Full Time: AFL: Al Ahly 0-0 Mamelodi Sundowns (Agg 0-1) | Cairo International Stadium | 01.11.2023 |

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,493
105,614
Baada ya 1st leg kumalizika kwa Mamelody kuibuka na ushindi wa bao 1-0 leo ni mchezo wa pili wa marudiano.

Mechi inayarajiwa kuwa ngumu kwa dakika zote.

Muda wa mechi ni 21:00

Al.jpeg

Kikosi cha Al Ahly
Mamelodi.jpeg

Kikosi cha Mamelodi
Mchezo una kasi, Al Ahly wanapambana kutafuta goli la kusawazisha kwa kuwa katika mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0.

Kumbuka mshindi wa hapa ataenda fainali kukipiga dhidi ya Wydad AC ambayo imefika hatua hiyo kwa kuiondoa Espérance de Tunis ya Tunisia kwa penati 5-4, baada ya matokeo ya jumla kuwa 1-1.

Kipa wa Mamelodi, Ronwen Williams anapangua penati ya Ali Maâloul

Mamelodi Sundowns FC wanashambuliwa lakini nao wanajibu mapigo kwa kufika langoni kwa wapinzani wao mara kadhaa.

Mpira unaopigwa hapa ni mwingi kwa timu zote mbili, kama wewe ni shabiki wa soka hautakiwi kukosa mchezo huu.

Hadi dakika ya 30, Al Ahly ndio wanaofanya mashambulizi mengi na makali huku wakiungwa mkono na mashabiki wao wanaoshangilia kwa nguvu.

Mapumziko: Matokeo ni 0-0

Kipindi cha pili kimeanza

Mambo bado ni magumu kwa timu zote hasa wenyeji Al Ahly ambao wanaonekana kuwa na presha kubwa kwa kuwa wapo nyuma kwa matokeo ya jumla.

Dakika ya 62, hakuna mbabe hapo wenyeji wanaendelea kutoa presha kwa wapinzani wao.

Dakika ya 67' Mamelodi wanalalamika mchezaji wao kuchezewa faulo ndani ya boksi lakini refa anasema "hakuna kitu kama hicho".

Dakika ya 83' Mendieta wa Mamelodi anapata kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kucheza faulo.

Zinaongezwa dakika 7 lakini haziisaidii Al Ahly, mwamuzi anamaliza mchezo na Mamelodi inaingia fainali.
 
Baada ya 1st leg kumalizika kwa Memelody kuibuka na ushindi wa bao 1-0 leo ni mchezo wa pili wa marudiano.

Mechi inayarajiwa kuwa ngumu kwa dakika zote.

Muda wa mechi ni 21:00
Mkuu nategemea kupata up date kutoka hapa mazee.
Hivyo jitahidi kila tukio muhimu uwe unatujulisha, leo niko mbali na tv, alafu hii game ni muhimu sana.
Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom