Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe: Uchaguzi Mkuu wa 2020 CHADEMA hatukuwa na wagombea sahihi

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.

Mbowe amesema Chadema haijawahi kuishiwa ajenda za kupambana na CCM.

My take.

Watakiri yote waliyomsingizia mwendazake laana ya kumtukana imeanza kuwatafuna.

Kumbe waliweka wagombea dhaifu alafu wakasingizia wameibiwa kura na mwendazake. Hovyo kabisa.

=====

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Pia, amesema kwa sasa falsafa zake za kisiasa zinakwenda sawa na zile za aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Thomas "Tip" O'Neil Jr.

Amesema O'Neil kupitia kitabu chake cha 'All Politics is Local' amesema siri za ushindi za chama cha siasa ambazo ndizo anazutimia kuongoza mapambano ya kushika dola nchini.

Amezitaja falsafa hizo kuwa ni chama kupata mgombea sahihi na nayekubalika kwa wapiga kura.

"Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani," amesema Mbowe.

Ametaja jambo la pili kuwa ni chama kuwa na ajenda ya kuwashawishi wanachi kukichagua, ambapo kwa upande wa CHADEMA, Mbowe amesema hakijawahi kukosa ajenda ya kushindana na Chama tawala-CCM.

"Ilani yetu ya uchaguzi ilikuwa bora kwa sababu imefanyiwa utafiti," amesema.

Mambo mengine ambayo Mbowe ameyataja ni kuwa na uongozi imara na rasilimali fedha ambapo kwa sasa chama kinatengeneza miundombinu rafiki ikiwemo kuwekeza kwa vijana na kukuza teknolojia kutoka analojia kwenda dijitali.

"Sasa hivi wanachama wa CHADEMA ni ambao hawazidi umri wa miaka 45 hii ni dalili nzuri kwamba, upinzani utakuwa imara zaidi lakin pia tunapambana kuhakikisha kila kitu tunachokifanya kinafanyika kidijitali," amesema Mbowe.

Kiongozi huyo amesema kikao cha Kamati ya Utendaji ya CHADEMA Kanda ya Victoria kimeafiki kuwa kila Jumamosi kuwa siku ya kuvaa sare ya Chama hicho kwa wanachama wake.

"Tunatambua kuwa wana CHADEMA walikuwa wameshaanza kusahau hadi kuvaa sare, lakini sasa wanachama wa CHADEMA watavaa sare kila Jumamosi ili kuongeza motisha na idadi ya wafuasi wetu," amesisitiza.

Chanzo: Mwananchi
 
Chadema imewashika watu pabaya kweli yaani, na mtanyooka yaani Hilo nduo dude linaitwa Chadema, mkilisikia tu mnatafuta pa kujificha yaan🤣🤣🤣
 
Mbowe hawezi ongea ujinga wako wa kutunga
Laana ya Magufuli imeanza kuwatafuna, ukweli haujifichi daima ndiyo mpaka leo Lema na Lisu wanaendelea kulelewa Ulaya na hawana dalili za kuacha kulelewa licha ya kwamba Magufuli hayupo tena hapa duniani.
 
Kampiga dongo Lisu kiaina,ila itafahamika tu kama kweli Lisu alikua dhaifu ama ni futna za Mbowe kwa Lisu.
 
Nilishasema kuna bifu Kati Lisu na mwenyekiti wake haya sasa wale wapambe nuksi njoeni tena.
Utabiri wangu Mbowe atadondoshwa na Lisu maana Ile mashine sio mchezo.
Kweli kabisa
 
Kama Ndo hivyo alivyoongea Mbowe itakuwa ana matatizo makubwa nahisi sababu ya matatizo Yake ni Chanjo ya Corona aliyopata AstraZeneca
Kumbe kaanzisha campeni ya kuwasameeh wanasiasi waliokiacha chama heti warudi Chadem waje kajenga chama , anatafuta wagombea sahihi wanye ushawishi
 
Kama Ndo hivyo alivyoongea Mbowe itakuwa ana matatizo makubwa nahisi sababu ya matatizo Yake ni Chanjo ya Corona aliyopata AstraZeneca
Kumbe kaanzisha campeni ya kuwasameeh wanasiasi waliokiacha chama heti warudi Chadem waje kajenga chama , anatafuta wagombea sahihi wanye ushawishi
Ukweli huwa haujifichi
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi...
Pole, naona dhambi ya mwenda zake haijawaisha kichwani. na bado tutawaoa
 
Nilishasema kuna bifu Kati Lisu na mwenyekiti wake haya sasa wale wapambe nuksi njoeni tena.
Utabiri wangu Mbowe atadondoshwa na Lisu maana Ile mashine sio mchezo.
Huo uzushi wenu mnatunga Lumumba halafu mnamlisha Mbowe maneno shenzi zenu MATAGA.
Weka uthibisho wa Ujinga wenu huo mnao sema.
 
Back
Top Bottom