Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,209
- 25,548
Ni Ibara ya 99 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inabeba dhana ya utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mambo ya fedha. Ibara husika ina ibara ndogo 3. Tafadhali someni Ibara hii na mjiridhishe iwapo Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M. Lissu alikuwa sahihi au la kwenye hoja yake ya kuhusu 'mamlaka ya Rais kikatiba na masuala ya kodi/tozo'.
Nainukuu:
99.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.
(2) Mambo yanayohusika na ibara hii ni haya yafuatayo:- (a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(ii) kuangiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko wa Serikali mwingine wowote au kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine yoyte isipokuwa kupunguza; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(iii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko wa Serikali mwingine wowote wakati ikifahamika kwamba fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo yaongezwe;
(iv) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) hoja au mabadiliko yoyote ya Hoja kwa ajili ya lolote kati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya ibara hii ndogo.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa muswada wowote uliowasilishwa kwenye Bunge au Hoja yoyote iliyotolewa katika Bunge na Waziri au Naibu Waziri.