HAITI "Mountain Country"

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
IJUE HAITI (nchi ya milima) NCHI YA KWANZA DUNIANI AMBAKO WATUMWA WENYE ASILI YA AFRIKA WALIFAULU KUPINDUA UTUMWA NA KUJIPATIA UHURU TAREHE 1 JANUARI 1804.

Na.Comred Mbwana Allyamtu.
Thursday-09/11/2017

Haiti iko katika kisiwa chenye joto cha Hispaniola, ambacho kina milima mirefu zaidi katika eneo la Karibea. Milima hiyo ina urefu wa zaidi ya meta 2,400. Vidimbwi vidogo vilivyo katika maeneo yaliyoinuka vinakuwa na ukungu na barafu wakati wa miezi ya “baridi.”

Maeneo yenye milima na mabonde kusini mwa Haiti yamefunikwa na misitu mikubwa sana. Maeneo mengine yenye milima hayana misitu, kwa sababu imeharibiwa. Ukienda kaskazini au kusini, utagundua kwamba Haiti ni nchi maridadi sana. Ukipita katika vijia fulani vyenye kupinda-pinda milimani, utaona maeneo mbalimbali yenye kuvutia sana ya nchi kavu na bahari. Kila mahali unaweza kuona maua mbalimbali yenye rangi za kuvutia.

hii ndio Haiti nchi nilio itembelea mwaka 2015, nilijifunza umaridadi wake na vivutio lukuki vyenye kufunza na kuburudisha. Watu wake ni wacheshi mno... Wenye ukarimu na upendo wakati wote, ukweli nilijihisi nipo nyumbani Tanzania wakati wote nilipo kuwa nchini humo.

Nchi hii ya Haiti ni maridadi kweli ina watu milioni 8.3, na wengi wao wana asili ya Kiafrika na wanaishi mashambani. Wengi wao ni maskini, lakini ni wenye fadhila na wakarimu Haiti ni nchi ya kwanza duniani ambako watumwa wenye asili ya Afrika walifaulu kupindua utumwa na kujipatia uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1804.

Jina la "Haiti" lina asili katika lugha ya Kitaino ambayo ndio lugha ya wakazi asilia, linamaanisha "nchi ya milima", na kweli kisiwa kina milima mingi. Hata hivyo Haiti ni kati ya nchi maskini kabisa duniani na nchi maskini zaidi katika bara la Amerika yote. Kijeographia Nchi hii ina wilaya kumi.

Wakazi ni milioni 8.3 (Lakin Inatajwa kufika million 10 sasa kwa takwimu ya sasa yani mwaka huu 2017), lakini wananchi wengine wengi wamehama kutokana na ufukara. Karibu 900,000 (laki tisa) wako Marekani, 800,000 (laki nane) wako Dominikana na 300,000 (laki tatu) wako Cuba, halafu wengine wapo Canada, Ufaransa na Bahamas hapa utaona namna gani kiwango kikubwa cha wakazi wake wako uhamishoni na hii ni kutokana na hali mbaya ya uchumi wa taifa hilo dogo.

Kuna lugha rasmi mbili moja ni Kifaransa na nyingine ni Kikreoli ya Haiti ("Kweyol") inayotokana nacho. Wakazi wengi ni wafuasi wa dini ya Kristo katika dhehebu la Kanisa Katoliki (kwa karibu 80%) lakini wengi hufuata vilevile dini ya vudu inayotokana na dini za jadi kutoka Afrika ya Magharibi. Waprotestanti ni 16% tu katika nchi hiyo.

SASA TUFAHAMU HISTORIA YA HAITI

Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak. Baada ya kufika kwa Christopher Columbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana na magonjwa ya Ulaya ambayo hawakuzoea na kukosa kinga dhidi yao na pia kutokana kutendewa vibaya kwa unyama na mabwana wapya wazungu wa ulaya. Mnamo mwaka 1600 Waindio wachache tu walibaki kutoka malakhi wakati wa Columbus wakapotea kabisa kwa njia ya kuoa au kuolewa na wazungu na weusi. Wahispania walianzisha mashamba kwa kuwatumikisha kazi watumwa kutoka Afrika.

Ukoloni wa Ufaransa

Katika karne ya 17 Wafaransa walifika kisiwani wakanunua theluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujenga uchumi wa mashamba makubwa hasa ya miwa. Koloni ya Saint-Domingue ilikuwa koloni tajiri ya Ufaransa katika Amerika huo.

Mapinduzi ya Ufaransa

Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa 1789 koloni ilikuwa na wakazi wa aina nne kwanza Wazungu hasa Wafaransa waliokuwa mabwana lakini waliokuwa na tofauti kubwa kati yao na wengine wao walikuwa ni matajiri sana huku wengine wakiwa ni maskini jumla ya hao mabwana wa kifaransa walikuwa ni takriban watu 32,000.

Pili ni machotara na weusi huru ambao walikuwa raia wa daraja ya pili wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa jumla yao ni watu 28,000 watumwa wa asili ya Kiafrika - jumla watu 500,000.

Wamaroni walikuwa watumwa wakimbizi walioishi mlimani katika pori idadi yao haijulikana hawakuwa wengi. Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwa haki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya machotara wenye mali ya kukubaliwa kama raia kamili wenye haki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.

TOUSSAINT L’OUVERTURE KIONGOZI WA UHURU WA HAITI.

Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada wa Uingereza na Hispania wakichukia mapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na weusi huru wenye elimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hawa bila sheria za Ufaransa utakuwa vibaya zaidi kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza harakati za mapinduzi.

Kiongozi wao alikuwa Toussaint L'Ouverture aliyefaulu kushika serikali ya koloni tangu 1798. Awali alipigania jeshi la Ufaransa baada ya bunge la Paris kutangaza mwisho wa utumwa alishirikianna na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye shamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.

Toussaint L'Ouverture alishinda pia Waingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa wa Paris na 1801 akateka kaskazini ya kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawala Hispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.

Lakini mmnamo mwaka 1802 siasa ya Paris ilibadilika na mtawala Napoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola kwa hali ya awali ya kuwa koloni la Ufaransa akatuma jeshi kubwa la askari 40,000.

L'Ouverture alikamatwa alipokubali kushauriana na jenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakini makamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia kuhusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianza vita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Jean-Jacques Dessalines alitangaza uhuru mwingine tena dhidi ya koloni tarehe 1 Januari 1804 kwa jina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi walio huru” toka hapo Haiti ikawa huru mpaka leo hii ndio Haiti ninayoijua...

Wako Mjoli wa Historia ya dunia na mambo ya diplomasia ya dunia......

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com.
IMG_20190510_205131_022.jpeg
 
Vipi kuhusu fursa za biashara nchini humo? Ni vitu gani tunaweza peleka then tukapiga pesa
 
Vipi kuhusu fursa za biashara nchini humo? Ni vitu gani tunaweza peleka then tukapiga pesa
Hakuna fursa ni umaskini tu nchi imeharibika vibaya kwa tetemeko na majanga mengine ya asili ikiwemo magonjwa kama Malaria,kipindupindu n.k..na pia nchi hii haipewi misaada yoyote kutoka nje yaani ni umaskini uliopitiliza "Absolute poverty" na raia wengi wa hapa ni wachawi sana kuna uchawi unaitwa VOODOO unauliwa dakika mbili tu..mtu anakuwa na kimdoli chake anakichoma sindano huku akitaja jina lako wewe huko ulipo unakufa fasta tu
 
Uchunguzi wako wa mwaka gani mkuu? Ikiwa hawapokei msaada na kilimo cha ni hafifu ina maana soko la chakula lipo kulisha wenye uwezo wa kati na juu

Nilipata kusikia watu wao ni wakarimu sana ikiwa nitakwenda kwa biznez zangu watanilogha kama sijamkosea mtu?

Natamani sana kuitembelea hii nchi uchawi wao siujali, mkuu una mdau yeyote mwenye trip za huko uniunge nae nimuulize maswali ya hapa na pale
 
Nimewahi kutembelea Haiti miaka ya zamani sana nikitokea British Virgin Islands nina experience ya maisha ya huko unapoambiwa ni maskini ni maskini kweli mara 5 ya hii Tanzania tunayoiita maskini..labda nikuulize bidhaa gani ambazo unadhani zinaweza kuuzika HAITI?!?..maana kwa uzoefu wangu Haiti asilimia 80 ya bidhaa zake ana import From USA,na asilimia chache CUBA
 
Ndio ni maskini na kula ni lazima mkuu, kwa utafiti juu juu kg 100 za mchele kule ni dola 250 ambao wana import USA na bado hautoshi
 
Ndio ni maskini na kula ni lazima mkuu, kwa
utafiti juu juu kg 100 za mchele kule ni dola 250 ambao wana import USA na bado
hautoshi
Ku export mchele kwenda katika nchi za America kama hizi kutokea Africa ni kazi ngumu kupita maelezo..kama unataka kufanya biashara hii ni bora ukawa na mtaji mkubwa sana ndio utafanikiwa kama hii ndio biashara yako kwanini mchele usiuze hata hapo Rwanda kuna soko zuri? Kuliko ku export kwenda Hayiti?..hapa unatakiwa kuwa na mtaji sio wa kitoto
 
Rwanda bei zao zikoje?
 
Rwanda bei zao zikoje?
nasikia gunia moja linafika hata shillingi 200000..i mean gunia la mpunga lenye debe saba wakati hapa Tanzania bei ya sasa ni 80000 kwa mbegu ndogo na 100000 kwa mbegu kubwa za super Shinyanga,Kyela na mbawa mbili..sijajua bei ya mchele watu wengi Rwanda wanapelekaga tu mpunga ambao haujakobolewa
 
Ooh unaweza ukawa una ukweli. Lile tetemeko walilopigwa kuna MTU aliwatuma kuwaonya watubu na nakumbuka aliwaambia dhambi yako ni uzinzi kwenye fukwe Zao na witchcraft.kwa maelezo yako nimejua kumbe ni kisiwa tena kina ma beach sio? Ule utabiri ulikua sahihi kabisa
Hakuna fursa ni umaskini tu nchi imeharibika vibaya kwa tetemeko na majanga mengine ya asili ikiwemo magonjwa kama Malaria,kipindupindu n.k..na pia nchi hii haipewi misaada yoyote kutoka nje yaani ni umaskini uliopitiliza "Absolute poverty" na raia wengi wa hapa ni wachawi sana kuna uchawi unaitwa VOODOO unauliwa dakika mbili tu..mtu anakuwa na kimdoli chake anakichoma sindano huku akitaja jina lako wewe huko ulipo unakufa fasta tu
 
Haiti ina laana kutoka kwa Mola. Umeona wanavyofurahia kula nyama ya watu ambao ni wapinzani wao. Ukitofautiana na magenge ya wahuni wakafanikiwa kukukamata unachomwa mzima mzima kama ndege wa porini then unaliwa nyama choma kama wale mbuzi wa pale Dakawa mnadani au wale Mbuzi wa Msalato pale Dodoma kila wikiendi.

Haiti is a fallen State.
 
Kama Wa-Haiti ni watu wakarimu na wenye upendo, nini kimewakumba hadi nchi kuendeshwa na magenge ya kihuni baada ya kumuua Rais wao??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom