Handeni: Dereva wa Bodaboda agonga bundi na kufariki

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
9,332
30,681
Afisa mifugo wilayani Handeni mkoani Tanga (Jina lake bado halijafahamika) amefariki dunia baada ya kumgonga ndege aina ya Bundi na pikipiki aliyokuwa akiendesha yenye namba za usajili STM 0232 . Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Ijumaa, Mei 17 2024 eneo la Sindeni, Handeni jirani na kona ya PRS 2.

Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamesema baada ya dereva huyo kumgonga bundi pikipiki yake ilipoteza mwelekeo na kuanguka na dereva huyo kupasuka kichwa. Na bundi huyo baada ya kugongwa alikufa papo hapo.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Albert Msando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa haamini kama ajali hiyo imetokana na imani za kishirikina.

#CloudsDigitalUpdates
 
Bundi wa mchongo huyo
20240517_181855.jpg
 
Screenshot_20240517-185216~2.jpg
Afisa mifugo wilayani Handeni mkoani Tanga (Jina lake bado halijafahamika) amefariki dunia baada ya kumgonga ndege aina ya Bundi na pikipiki aliyokuwa akiendesha yenye namba za usajili STM 0232 . Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Ijumaa, Mei 17 2024 eneo la Sindeni, Handeni jirani na kona ya PRS 2.

Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamesema baada ya dereva huyo kumgonga bundi pikipiki yake ilipoteza mwelekeo na kuanguka na dereva huyo kupasuka kichwa. Na bundi huyo baada ya kugongwa alikufa papo hapo.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Albert Msando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa haamini kama ajali hiyo imetokana na imani za kishirikina.
========
KARIBUNI HANDENI MJIPATIE MASHAMBA YA BEI CHEE!

#CloudsDigital
 
Back
Top Bottom