Gharama za mobile banking zinatisha, ni ujambazi kwelikweli

Rolla Patrick

Member
Aug 24, 2021
31
110
Dah sijui tunaelekea wapi, hizi huduma zilipaswa kutupa unafuu wananchi kufanya miamala bila usumbufu lakini imekua ujambazi hasa hasa.

Niliwahi kuhamisha laki mbili kutoka Benki kwenda mpesa nikakatwa 11,000/= hapo bado sijakutana na Makato ya mpesa, nikajikuta nakatwa karibu 16000/= kupata 194,000 sijui, nikabaki nimeduwa.

Ukitoa hata 40000 wanakata 6000/= Makato ya mpesa/tgopesa/Airtel money utakutana nayo juu kwa juu.

Jana nimenunua vocha ya 2000 kutoka mobile banking naangalia statement wamekataa 700/= anyway sawa tu IPO siku kitaeleweka tu maana washatuona misukule.

Nimefuta app zao zote ila najua hata kwenye atm ni yaleyale.
 
Simbanking niliachaga kutumia miaka mingi sana asee.
Bora niende ATM ya bank nyingine.
Atm ya bank nyingine ndio balaa yale yale.bora uende atm ya bank yako.nilitoa 1,200,000 bank nyingine wakanikata 12,000 tsh.
 
Si MNASEMA MAMA ANAUPIGA MWINGI MBAKA UNAMWAGIKA NYIE MLIKUA MNALISHWA MATANGO POLI NA MKALA SASA HAMUISHI KUYAMBAYAMBA KARIBUNI DUBAI
 
Lkn sikuhizi wameadvance ukitoa kwa kupitia app unauwezo wa kwenda kuichukulia kwenye atm na makato ni yale yale kama ungetoa kwenye atm card
Yaani nitumie app lets say ya NBC nikatote kwa wakala wa Airtelmoney hizi ni transactions mbili Bank ale na Mpesa ale haiwezi kuwa sawa
 
Back
Top Bottom