KERO Hela ya malipo ya transcript imelipwa lakini bado NACTE hawataki kuitoa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

OCCID Dominik

Member
Apr 29, 2024
64
59
Wakuu habari ya muda..mdogo wangu amehitimu ualimu miaka minne nyuma sasa punde baada ya kuhitimu huwa wanapewa mapema ACADEMIC CERTIFICATES kuliko vyeti vingine..kwa hiyo alifanikiwa kuipata mapema tuu sasa Kimbembe ikawa kupata TRANSCRIPT.

Pesa ilishalipwa katika control number husika na sms ya kuthibitisha na NACTE akapata ila mwaka umeisha NACTE hawataki kumpa TRANSCRIPT.

Baada ya kutuma hela katika control number alipata ujumbe kwenye simu kuwa,"NACTE HAS FAILLED TO PROCESS YOUR TRANSCRIPT BECAUSE THE RESULT HAS SOME PROBLEMs".

SWALI:Je iwapo matokeo yana shida ni kwa vipi akapata academic certificates? Yeye alisoma iringa kwa hiyo huwa anaenda kwenye office ya NACTE kanda kusini pale Mbeya Uhindini wanamzungusha tuu hawamwambii kinachoendelea.

Kwa wenye experience na haya mambo wakuu ushauri wenu maana tunahitaji aipate mapema sababu ni lazima kwenye maombi ya ajira.
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    93.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom