BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 425
- 1,071
Kama tunavyojua kwenye maeneo ya mikusanyiko kumekuwepo na kawaida ya kuzalishwa taka, hali ambayo inasababisha wasimamizi wa maeneo kuweka utaratibu wa kukusanya taka hizo ili zisilete athari za kiafya kwa wananchi.
Nasikitishwa sana na hali inayoendelea Kariakoo sehemu ambayo ni mlango wa Jiji hata Nchi kwa jumla hususani kwenye sekta ya biashara ili linadhibitishwa na ripoti za Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu mapato yanayokusanywa.
Lakini kibaya zaidi mkandarasi na Jiji wameshindwa kuweka maeneo rafiki ya kurundika taka zinazozalishwa hususani taka zinazotokana na vyakula.
Kumekuwepo na utaratibu wa wafanyabiasha hususani Mama ntilie ikifika jioni wanachukua uchafu na kuulundika kwenye maeneo ambayo mkandarasi ameyahalalisha kama maeneo rasmi ambapo asubuhi magari ufika kuchukua uchafu huo.
Utaratibu huu unaratibiwa kwenye maeneo yasiyo rafiki ni maeneo ambayo kuna shughuli za kibiashara na tumekuwa tukikumbana na kero maana kuna wakati uchafu huo unaweza kukaa siku hata mbili bila kuzolewa au wakati mwingine watu wanamwaga taka mapema saa 10 muda ambao bado shughuli za kijamii zinaendelea kwenye maeneo hayo.
Hali hii ni kero kubwa kwetu hasa mvua ikinyesha uchafu huo unatoa harufu mbaya huku nzi na wadudu wengine vyote vinakuwa sehemu hizo huku uchafu unaendelea kuzagaa kiholela kwa sababu unarundikwa tu sehemu ya wazi, hali ambayo inaweza kupelekea magonjwa ya mlipuko.
Nasikitika kwa kuwa kila wakati uliowekwa kiutaratibu Watu Kajenjere wanafika kuzoa taka lakini wao hawatupi huduma bora, kama hali itaendelea hivi itafika wakati nasisi tutakuwa wagumu kutoa pesa ya taka maana kuna wakati mteja anataka kuja dukani kwako anaona eneo hilo limezungukwa na uchafu.
Kama Mkandarasi au Jiji wanashindwa kusimamia suala hili mfano kuweka miundombinu rafiki ya wananchi kumwaga taka na kuziondoa kwa wakati bila kupelekea kero kwa wananchi basi hawana kudi kuwajibika kama sio kuwajibishwa maana Kariakoo ni sehemu kwa maendeleo ya Taifa yetu inatakiwa kuwa na mazingira rafiki yanayovutia watu sio kukimbiza watu.