawaomba mnisomeni kwa makini hapa
"Jamaa yetu!" sio lazima Yeye tuu ndiye awe Rais wetu 2015!.

Nawatakia Jumapili njema!.

Pasco




























555.jpg




222.jpg




99.jpg


 
Umejitahidi kuzunguruka mbuyu lakini target yako kuu ni Lowasa.. Acha uoga we sema wazi kuwa Lowasa ndio chagua la Mungu na chaguo la Watanzania wote..
 
Kwa mala ya kwanza nimesoma bandiko ndani ya JF, Zaidi ya mala mbili, Lakini sijalielewa vizuri. Ngoja niendelee kusoma maoni ya wachangiaji.
 
Safi kijana deep discussion mleta mada kina mtu namuona tayari yupo ikulu kwa jinsi mijadara inavyoenda
Jana namuona rais wetu wa nchi anawambia wajumbe wa nec wamchague mtu anae kubalika na wapiga kura mil 23 na sio wao wajumbe mil6
 
Kwa mala ya kwanza nimesoma bandiko ndani ya JF,Zaidi ya mala mbili,Lakini sijalielewa vizuri.Ngoja niendelee kusoma maoni ya wachangiaji.
Mkuu KALINZI KA NYUMBANI, pole sana!, kuna threads nyingine humu, ili kuweza kuzielewa, kunahitaji level fulani ya uelewa, ila ukiendelea kuzifuatilia tuu threads kama hizo hata kwa kuzisoma tuu bila kuchangia chochote, kuta boost uelewa wako na wewe hatimaye utakuwa unazielewa!.

Na ni kufuatia uelewa huu, utaona wachagiaji wa uzii huu ni wachache wa levels hizo, ila huu ungekuwa ni uzi kumhusu Daimondo na Zari au Wema Sepetu, wengi mgechangia!.

Pole

Pasco
 
Jana nafkiri mkuu wa nchi anajua na anakiri kwamba EL Kwa ccm Hana mpinzani kabisaaa akichukua form anapitiswa sasa kazi ipo Kwa ccm kuwaconvic watanzanzania wamwelew jamaa na wapige kura ccm
 
Mkuu KALINZI KA NYUMBANI, pole sana!, kuna threads nyingine humu, ili kuweza kuzielewa, kunahitaji level fulani ya uelewa, ila ukiendelea kuzifuatilia tuu threads kama hizo hata kwa kuzisoma tuu bila kuchangia chochote, kuta boost uelewa wako na wewe hatimaye utakuwa unazielewa!.

Na ni kufuatia uelewa huu, utaona wachagiaji wa uzii huu ni wachache wa levels hizo, ila huu ungekuwa ni uzi kumhusu Daimondo na Zari au Wema Sepetu, wengi mgechangia!.

Pole

Pasco
Kutokana na uandishi wako naona kama umekubali matokeo vile kuhusu jamaa yako? Sasa unaangalia options mbili,aidha atoke ndani ya kile chama akagombee urais kupitia chama kingine au mbakie ndani ya hicho chama na kuhamishia nguvu kwa mbadala wake.

"Jiwe walilokataa waashi kugeuka kuwa jiwe kuu la pembeni"-mnamaanisha atagombea urais hata ikibidi kwa tiketi ya Upinzani.
"Siyo lazima ni yeye awe rais..."-mnaweza kumuunga mkono mbadala wake kutoka ktk genge lenu.
 
Mkuu KALINZI KA NYUMBANI, pole sana!, kuna threads nyingine humu, ili kuweza kuzielewa, kunahitaji level fulani ya uelewa, ila ukiendelea kuzifuatilia tuu threads kama hizo hata kwa kuzisoma tuu bila kuchangia chochote, kuta boost uelewa wako na wewe hatimaye utakuwa unazielewa!.

Na ni kufuatia uelewa huu, utaona wachagiaji wa uzii huu ni wachache wa levels hizo, ila huu ungekuwa ni uzi kumhusu Daimondo na Zari au Wema Sepetu, wengi mgechangia!.

Pole

Pasco

Mkuu kama nimemuelewa JK ni kwamba Ccm inahitaji ushindi uchaguzi ujao na akidi ya wanachama haitoshi kuwapa ushindi.

Kwa lugha rahisi tu hata kama hatumkubari jamaa yetu mwamba wa kaskazini ni yeye peke yake kutoka Ccm ndio ameonesha kwa vitendo anaungwa mkono na makundi tofauti nje ya Ccm.

Watu wengi hawamjui JK wao wanajiaminisha JK ana ubavu wa kukata jina la jamaa yetu hizi ni daylight dream, kwanza kitendo cha kamati kuu kutamka adhabu yao imekwisha ni pigo kwa kina Mangula wanaotembea na makablasha ya tuhuma.

Kweli ukweli nitasimamia kweli jamaa yetu wanamuonea sana na yeye yupo kimya tu, mimi naijuwa Ccm hakuna mgombea yeyote asiyetumia rushwa kushinda kura za maoni kuanzia ngazi ya mtaa ubunge udiwani hadi urais, wanachozidiana ni dau tu na kwa hili jamaa yetu kawapiga bao kwa mbali mno.

Nawashauri UKAWA wasipoteze muda na sarakasi za maccm mgombea wao oöatakuwa ni huyuhuyu jamaa yetu wajiandae sasa kumkabiri vilivyo maana King maker Rostam yupo anasubiri kipenga tu.

Kwa mtandao wa nje ya chama aliyoutengeneza jamaa yetu ni kichaa peke yake ndio anaweza kukata jina lake Ccm na kuizika Ccm rasmi.
 
Nadhani umejitahidi sana kuandika ila mwisho wa yote vox populi wako ni Lowassa, unataka tukutajie jina ili utuite simple minds lakini ukweli utabaki kuwa tayari una jina lako
 
Swali ni nini?
Jumapili ya leo, naomba tutafakari kwa pamoja msemo huu wa lugha ya Kilatini kuwa "Vox Populi is Vox Dei" ukimaanisha "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu!", au "Kauli ya wengi ni kauli ya Mungu", ikimaanisha "Chaguo la wengi ndilo Chaguo la Mungu!".

Uliza swali kuhusiana na mada hii? Wengi madarasa ya fasihi hatukuhudhuria
 
Mungu anasingiziwa mengi kweli kweli Duniani na haswa Tanzania,lakini Yote hii ni ulaghai na umbumbu pia!!

Hivi Mungu ndo alipanga Kikwete awe raisi na kuwatumia wakina Lowasa na Rostam Aziz wamtafutie uraisi Kikwete??!!

Mungu ndio Kapangwa Ridhiwani Kikwete awe mbunge wa Chalinze huku Baba akiwa raisi na pia Kikwete,Salma na Ridhiwani na yule mjomba wa Bagamoyo wawe wote wajumbe wa NEC??!!

Mungu ndio alipanga Mgabe awe raisi wa Zimbabwe kwa miaka dahali mpaka anakaribia kupoteza fahamu na uwezo wa umakini huku akisema bado tena miaka 25??!!

Mungu ndio alipangwa Daud Mwangosi apigwe bomu mbele ya RPC na askari wanne halafu RPC ndio apandishwe cheo??!!

Mungu ndo kapanga alibino wa Tanzania tu wauliwe na kukatwa katwa viungo vyao na binadamu wenzao??!!

Mungu ndo kapanga Tanzania tuwe masikini ili hali katujaalia kila mali asili yenye utajiri??!

Mungu ndo kapanga viongozi wetu baada ya Nyerere wakubuhu kwa wizi na ufisadi huku wakijali tu nepotism??!!

Pasco mkuu najua unajua na unakubali unaabudu brown envelopes,je siku hizi unakula maharage ya wapi??!!

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
Hii topic ni kudiscuss ideas za rais wetu ajae na sio ku discuss people!. Great Minds discuss ideas, hivyo hawajaji taji majina na ndio maana mmeona kwenye uzu huu, sijataja jina lolote!. Hivyo nakuomba na wewe ujitahidi kuchangia bila kutaja taja majina!,SASA HAPA UMEJADILI EVENTS/ISSUES AU UMEMJADILI MTU? yule jamaa yetu, just simple mind.
 
Back
Top Bottom