NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
85
133
tWsSvb09WEC1d6Kcr53BTZ6w7PmzVuSyKpJ-nAjSNbbKze2Aettn3zcGnf8h1ZRdsdLP8KFB6fd62-JkZfky3fJ6EZFtOHTnxXpeBZQWjsTpUPelxP5r9yHNy0kV4ZOdReXNPQdw


Habari za muda huu, leo nmeona itakuwa vema kushare na wana JF, nakala hii ambayo inaelezea hatua ambazo mimi huwa ninatumia kutengeneza websites zenye thamani kubwa na zinazozalisha matokeo makubwa.

Watu wengi sana wanafahamu jinsi ya kutengeneza websites, lakini wengi wao websites zao huwa hazileti matokeo wanayotarajia hata kidogo na hii ni kwasababu wote hao huwa wanatengeneza websites bila kutumia utaratibu mzuri.

Wengi huanza moja kwa moja kufungua editor au builder za websites (yani, html editor, wordpress, wix, n.k) na kuanza kutengeneza moja kwa moja kwa kutumia idea tu walizonazo kichwani. Na ndio maana websites nyingi zinafeli kuleta matokeo mazuri.

Kwa ufupi watu wengi huwa wanaruka hatua nyingi ambazo ndio za muhimu sana katika kutengeneza website.

Zifuatazo ni hatua 12 muhimu ambazo huwa nazitumia kutengeneza websites za thamani kubwa.

HATUA 1: KUELEWA MATATIZO NA MALENGO (CONSULTATION)

jTQMcmSTuRUI8FNq0p_FcPmO2E2j7eoH6IyUgbMzF6sAH5YKQUBGdjHe3AFoF0vrj3GBxMVl_lJgqoW7X1QmLgzofumv5i8kikZM78j1w_GLavZYnOAHYWIPPHRfXEqBrKLwv6n2



Hii ni hatua ya mwanzo kabisa na muhimu sana, ambapo hapa, najaribu kuuliza na kuangalia ni matatizo yapi ambayo biashara au kampuni husika inapitia, ambayo kupitia website yataweza kutatuliwa.

Lakini pia najaribu kuuliza na kuangalia malengo yao ni yapi ambayo yamewafanya kutaka kuwa na website kwa ajili ya Brand au Kampuni yao.

Hata kama unatengeneza website kwa ajili yako mwenyewe, jaribu kujiuliza maswali juu ya matatizo yanayokufanya uhitaji website na malengo unayotamani kuyafikia kupitia hiyo website.

Ni vema ukawa na notebook ambayo unakuwa unaandika taarifa zote unazopata hapa, kwa maana taarifa hizi ni muhimu sana kwa hatua za mbeleni.

HATUA 2: KUFANYA UTAFITI (RESEARCH)

3G-fMD8HIEu6iZGggtp8Dbl_Y_iGs-wKdIhBFzmCWqpMcb0JayFw8IjBXL3hyotrKOAdFR1RLI9Pyf94tZ89zYNkO_sbgdtg_8IQWOfR42-VcbgAF1IY0DQrhCmPM25wp1JiEuSf



Baada ya kutambua matatizo pamoja na malengo, sasa naanza kufanya utafiti ili kupata namna nzuri ya kuyatatua hayo matatizo na kufikisha hayo malengo kupitia website nitakayotengeneza.

Utafiti huu huwa naufanya kwanza kwa kuangalia soko linafanyaje, yani naangalia website tofauti tofauti kitaifa na kimataifa pia, ambazo ziko kwenye aina ya biashara inayofanania na hii nnayoshughulika nayo kutengeneza website.

Kisha naandika taarifa muhimu nnazopata kupitia website mbali mbali za kufanania, lakini pia naandika pembeni majina ya websites hizo ili zije kunisaidia kwenye ujenzi wa muundo wa website baadae.

Lakini kama aina hiyo ya biashara ni wazo jipya kabisa, basi hapa itanilazimu kufanya utafiti kwa kuuliza watu mbali mbali ambao wanaweza wakawa ni wateja wa biashara hiyo, ili nijue ni vitu gani ambavyo wataweza kunufaika navyo kwa uwepo wa website hiyo.

HATUA 3: KUTENGENEZA MPANGO MKAKATI (STRATEGY SESSION)

-dO9M7QwBc8b0TTLQRfRO3v95_FrzOPqHOzrNglLfqvcFOGMtZZ-v7ERBaLAppSlWi3I50YE5yLqCab3MxxPr9C-s1oKGGw3PEtjuF_1Y2wXvk8oy8hKbGxoRnNCJJqGGDbMtd6p



Mara baada ya kupata taarifa mbali mbali kutokana na utafiti nlioufanya, sasa nakaa chini kuandaa mkakati wa kipekee na ulio bora, ambao huo ndio utakaokuwa ramani kuu katika kutengeneza hiyo website.

Mpango mkakati huo, utakuwa ukihusisha vitu kama, sitemap, visual direction, content type, brand story, website structure, website flow, time, budget, n.k.

Naandika kwenye document au slides mpango mkakati huo, kisha tunaujadili na mliliki wa kampuni au biashara. Then tunarekebisha na kuupitisha.

HATUA 4: KUANDAA MAUDHUI KWA AJILI YA WEBSITE (CONTENT DEVELOPMENT)

Uy16_dBi7nL4dMdbT2mf3F46Xh3-I2XOdDQr832RJKeVQE9Z1GnrzI6QGpVmqCW7JzxaSLfLzTCkataSBPuaUmofQL7Izb4r3-r9kvLn0mXxS6_Ye3-i78oVfuKKfil8eyUwf0JS



Watu wengi sana huwa wanakimbilia kutengeneza website, kabla hawajaandaa content (maudhui), hiyo ni mbaya sana na inafanya kazi kuwa ngumu na kutokuwa na mvuto.

Hivyo basi ni vema kuifanya hatua hii ya kuandaa maudhui kabla hujaanza kutengeneza Website yenyewe. Naeleza haya kutokana na uzoefu wangu.

Kiukweli kazi ya kutengeneza website huwa rahisi zaidi pale ambapo unakuwa tayari umeshaandaa kila kitu yani Maandishi, Picha, Video na vinginevyo vyote. Unakuwa umebakiwa na kazi moja tu ya ujenzi wa website.

Nakushauri uandike kwenye document maudhui yako yote katika mpangilio mzuri, yani kwa kila ukurasa wa website, content yake na uandike mahali itakapo kaa kwenye ukurasa wa website.


HATUA 5: KUTENGENEZA MUUNDO WA WEBSITE KWA KARATASI NA PENI (LOW FIDELITY WIREFRAMING)

XpAs5ZplzGFeXrfhrWqNm-Va2q4X2tEmZQtWRWZHv4zuIuy6_3UjSZ2D-KJmT88q8cHwJuTp0NGX4nSebyaDf7fy8x-6iNcyGvXyfkl6EE5h7_DdzUvL2aM93r_EFfbJgxCOAH1v


Katika hatua hii nachukua daftari na kalamu, na kuanza kutengeneza muundo wa website kutokana na taarifa nlizokusanya kwenye utafiti nlioufanya hapo mwanzo.

Huwa naanza na ukurasa wa mbele kabisa ambao ndio mkuu, kupitia hapo inakuwa rahisi kupata ubunifu wa kurasa zinazobaki.

Katika kuchora website kwenye karatasi, naweka pia maandishi ya vichwa vya habari ili kupata picha kamili ya ubunifu wangu, japo kwa mbali kiasi.

Nachora miundo tofauti tofauti kisha mwisho wa siku, ntaangalia upi utakaofaa zaidi. Hata hivyo badae naweza nkawa nabadilisha vitu mbali mbali, ila angalau nakuwa na uelekeo mzuri kwanza.


HATUA 6: KUWEKA MUUNDO WA WEBSITE KIDIGITALI (HIGH FIDELITY WIREFRAMING)

6OZ-MH7vxVVdanW3yEwNGJJXhCuQJTNAaP8TNIFh390qAbGmGr0lmMBP-dhoa8JVJ2ZJQbiWAI3axyJ3iANGBvOh5emEbkgwSwe658sEXEDCS4S_ltmBsOWQI3Lh6Si1E57KxAnI




Hapa nachukua mchoro wangu wa kwenye karatasi nlioupitisha, kisha natumia programu za computer kama, figma, adobe xd au sketch, kuuweka katika mfumo wa kidigitali zaidi.

Situmii rangi mchanganyiko katika kutengeneza muundo huu kwenye hii hatua, natumia rangi aina moja tu, pamoja na nyeupe au nyeusi, basi.

Pia hapa ntaweka na maandishi yote (bila picha), ili nione uhalisia na uhusiano kati ya kilichoandikwa na muundo wa website.

HATUA 7: UBUNIFU WA MUONEKANO KAMILI KWA KUTUMIA PROGRAMU (VISUAL DESIGN)

X9dS6jp1VLLNhtsBZv_ycRoRhRC9W3ijFCMXazK1jDe-YnJnkZh1v8Sw7rC91egmTxngpxfSbcvc4UwqRb5cevmeklfuwKhlsvLbgtvcECivYo1tXUN2B8mF7XeGhWzSAaMpc-7k



Hapa sasa ndipo ambapo kazi ya kufanya ubunifu wa website inapo kamilika. Kwenye hatua hii natumia programu za ubunifu za computer (design tools) mfano figma, kutengeneza muonekano kamili wa website.

Picha, aina ya miandiko, rangi, maandishi na kila kitu kinachotakiwa kuwepo kwenye website nakiweka hapa.

Hatua hii na hizo nyingine zilopita za kutengeneza muundo wa website, muhimu sana kwa maana, huku ni rahisi mno kutengeneza sura halisi ya website yako.

Hivyo utakapoanza kuijenga kwenye Wordpress au Html n.k, utakuwa unaangalia tu ulichotengeneza hapa na kukibandika huko. Kwa ufupi hutoumiza kichwa kwenye suala la ubunifu tena.

Ni rahisi sana kufanya hii hatua unachohitaji ni ubunifu wako tu. Binafsi napenda pia kufanya hivi kwasababu nikitaka kubadili chochote ni rahisi mno, kuliko nikiwa kwenye ujenzi kabisa kule kwenye Wordpress mpaka nianze kufungua mafaili mengi mengi, ni usumbufu sana.




HATUA 8: KUTENGENEZA PROTOTYPE (PROTOTYPING)


x4gJe9EeD8uRZfFhcxd6WlZIHGVnsEj-CSsnQS-YHUM0_8VHUE5SAbqWcb6GWp3RGpBuXk8c9FonP09oAzf7g5F8SnkBN7xlchYLgIPq4mUEiaT4cck5KZHLqGrMmu07NPq2JRue



Prototype ni kama mfano wa kitu halisi, au kivuli cha kitu halisi (au sample). Kwahiyo unapotengeza prototype ya website mara baada ya kutengeneza ubunifu (visual design) kwenye programu, inamaana unajaribu unatengeneza uhalisia wa website itakavyokuwa kwa mtumiaji.

Visual design inakuwa kama picha tu, lakini prototype inakuwa kama kitu halisi kabisa, japo bado haitaweza kuwa kamilifu, ila unaweza kufanya baadhi vitu kama kubonyeza kitufe na kutokea kitu.

Hii inanisaidia kugundua changamoto ambazo mtumiaji wa website, anaweza kuzipata wakati anaperuzi kwenye website yangu nnayojenga, na kwahiyo najitahidi kuondoa changamoto zote kabla sijaiweka website yangu kazini.

Ni rahisi mno, kufanya prototyping kwa sababu kifaa hicho hicho (figma) nnachotumia kutengenezea muonekano kamili wa website, ndipo huko huko moja kwa moja natengeneza prototype, kwa kubonyeza tu sehemu kadhaa.

TAZAMA HIYO PROTOTYPE LIVE HAPA:
https://bit.ly/3uoqqyI

HATUA 9: KUFANYA MAREKEBISHO YA UJUMLA (REVISIONS)

HqRV5-BImRYbi89OVfLk4wxz_KBc0MLF23j4smvwrjlvYvFc0yp3GpSyekQ8cqYaxrWHh6jfF7HEDzNycDmjS05jUm-r1TCfXU9It_wlp3puEnxsXssJvxEm7QOrUNZdmj4Ei_DW



Kwenye hatua hii sasa, huwa nahakikisha nmefanya marekebisho yote ambayo yanahitajika, kabla sijaanza kutengeneza website halisi.

Ntaangalia kuanzia picha, maandishi, miundo, na kila kitu kwenye website yangu nliyoifanyia ubunifu.




HATUA 10: KUTENGENEZA WEBSITE HALISI (DEVELOPMENT)

4_UEVQ8mZJrOuo2VS-7gg_w32SYwHhJGd7rDjc_S2cPoQ7W4T38kR4e8-vqdSgIfoImdwt2hGKQ1NXKhO1L6n6QZzjFFqVVBijsJ8mk6X2CzIecQegY2SSWEAUG08WACM5g2etAf


Kufikia hatua hii kazi inakuwa rahisi sana. Ninachokifanya baada ya kukamilisha marekebisho yote, ninakusanya mafaili (picha, icons) yote nliyotumia wakati natengeneza mtindo wa website kwenye hatua zilopita.

Kisha baada ya kuhakikisha mafaili yote yako tayari, kazi ya kutengeneza website yenyewe inaanza.

Binafsi natumia WORDPRESS kwa sasa kutengeneza website zangu, kwahiyo nitanunua Domain na Hosting, na install Wordpress yangu, kisha naendelea na ujenzi.

Sitoweza kuonesha hatua kwa hatua jinsi nnavyotengeneza website kwenye WordPress,
Kwa sababu ni somo refu kiasi, lakini sio ngumu kwa sababu tayari unavyanzo na rasilimali zote kwa ajili ya ujenzi wa website yako.


HATUA 11: KUFANYA MAJARIBIO NA MAREKEBISHO (TESTING & REVISIONS)

mY6pkfPW2GbkjPyfEda1NSzg-VuAI9vqFnDlYFY4ukE7RQyfzCpbZIvXslJp24sLIALQnr07iRZ-_16ki8dodvFf3PQBMDMX5bwr2ouxl7UxmDu7HcPTmdBH3BLsHpsedwv96gwL


Mara baada ya kuitengeneza (develop) website yangu kwenye Wordpress, hatua inayofuata ni kufanya majaribio, ili kuhakikisha kama kila kitu kinafanya kazi kiusahihi, kabla sijaiweka website mtandaoni.

Pia ntaangalia na kukagua kama kuna mahali popote panahitaji marekebisho, kisha niyafanye hayo yote na kuendelea na hatua ya mwisho.

HATUA 12: KUCHAPISHA WEBSITE MTANDAONI (LAUNCHING)

qO8iYPhQuFoQV4rFrIJmvMvm3fc0qle3AsF-mQO6AzCx397VeDjEWVCQeQhWu-mlXho4aRlNqcyzujAUm6tu-Di2Qkno802Em1CcMoVTIvPklrSDQR46lCNYooo79P7a-ld5_dkW



Katika hatua hii nakwenda kuruhusu sasa website ipatikane kwenye mtandao wote. Kwenye Wordpress hili ni jambo rahisi mno kufanya. Unachokifanya ni kubonyeza kitufe tu kilicho andikwa “Publish”.

Ila hakikisha kila ukurasa umefanya hivyo, yani kubonyeza “Pupblish”, la sivyo kurasa nyingine hazitoonekana.

HITIMISHO
Nakuhakikishia kama utapitia kwa utaratibu na kwa usahihi hatua hizo zote, na kwa undani zaidi, basi hutotengeneza tena websites zenye thamani ya laki 2, 3 au 4. bali utakuwa unatengeneza websites za thamani zaidi ya Milioni 4 na zenye kuleta matokeo mazuri kwenye biashara husika.


Imeandaliwa na Erick Ngimba
Email: hello@erickngimba.com
Whatsapp: 0627 813 264
2021 -
Erickngimba.com
 
Baada ya kuitembelea tovuti na nikiangalia hii post nimegundua kuwa unafanya MARKETING ila bandiko lina upotoshaji (sina lengo la kukuaribia biashara)

Ndugu, upotoshaji gani huo, mimi nmeshare kile ninachokifanya na ninachokifahamu au unaona wivu mimi kufanya hivyo ... naomba tafadhali uoneshe upotoshaji wangu uko wapi hapo, au nmemuomba mtu fedha?? maana ninachokiona ni kuwa kama unajaribu kupinga tu, na wakati kila ulichouliza nimekujibu.
 
Baada ya kuitembelea tovuti na nikiangalia hii post nimegundua kuwa unafanya MARKETING ila bandiko lina upotoshaji (sina lengo la kukuaribia biashara)

Wewe kama unaona Post yangu haijakufunza chochote basi acha sio lazima kufata, na pia kama kuna kitu unakiona hakipo sawa basi sema na uoneshe unachokiona wewe kipo sawa.
 
Back
Top Bottom