Hashim Mbita alivyoleta uhuru wa Sao Tome and Principe

hawa akina Zitto ndio aina ya viongozi tulionao leo. wanapenda kuusimulia na kuuelezea uzalendo lakini hawawezi kuutekeleza kwa vitendo. wanatufundisha waliyofanya akina Mbita, ila wao wako bize na ACT wakipambana na wapinzani wenzao. eti wanajiita wazalendo! watamfikiwa Mbita hata kwa robo tu ya uzalendo wake?
 
hawa akina Zitto ndio aina ya viongozi tulionao leo. wanapenda kuusimulia na kuuelezea uzalendo lakini hawawezi kuutekeleza kwa vitendo. wanatufundisha waliyofanya akina Mbita, ila wao wako bize na ACT wakipambana na wapinzani wenzao. eti wanajiita wazalendo! watamfikiwa Mbita hata kwa robo tu ya uzalendo wake?

huna unachoelewa wew,zito hakutaka kuongozwa na six 0
 
Hashim Mbita alivyoleta uhuru wa Sao Tome and Principe

Jumatano tarehe 29 Aprili 2015 Mtanzania aliyetukuka na Mwafrika asiye na chembe ya mashaka anapumzishwa katika nyumba yake ya milele. Huyu ni Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) 1972 - 1994 na mtumishi wa Umma wa Tanzania akiwa Balozi na nafasi nyingine mbalimbali ikiwemo kuwa msaidizi wa Mwalimu Nyerere.

Wakati tunampumzisha Mzee Mbita nimeona kuwashirikisha habari moja ambayo watu wengi hawaifahamu na mimi niliisoma kwenye Kitabu nikiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka ya mwisho ya Tisini. Hii ni hadithi ya kipekee kabisa ya namna Hashim Mbita alivyoharakisha Uhuru wa nchi mojawapo ya Afrika kwa mazungumzo yasiyo rasmi tu.

Moja ya kazi ambayo Kamati ya Ukombozi ya OAU ilikuwa ikifanya ilikuwa ni kutafuta vikundi vya ukombozi katika mataifa ya Afrika yaliyokuwa yakitawaliwa na wakoloni. Visiwa vya Sao Tome na Principe vilikuwa chini ya ukoloni mkongwe wa Ureno lakini hapakuwa na vyama vya ukombozi vyenye nguvu.

Hashim Mbita alipoteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi alianza jitihada za kutafuta watu wa visiwa hivi ili kuunda vyama vya ukombozi. Huu ulikuwa ni wakati wa mapambano makali dhidi ya Wareno katika nchi za Msumbiji, Angola na Guinea Bissau na Cape Verde kwa Amilcar Cabral. Baada ya jitihada kidogo wakajulishwa kuwa kulikuwa na kikundi kinaitwa Committee for the Liberation of Sao Tome and Principe (CLSTP). Hata hivyo chama hiki hakikuwa hata na ofisi na hivyo Hashim Mbita akaagiza kutoka kwenye Bajeti ya Kamati ya Ukombozi kuwa wapewe dola 1000 za kimarekani ili kuweza kufungua ofisi jijini Libreville, Gabon.

Chama hiki cha ukombozi kilikuwa chini ya mtu anayeitwa Miguel Travaola. Hata hivyo mahusiano yalikuwa sio mazuri sana kutokana na kukosekana kwa umakini wa chama hiki cha ukombozi. Lakini Mbita hakuchoka aliendelea kuwasiliana nao na kuwataka wajipange vizuri ili kuanza kazi ya ukombozi. Kamati ya Ukombozi iliendelea kuwalipia ofisi na kuwasaidia kuendesha migomo na maandamano katika visiwa hivyo ili kupaza sauti ya ukombozi. Hata hivyo CLSTP haikuwa na nguvu kabisa nchini mwao na viongozi wao walikuwa wakitoa taarifa za uongo kwa Brigedia Mbita hali ambayo iliwafanya washindwe kuanza mashambulizi ya kumtoa Mreno Sao Tome and Principe.

Akiwa safarini jijini Maputo kwa ajili ya kuandaa shughuli za uhuru wa Msumbiji, akiwa ameambatana na Joachim Chissano aliyekuwa Waziri Mkuu wa Msumbiji wakati wa mpito, Hashim Mbita akakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno Mario Soares. Kiutani tu lakini akiwa amekunja ndita Mbita akamwuliza Soares “ lini mnawapa uhuru watu wa Sao Tome and Principe”? Soares akamwuliza Mbita kama kuna watu wan chi hiyo wanaotaka Uhuru. Mbita akamjibu ndio wapo. Akamwuliza tena kama kuna chama chochote cha ukombozi huko ambacho anaweza kuongea nacho ili kuwapa uhuru, Mbita akajibu ndio kipo. Waziri huyu wa Ureno akasema basi nikutanishe nao tuanze mazungumzo.

Hashim Mbita aliporudi Dar es Salaam akatuma ujumbe kwenda Libreville na wakati huo CLSTP ilikuwa imepata kiongozi mwingine Dkt. Manuel Pinto da Costa. Akamwita aje Dar es Salaam, akampa salaam zile na wakakubaliana na Serikali ya Algeria kuwa mkutano wa mazungumzo ya uhuru wa Sao Tome and Principe yafanyikie huko.

Ndani ya mwezi mmoja mazungumzo yakaanza mnamo tarehe 23 novemba 1974 na Chama cha CLSTP kikaunda Serikali ya Mpito. Tarehe 12 Julai 1975 nchi ya Sao Tome and Principe ikapata Uhuru wake kutokana na mazungumzo ya utani tu na kukunja ndita ya Brigedia Jenerali Hashim Mbita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno. Wakati watu wa Angola, Msumbiji na Guinea Bissau walishika mtutu wa Bunduki kutafuta Uhuru wao, Sao Tome and Principe walipata uhuru wao kwa kazi ya mtu mmoja tu asiye raia wa nchi hiyo lakini mkombozi mkubwa wa bara la Afrika Hashim Mbita kutoka Tabora, Tanzania.

[Habari hii imesimuliwa kutoka kutabu cha Inside OAU – Pan-Africanism in Practice kilichoandikwa na C.O.C Amate. ]


Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Hashim Mbita mahala pema peponi. Amin

aamin rabin alamiin,MUNGU aendelee kukutunza inshallah,vitu hivi ni ngumu kwa mtu kichwa maji kufaham.
 
Mbona alikimbia ya akina sheikh Mkwawa,Sheikh Kije,na wale wamanyema waafrica wa first class pale Dar...?Mbona hakulalamika kwanini historia imeutoa usheikh wao,na kuwatoa ktk biashara na upiganaji wao mkubwa wa jihad?

Ungewajuwaje hao bila kuwasoma? tukuulize, uliwasoma wapi?
 
Kumbuka sijasema kwamba sisi Waafrika hatukupigania Uhuru wetu, HAPANA, uulipigania sana tena hamna hata haja ya kwenda mbali sijui kwa Msumbiji au Sao Tome bali hapa hapa kwenye ardhi yetu kuanzia Vita vya Maji Maji mpaka kwa akina Mkwawa n.k na tumepoteza watu wetu wengi sana tu kwanza hata kabla ya akina Mkwawa watu wentu walikuwa wanapigana na wageni ila haya mapigano siyo yaliyoleta Uhuru Afrika, yaani Wazungu hawakutoa Uhuru TanZania kwa kuwa Mlm.Nyerere aliawashinikiza au Waingereza hawakutoa Uhuru Kenya kwa sababu sijui ya Mau Mau hapana, Wazungu walitoa Uhuru kwa sababu muda ulikuwa umefika na ndio maana nchi zote za Kiafrika tuliapata Uhuru karibu wakati mmoja miaka ya sitini mpaka sabini lakini siyo kabla ya hapo!
Ukisikia BRN hii ndo yenyewe pure!
 
Ungewajuwaje hao bila kuwasoma? tukuulize, uliwasoma wapi?
Haha...kwanini kasema kuwasoma ni issue hapa....?niliwasoma sehemu nyingi san,na nikafany deep analysis.kwanini usiende ktk fact tuuu unataka uliza nini?
 
Kiutani tu lakini akiwa amekunja ndita Mbita akamwuliza Soares...

... kutokana na mazungumzo ya utani tu na kukunja ndita ya Brigedia Jenerali Hashim Mbita
Katibu wa taasisi ya kutafuta uhuru kwa nini aulize swali kuhusu kutafuta uhuru kwa utani? I mean, kwa nini tuichukulie seriously hadithi ya efforts za mtu ambazo yeye mwenyewe alizichukulia kiutani utani? Nothing short of ridiculous.

Mwafrika asiye na chembe ya mashaka anapumzishwa
Mwafrika gani ambae ana chembe ya mashaka, singa singa wa Escrow??

habari moja ambayo watu wengi hawaifahamu
Unajuaje watu wengi hawaifahamu? hahahahaaaaaaaaa!
 
Ndiyo hapo sasa pa kujiuliza hivi Waingereza na Military yao yote ile wangeamua kubakia Tanganyika ni nani angewazuia? Sisi tulikuwa na Jeshi gani la kuweza kuwaondoa? Tunasoma hata ktk Historia Mkwawa mara ya kwanza aliwauawa Wajerumani kwa sababu walimdharau lakini mara ya pili Jeshi la Wajerumani liliwamliza wote kwa mara moja tu na kuendelea kutawala sasa tulikuwa na nini cha kumtoa Mzungu kwa nguvu?
kama hujui historia ni bora ukae kimya, kuliko kuandika usicho kijua, vita vya wahehe na wajerumani havikuwa vya mara moja kama unavyoudanganya umma, ilichukua miaka minne mpaka mkwawa kujipiga risasi, haikuwa rahisi hivyo kijana
 
Hapa ndipo unaona tofauti ya ZZK na baadhi ya viongozi wa SACCOS kwenye masuala yenye kuhusu uelewa mpana wa mambo ya kimataifa. Wao wanachojua ni madisko na uasherati tu
 
Hivi huu Upuuzi wa kudanganya na kujidanganya Mtaacha lini? Hakuna Mwafrika aliyeleta Uhuru Afrika, Nchi zote za Afrika zilipewa Uhuru na watawala wao kwa sababu muda wa kupewa Uhuru ulikuwa Umefika, hivyo umefika wakati sasa tuache kudanganya, Acheni Propaganda za Uongo!

Mshukuru mungu angalau kwa kujua kusoma, kuandika na kuijua jf.
Akili yako ni ya kuvaa nguo tu, harakati za ukombozi zina simulizi nyingi za za kimaandiko na za mdomo kuhusiana na watu waliopoteza maisha kwa bunduki kwa ajili ya Afrika, wewe umejifunzia wapi kusoma?
 
Umekuja uza chai huku tena?Vipi Escrow umechemsha......ngoja tupitie na hii.....ungekuwa Mbita si ungempindua Nyerere....na ungekuwa umedai Ubaba wa taifa kabisa?


zitto atakufanya upate ugonjwa wa moyo...ambacho hakutaka ni kuongozwa na akili ndogo (mr dj) ambaye aligonga zero form 6, usichokielewa hapo nn?!
hata hivyo sikushangai kwa akili zile za kumfungulia lema thread ya kumpamba siwezi kutarajia zaidi kutoka kwako...ndege wafananao huruka pamoja!
 
kama hujui historia ni bora ukae kimya, kuliko kuandika usicho kijua, vita vya wahehe na wajerumani havikuwa vya mara moja kama unavyoudanganya umma, ilichukua miaka minne mpaka mkwawa kujipiga risasi, haikuwa rahisi hivyo kijana


Uongo na Upotoshwaji mwingine huu, Mkwawa (Apumzike Kwa Amani!) Risasi na Bunduki alivipata wapi kwenye hiyo miaka ya 1890? Na nani hata alimfundisha kuvitumia? Wakati vita hapo zamani tulikuwa tunatumia silaha za jadi kama Mawe,Upinde, Mishale, Mapanga n.k!
 
Mshukuru mungu angalau kwa kujua kusoma, kuandika na kuijua jf.
Akili yako ni ya kuvaa nguo tu, harakati za ukombozi zina simulizi nyingi za za kimaandiko na za mdomo kuhusiana na watu waliopoteza maisha kwa bunduki kwa ajili ya Afrika, wewe umejifunzia wapi kusoma?

Kuna Watu wetu wengi sana waliopoteza Maisha na ,,Wapuumzike kwa Amani" lakini bado haibadilishi UKWELI kwamba Wakoloni hawakuondoka Afrika kwa sababu eti tuliwafukuza, HAPANA, bali waliondoka kwa sababu waliamua kuondoka na muda wa wao kufanya hivyo ulikuwa umewadia, kama yalivyo mambo mengine hapa Duniani kila jambo lina wakati wake kama ilivyokuwa Utumwa haukusitishwa kwa sababu Waafrika tuligoma kuuzwa au kuuza watu wetu bali uliisha kwa kwa sababu Mashine ziligunduliwa ambazo ziliweza kufanya kazi kwa ufanisi na kwa haraka kuliko Watumwa hivyo Watumwa hawakuhitajika tena na hivyo Biashara hiyo kusimamishwa vivyo hivyo Ukoloni ulisitishwa kwa sababu muda ulikuwa umefika na haukuleta faida tena kwa Wazungu ila hasara na ndio maana wakatoa Uhuru na kuanzishwa Ukloni mamboleo ambao unaendelea mpaka leo hii!
 
Faiza hujielewi kabisa! Dini imekupofusha kabisa. Unadhani unaongea mambo ya maana sana kumbe upuuzi tu! dini dini dini, what a F. Be critical! Amini usiamini, watu wengi hapa hatufikirii in terms of dini km unavyodhani na dini kwa wengine is not a cup of tea! ndio maana Pengo akichemsha tunamshukia km mwewe bila kujali ni wa dini gani! Achan na haya mambo utakuwa mrembo!

Kama wewe unaogopa sana Uislam unapotajwa usinisome.

Labda haujuwi ni nini maana ya "dini".

Wasiofikiria mambo ya dini hata ku comment hawa comment, sema yamekugusa patamu tu.
 
Kuna Watu wetu wengi sana waliopoteza Maisha na ,,Wapuumzike kwa Amani" lakini bado haibadilishi UKWELI kwamba Wakoloni hawakuondoka Afrika kwa sababu eti tuliwafukuza, HAPANA, bali waliondoka kwa sababu waliamua kuondoka na muda wa wao kufanya hivyo ulikuwa umewadia, kama yalivyo mambo mengine hapa Duniani kila jambo lina wakati wake kama ilivyokuwa Utumwa haukusitishwa kwa sababu Waafrika tuligoma kuuzwa au kuuza watu wetu bali uliisha kwa kwa sababu Mashine ziligunduliwa ambazo ziliweza kufanya kazi kwa ufanisi na kwa haraka kuliko Watumwa hivyo Watumwa hawakuhitajika tena na hivyo Biashara hiyo kusimamishwa vivyo hivyo Ukoloni ulisitishwa kwa sababu muda ulikuwa umefika na haukuleta faida tena kwa Wazungu ila hasara na ndio maana wakatoa Uhuru na kuanzishwa Ukloni mamboleo ambao unaendelea mpaka leo hii!

Huo utumwa "umesitishwa" jina jina tu, mpaka leo upo na umeshamiri. Na bado ni tatizo duniani.

Na sisi Tanzania hatupo nyuma kwenye hilo. Hapahapa JF tumesoma watu wanaovyokwenda kuuzwa na Watanzania wenzao nje ya Tanzania.
 
Watu kama hawa hawaongelewi mpaka wamekufa kwa Uislam wao tu.

Na baada ya miaka miwili mitatu kupita akitokea Muislam kuandika habari zao ataambiwa mdini.

Wala siyo siri, Alama mohamed Sais amendika historia ya wazee wake walivyokuwa mstari wa mbele katika harakati za kupigania uhuru, wajinga wachache humuhumu JF wanamuita mdini.

Akitokea FaizaFoxy kuuliza iweje mnamuita mdini? na yeye ndiyo huwa si mdini tu bali ni jinni pia.
Faiza, huyu mzee ulimwona msikitini mara ya mwisho mwaka gani?
 
Faiza, huyu mzee ulimwona msikitini mara ya mwisho mwaka gani?

Sijawahi kumuona kwa sababu mimi ni mara mojamoja sana kwenda msikitini, tena nikienda huwa sitazami nani kaja nani hajaja, hatuchanganyiki na mimi hufata ibada na darsa na si kutazama waliohudhiria.

Kumbuka kuwa msikitini hakuna fashion show kama zile za makanisani.
 
Back
Top Bottom