Google Advertising (Google Ads)

Cainan

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
440
491
Habarini wakuu,
Ukiacha advertising platform kama facebook , instagram na twitter nani yupo familiar na google ads namaanisha vitu kama gharama, namna ya kudeliver na vitu vingine muhimu

Maana kwenye biashara ni kitu muhimu sana kuongeza wigo au coverage,
 
Unataka kutangaza biashara kwa kutumia google ads, ni kama sijaelewa swali
 
Njia ya search unapata wateja wenye uhitaji kabisa wa bidhaa ama huduma unayouza

Google wanatumia keywords(maneno watu wanayotafuta) halafu tangazo lako linaonekana
Unaweza tengeneza tangazo kwenye hii link google ads Google Ads ‒ Mit Onlinewerbung Kund*innen gewinnen und mehr Umsatz erzielen

Ila kabla ya kuweka tangaza ni bora ukajua keywords wateja unaowalenga hutumia wakati wakitafuta taarifa zinazoendana na kitu unachotaka kuuza, na pia ujue idadi ya watu wanao-type hiyo keyword kwa mwezi, na metrics zingine
Ili ujue hizo keyword tumia Google keyword planner itakupa mapendekezo ya keywords mbalimbali zinahosiana na bidhaa yako, Google Ads - Sign in

Mteja anayetafuta kitu kwenye google ana chansi kubwa ya kununua bidhaa maana anafahamu kuwa ana uhitaji wa kitu fulani tofauti na mteja anayekutana na tangazo ghafra akiwa anaperuzi picha na video instagram
 
Back
Top Bottom