Hayati Magufuli aliua upinzani, Rais Samia Suluhu ameuzika rasmi

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,525
6,470
Tangu 2015 JPM alipoingia madarakani, kubwa zaidi alifanikiwa ni kuua upinzani na CCM ilipata kutamba kweli kweli pasi na kupingwa na chama chochote

Muda mfupi tu tangu Rais Samia Suluhu kushika nafasi kuiongoza nchi hii upinzani umezikwa rasmi.

Kwa sasa Tanzania haina upinzani tena, si ACT, CUF wala CHADEMA kinaweza kuipinga serkali hii ya CCM chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa anayoyafanya Rais ni wazi sasa upinzani umezikwa hapa nchini baada ya kuuliwa na hayati Magufuli
 
Hakuna upinzani tena...at least kwa muda wote ataotawala Mama Samia.

Bogeyman wa upinzani hayupo tena.

Huyu mama hawawezi kumsema vibaya.

Wakimsema vibaya, wataambiwa wanamsema vibaya kwa vile ni mwanamke.

Hawana jinsi tena. Ni kuunga mkono juhudi tu sasa.
 
Rais aliyepita alitumia nguvu kuua upinzani lakini wakati anaanza Urais watu waliamini matendo yake yani utendaji wake tu unatosha kabisa kuuwa upinzani na iliaminika wapinzani hawana tena hoja lakini ulionaje.

Kwahiyo watu wamekaa mahali wanaangalia muelekeo wa upepo bado haijafahamika direction lakini mambo ni mengi Sana wapinzani wana hoja nyingi tu ambazo zitazua mijadala mipana sana kwa kuwa uongozi uliopita umeacha matatizo mengi tu ya uvunjaji wa Katiba na vitu vingine.

Lakini kama Rais ni mwenye kiti wa CCM na CCM ndiyo ipo tangu na tangu itabidi ujipange pia kujibu mapungufu ya watangulizi wako
 
Yeye kafa kauacha upinzani. Upinzani hawezi kufa kamwe, unaweza kudhoofisha vyama vya upinzani ila huwezi kuudhoofisha. Angalia sasa kuna watu walikuwa karibu sana na yeye wameanza kuonyesha kwamba walikuwa wapinzani wake
 
Kwa lawama za jiwe , mama Samia anapata Neema , hata hvyo Mo Dewij ni billionaire Kwa hustling za Mzee wake .....
 
Weka akiba ya maneno. Magufuli alikuwa na majitambo kama haya. Leo siku ya pili yupo ndani ya kaburi. Ila hesabu za CAG inaonesha ameikagua pia CHADEMA. Chama mfu kinakaguliwa mahesabu yake?
 
Kilichofanywa hakikuwa kwa ajili ya afya na ustawi bora wa taifa letu, bali afya na ustawi wa kundi la wachache .Ni matumaini yangu kua mwanga umeanza kuonekana, na mwanzo mpya wa mustakabali mwema wa taifa letu .
 
Hakuna upinzani tena...at least kwa muda wote ataotawala Mama Samia.

Bogeyman wa upinzani hayupo tena.

Huyu mama hawawezi kumsema vibaya.

Wakimsema vibaya, wataambiwa wanamsema vibaya kwa vile ni mwanamke.

Hawana jinsi tena. Ni kuunga juhudi tu sasa.
Katiba Mpya....hili tu linatosha kumuyumbisha madam....kama atalikwepa kina Warioba wapo hai ujue
 
Hakuna upinzani tena...at least kwa muda wote ataotawala Mama Samia.

Bogeyman wa upinzani hayupo tena.

Huyu mama hawawezi kumsema vibaya.

Wakimsema vibaya, wataambiwa wanamsema vibaya kwa vile ni mwanamke.

Hawana jinsi tena. Ni kuunga juhudi tu sasa.
Katiba Mpya....hili tu linatosha kumuyumbisha madam. Kama atalikwepa. Kina Warioba wapo hai ujue
 
Upinzani ndio umemuua huyo Hayati wenu kwa dua na matambiko

Nyerere alifuta vyama vingi tena kwa kubadili Katiba kabisa, akakaa madarakani miaka 23, miaka zaidi ya 30 baadae ikabidi atengue kauli take mwenyewe maana aliona ku suppress mawazo mbadala haina afya kwa taifa

Kama Nyerere hakuweza kuua Upinzani kwa miaka zaidi ya 30, tena kwa kubadili Katiba kabisa, Magufuli ndio aweze ndani ya miaka 5 kwa njia ambazo hata sio rasmi
 
Hakuna upinzani tena...at least kwa muda wote ataotawala Mama Samia.

Bogeyman wa upinzani hayupo tena.

Huyu mama hawawezi kumsema vibaya.

Wakimsema vibaya, wataambiwa wanamsema vibaya kwa vile ni mwanamke.

Hawana jinsi tena. Ni kuunga juhudi tu sasa.
Kama ataongoza vizuri, why not! Upinzani unakuwepo pale ambapo hukubaliani na anachofanya. Of course hawezi kuwa perfect kwa kila jambo lakini kama akijitahidi kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyokuwa yanasemwa kila mtu ataridhika na wapinzani wanaweza kujiunga kwenye serikali yake kumsaidia kama ataona kuna umuhimu.
 
Upinzani ni falsafa yenye mtizamo ya kutofautiana, kupingana au kushindana na yule anayetawala kwa muda huo.

Upinzani ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo milele kadri maisha na watu wanavyoendelea kuwepo. Ukitaka kuua upinzani kwenye jamii basi ondoa maisha na ondoa watu wasiwepo mahali ulipo.

Tanzania kikatiba ipo kwenye mfumo wa siasa za vyama vingi, hivyo upinzani ni suala la lazima kikatiba. Upende au usipende upinzani utaendelea kuwepo. Kama yalivyo maji na maisha ya mwanadamu, huwezi kuyakwepa.
 
Turuhusiwe kufanya Siasa za Majukwaani ili Mama atawale kwa Amani
Mchakato wa Katiba Mpya uanze kama mtatuona tukimsimanga
Mkuu upinzani siku zote huwa mkali pale ambapo kiongozi anakwenda kinyume na matarajio ya jamii anayoingoza. Kama atajitahidi kufanya vizuri mbona hatakuwa na upinzani? Ndiyo maana tulikuwa tunapiga kelele kipindi cha Magufuli kuwa asiue upinzani kwa kuunyima demokrasia kwani hatafaulu bali aue upinzani kwa kuongoza vizuri kulingana na matakwa ya watu.
 
Back
Top Bottom