Hali si hali: Magufuli ana uungwaji mkono kiasi gani ndani ya chama?

..wasiwasi wangu ni kwamba vijana wanaweza kuamini kwamba KUDUKUA mawasiliano ya MPINZANI wako ni mbinu HALALI ya kisiasa.

..Kwa uelewa wangu kashfa ya Watergate iliyosababisha Raisi Richard Nixon auteme wadhifa wake ilihusu makosa ya udukuaji yaliyofanywa na timu yake ya kampeni.

..Sijui sheria zetu za udukuaji mawasiliano zinasemaje.

Cc Nyani Ngabu, Kiranga
Magufuli kashasema hadharani kwamba anawadukua watu bila ridhaa zao.
 
Hahahaaaa, watu Nchi walimpa wao wenyewe, kelele za nini sasa?.Chezea paka wewe, chakula unampa wewe mwenyewe na ukileta za kuleta anakupalua.
 
Yawezekana labda ni mimi tu. Labda ni hisia zangu tu. Labda ni jakamoyo langu tu.

Natamani akili yangu iwe inanihadaa [my mind playing tricks on me...shout out to the Geto Boys. RIP Bushwick Bill].

Kinachoendelea sasa hivi nchini kimeanza kunipa wasiwasi.

Huyu mtu aitwaye Musiba naona kaibua mengi. Au labda niseme kasababisha yaibuke mambo ambayo yananipa hofu.

Yote yaliyotokea kabla ya hii kanda ya sauti inayodaiwa kuwa ni ya Nape Nnauye na Abdul Kinana, nilikuwa napuuzia tu. Kusema ukweli zile sauti zinafanana sana na sauti zao.

Wawili hao wanadaiwa kumteta Rais Magufuli.

Hii kanda imenifanya nijiulize mengi sana.

Najiuliza Magufuli anaungwa mkono kiasi gani na viongozi wa juu wa chama chake, wastaafu na waliopo madarakani.

Kama haungwi mkono na wengi, je, hii serikali yake ni dhoofu kiasi gani?

Manake sioni ni kivipi anaweza kuongoza na kufanya kazi kwa ufanisi kama atakuwa anapingwa kwa kiasi kikubwa na walio wengi kwenye uongozi wa chama chake.

Isije kuwa tuna raisi ambaye katengwa wenzake!

Mkuu Nyani Ngabu kwanza nikupongeze kwa kuanza kuuona mwanga... Hujachelewa sana ila umechelewa..
Mwenzio nilianza kushtuka mara baada ya kukutana na msafara wa JPM punde tu baada ya kutawaza kuwa raisi wa nchi hii. Ule ulinzi haukuwa wakaida.. Na tangu siku ile naamini kuwa Ikulu si mahali salama sana kwa JPM..
Anyway; nchi lazima itanukeeeee... itanuke weeee ili mwisho wa siku raia wapate uhuru na demokrasia kamili!
Price must be paid!
 
As long as CCM ndiyo imeshika jiko ni vigumu kuisambaratisha. Ingekuwa hivyo ba Lowassa angeimaliza kwani alikuwa na uungwaji mkono wa wajumbe wengi.

Alikuwa anaungwa mkono au alikuwa analiwa hela zake? Ccm kama chama sio imara, bali madaraka ya rais ndio yanayoipa uhai ccm. Ccm ikipoteza utii wa vyombo vya dola haiwezi kusimama tena kama chama cha siasa kwani inategemea mbeleko ya dola tu.
 
Kinana na Nape wakae kimya maana hili linaenda pabaya. Nimemsoma Albert Msando nakuona direction ya hili ....

..mbona sioni kosa lao.

..wana ccm wanapingana ktk nafasi mbalimbali ndani na nje ya chama, kwa mfano udiwani, na ubunge.

..kuna tatizo gani wakipingana ktk uraisi?

..mimi nadhani mwenye matatizo ni yule aliyekwenda kuwadukua.

..aliyepaswa kudukua ni vyombo vya usalama, tena kwa sababu mahususi.
 
Mimi sijawaelewa. Mmeshangazwa na nini kwenye hayo mazungumzo? Mbona ni mambo ya kawaida kabisa. Just men's talk. You guys need to grow up. Kwanza kwa nini mnaingilia mawasiliano binafsi ya watu? hiyo ni violation ya privacy.
 
Mkuu Nyani Ngabu kwanza nikupongeze kwa kuanza kuuona mwanga... Hujachelewa sana ila umechelewa..
Mwenzio nilianza kushtuka mara baada ya kukutana na msafara wa JPM punde tu baada ya kutawaza kuwa raisi wa nchi hii. Ule ulinzi haukuwa wakaida.. Na tangu siku ile naamini kuwa Ikulu si mahali salama sana kwa JPM..
Anyway; nchi lazima itanukeeeee... itanuke weeee ili mwisho wa siku raia wapate uhuru na demokrasia kamili!
Price must be paid!

I’ve been woke ever since I became me.

Woke is deeply embedded in my DNA.

Perhaps you don’t see that because I’m not down with the herd mentality.

I just don’t go along to get along.
 
Magufuli anaungwa mkono na na wananchi wa kawaida . Tatizo watanzania tuna extremely short memory inaeleweka waliasisi na kuishi na kunufaika kwenye mifumo aliyoibomoa Magu hawezi kumuunga mkono japo wanamuogopa kama ukoma ndo maana kurelease statement yao imekuwa kama kujiwasha moto

Mtu anayeongoza kwa hofu na kuchezea box la kura utawezaje kumpima kukubalika kwake? Ni wapi wananchi wako huru kuonyesha kweli wanamkubali zaidi ya kulishwa maneno? Ni mnyonge gani kafaidika na Magufuli kwamba akitoka madarakani huyo mnyonge atateseka? Hilo neno la kwamba Magufuli anakubalika yanatoka kwenye genge linafaidika na madaraka yake, na hakuna sehemu ya kusemea kwamba hakubaliki.
 
👿👿👿👿👿👿👿SASA YAMETIMIA:eek::eek::eek:☠☠☠
SASA TUONE KAMA ZILE TAMBO ZA JIWE KUWA ANGEWAPOTEZA NUSU YA WAJUMBE WA NEC. KAMA ALIKUWA ANAMZODOA JK TU AU ALIKUWA NA HUO UBAVU WA KUFANYA KWELI.

JIWE ANAUMBUKA NA TAMBO ZAKE. KAGUSA PASIPOGUSIKA.

CCM INA WENYEWE.

Wapi Jiwe ameumbuka....!!?
punguza ushadadizi...
nadhani walioumbuka ni hao alleged persons kwenye clip....
 
..wasiwasi wangu ni kwamba vijana wanaweza kuamini kwamba KUDUKUA mawasiliano ya MPINZANI wako ni mbinu HALALI ya kisiasa.

..Kwa uelewa wangu kashfa ya Watergate iliyosababisha Raisi Richard Nixon auteme wadhifa wake ilihusu makosa ya udukuaji yaliyofanywa na timu yake ya kampeni.

..Sijui sheria zetu za udukuaji mawasiliano zinasemaje.

Cc Nyani Ngabu, Kiranga

Kwa katiba hii mbovu chochote anachofanya rais inaonekana yuko sawa, na kundi linalotokea kubariki huo ushenzi ni kundi lile lile linalofaidika na madaraka ya rais. Wacha rais achezee madaraka apendavyo, lakini hata yeye atakapotoka atajikuta kwenye wakati mgumu. Kwani hata hao anaowasulubu sasa, walipokuwa wanafanya uhuni waliona ni sawa na kubatizwa kuwa ni mbinu za kisiasa
 
Mimi sijawaelewa. Mmeshangazwa na nini kwenye hayo mazungumzo? Mbona ni mambo ya kawaida kabisa. Just men's talk. You guys need to grow up. Kwanza kwa nini mnaingilia mawasiliano binafsi ya watu? hiyo ni violation ya privacy.

Hata mimi ninaona ni mazungumzo ya kawaida sana, maana kwa watu waliotoil kuinadi ccm na baadaye wanaambulia matusi ya Musiba, nilitegemea mazungumzo yao yangekuwa na maneno makali zaidi ya haya.
Kwa ninachokiona Mkulu inabadi atumie busara sana katika kudeal na suala hili na endapo atakurupuka basi matokeo yake hataamini macho na masikio yake stay tuned!
 
Kwa katiba hii mbovu chochote anachofanya rais inaonekana yuko sawa, na kundi linalotokea kubariki huo ushenzi ni kundi lile lile linafaidika madaraka ya rais. Wacha rais achezee madaraka apendavyo, lakini hata yeye atakapotoka atajikuta kwenye wakati mgumu. Kwani hata hao anaowasulubu sasa, walipokuwa wanafanya uhuni waliona ni sawa na kubatizwa kuwa ni mbinu za kisiasa

..tatizo anaweza kufanya mambo ya kikatili mpaka yeye mwenyewe na watu wake wakaogopa kuondoka madarakani.

..ndiyo yaliyotokea Zimbabwe. Mugabe alianza kwa matumaini makubwa, ila akazidisha ukandamizaji kiasi kwamba akahisi kuondoka madarakani siyo salama.

..au yaliyotokea ZANZIBAR. hofu ni kwamba chama kingine kikishika madaraka watakwenda kufukua records za attrocities zilizotokea miaka iliyopita.
 
Wapi Jiwe ameumbuka....!!?
punguza ushadadizi...
nadhani walioumbuka ni hao alleged persons kwenye clip....
Tunasubiria zile tambo zake kuwa yeye ni jiwe na angewapoteza nusu ya wajumbe kwa kuimba wana imani na mtu fulani. Lazima aumbuke. Tunamsubiri ajisogeze kwenye kona tupige nyundo kichwani. MEMBE FOR PRESIDENT.
 
Back
Top Bottom