Fursa ya kupata Vitalu vya Kufugia katika Ranchi za Taifa

Mfugaji123

Member
Apr 3, 2020
10
19
FURSA: Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ( NARCO LTD) ni Kampuni ya Serikali inayofanya ufugajina uuzaji wa Ng’ombe wa nyama, uchinjaji, uchakataji pamoja na uuzaji wa nyama ( Kongwa beef). Mwaka 2002 Serikali iliamua kuwa baadhi ya maeneo ya Ranchi yakodishwe kwa wananchi wenye nia na uwezo wa kuwekeza katika ufugaji wa kisasa na kibiashara. Hivyo, kutokana na maamuzi hayo, NARCO inaendelea kupangisha vitalu katika baadhi ya maeneo ya Ranchi zake kwa wafugaji wazawa kwa mikataba ya muda mfupi na mrefu

Mkurugenzi Mtendaji wa NARCO LTD anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye nia na uwezo wa kupanga katika vitalu vyake kwa lengo la kuinua tija kwa njia ya ufugaji wa kisasa na kibiashara. Taarifa kamili tembelea tovuti ya NARCO
Au Kwa msaada wa kuwasilisha maombi na kuandikiwa business plan usisite kuwasiliana nasi : 0621106923
 

Attachments

  • images (43).jpeg
    images (43).jpeg
    54.1 KB · Views: 4
Naona Sasa Narco Wanaanza Kupata Akili.Its a Good Move.Hivi Hectare Moja ni Sawa 10,000 Sqm ama?
 
Back
Top Bottom