Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 138
- 229
Taarifa ninazozijua ni kuwa Serikali ilitoa zaidi ya Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya machinjio hayo kwa ajili ya kata hizo mbili tangu Mwaka 2013.
Hadi sasa hakuna kinachoendelea na baadhi ya fedha za mradi zilipigwa, uonekano wa machinjio hizo na kiasi cha fedha ambacho inadaiwa kimetumika ni tofauti, japo viongozi waliopita walijaribu kufatilia ila huwa mambo yanaishia njiani bila kupata suluhisho la suala hilo.
Kutona na hiki unachokiona kwa sasa wauza nyama wanachinjia kwenye eneo la TRC ambapo awali yalikuwa makazi ya Watu, baada ya TRC kuwalipa fidia ili kupisha ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR.
Eneo hilo wanalofanyia shughuli za machinjio ya Wanyama hakuna mkaguzi anayekagua usalama wa nyama.
DIWANI AULIZWA
JamiiForums imewasiliana na Diwani wa Kata ya Goweko ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Uyui, Shabani Katalambula anaelezea:
Suala la fedha sina uhakika nako labda aulizwe Mkurugenzi Mtendaji ndio msimamizi wa fedha, mimi nimeingia Udiwani Mwaka 2014 sikuwahi kuona Mradi huo umetengeza fedha.
Ninachokumbuka kwenye miaka ya 2010 kulikuwa na fedha zimetengezwa zinzotokana na mapato ya ndani kama sijakosea.
Pamoja na hivyo kuna changamoto kadhaa ikiwemo ya maji pamoja na kwamba wakati wa ujenzi walikosea upande wa Kibra.
Taarifa nilizozipata kwa miaka hiyo, walipofika Waislamu kuangalia wakagundua kuna hicho changamoto kidogo.
Hivyo, Wachinjaji wanachinja pembezoni mwa eneo hilo, pembeni ya eneo hilo la Machinjio yaliyejengwa
Kuhusu suala la Afya wapo maafisa ambao huwa wanakagua, unajua wafugaji wetu sio wakubwa kama ilivyo wale wa mijini, Halmashauri yetu ya Uyui haijafikia kiwango hicho cha kuwa na machinjio makubwa.
Pia soma - Mradi wa Machinjio ambao hautumiki, DC w Uyui asema wametenga Tsh. 14m hadi 24m kuuboresha