TANZIA Gwiji wa Kiswahili, Mzee Amiri Soud Andanenga ametutoka

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,886
3,629
Msanii mkongwe na miongoni mwa washairi wakubwa nchini na Afrika Mashariki, Amir Sudi Andanenga amefariki dunia usiku wa Mei Mosi, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi nchini (UKUTA), marehemu Andanenga amekutwa na umauti akipatiwa matibabu katika hospitali ya Dkt. Mvungi, Kinondoni, Dar es Salaam.

Maziko ya Andanenga aliyefahamika zaidi kwa jina la sanaa ya ushairi la ‘Sauti ya Kiza’ yanatarajiwa kufanyika leo tarehe mosi, Mei 2024 wilayani Kinondoni Dar es Salaam.

andanenga.jpg

RIP Mzee wetu ANDANENGA
 
Huyu mzee kwa ugwiji wake
Hakutakiwi kuishi maisha aliyokuwa anaishi
ngoja tuanze kuwaona wanafki
wazee wa legacy na makala
Wanasemaje

Ova
 
Mzee baba hayo ndio yalikuwa maisha yake na yalipaswa kuwa hivyo alivyoishi sio unavyotaka au kufikiria wewe na wengineo. Tafsiri ya maisha ni nadharia pana kwa kila kiumbe chenye uhai. Yote kwa yote mashairi na tungo zake yataishi na kudumu.
 
Huyu mzee kwa ugwiji wake
Hakutakiwi kuishi maisha aliyokuwa anaishi
ngoja tuanze kuwaona wanafki
wazee wa legacy na makala
Wanasemaje

Ova
Magwiji huishi muda mfupi. Hata profesa Jize ilitakiwa awe amesepa kitambo. Jina lake lingevuma miaka mingi sana.......hapo vp ........hapo sawa
 
Sauti ya Kiza alivuma sana Radio Tanzania Dar es salaam na kwenye magazeti kipindi tunakua.

RIP.
Huyu mzee alikuwa anakaa kinondoni shamba,mwembe sindimba leo wanamzika makaburi ya kinondoni jirani na fm club
Ukiona mambo aliyofanya,utunzi wa vitabu nk hakutakiwa kuishi maisha aliyokuwa anaishi
Ngoja tuwaone sasa walevwanafki wa mambo ya historia kuelezea blah blah sjui kaachaa pengo,mara pengo lake alizibiki waje waanze kutema cheche

Nakumbuka.

Si unajua tena hatumthamini mtu mpaka afe kwanza.
 
Innalillaahi wa inna ilayhi raaji'uun....mola ampumzishe mahala pema peponi nguli wa ushairi
 
Msanii mkongwe na miongoni mwa washairi wakubwa nchini na Afrika Mashariki, Amir Sudi Andanenga amefariki dunia usiku wa Mei Mosi, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi nchini (UKUTA), marehemu Andanenga amekutwa na umauti akipatiwa matibabu katika hospitali ya Dkt. Mvungi, Kinondoni, Dar es Salaam.

Maziko ya Andanenga aliyefahamika zaidi kwa jina la sanaa ya ushairi la ‘Sauti ya Kiza’ yanatarajiwa kufanyika leo tarehe mosi, Mei 2024 wilayani Kinondoni Dar es Salaam.

RIP Mzee wetu ANDANENGA
Sikuwa nikimfahamu ila mimi kama mdau wa Kiswahili sanifu namtakia mapumziko mema ya milele.
 
Rip Undernenga, huyu Mzee na Shabani Kadaru walikuwa noma sana. Naomba mwenye mashairi yake au naweza PATA wapi ghani zake za ushauri?
 
Huyu mzee alikuwa anakaa kinondoni shamba,mwembe sindimba leo wanamzika makaburi ya kinondoni jirani na fm club
Ukiona mambo aliyofanya,utunzi wa vitabu nk hakutakiwa kuishi maisha aliyokuwa anaishi
Ngoja tuwaone sasa walevwanafki wa mambo ya historia kuelezea blah blah sjui kaachaa pengo,mara pengo lake alizibiki waje waanze kutema cheche

Ova
Mimi siku hizi Unafiki sitaki.....nakupa sifa Yako ukiwa hai nawe nipatie yangu nikiwa hai.....ohhh marehemu alikuwa hivi mara vile kimeshuka kikapanda
 
Back
Top Bottom