Uchaguzi 2020 Fr. Kitima: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa na vifo vingi kuliko chaguzi nyingine zote

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,038
9,928
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania (TEC), Fr. Charles Kitima ambaye aliwahi kuwa Vice Chancellor wa SAUT amekosoa wizi wa kura na kusema ni dhambi kwa Mungu kwa sababu ni uongo lakini pia inapelekea kuwa na viongozi wabaya. Amesema kwa miaka sita iliyopita, mazingira ya siasa Tanzania yameharibiwa kiasi cha kutoweza tena kuwa mfano wa nchi nyingine kuja kujifunza demokrasia nchini Tanzania.

Amekosoa suala la kuwa na wabunge wengi kupita bila kupingwa kwa wakati huu. Akiitaja hiyo kuwa ni sababu ya vijana wengi kutojihusisha na masuala ya siasa ikiwemo kupiga kura. Hivyo halihuwa ni mbaya na kupata viongozi wasiostahiki.

Aeyasema hayo katika kikao cha TCD ambacho pia amekikosoa kuwa hakuna haja ya maridhiano kwa kuwa hakuna waliokoseana. Hivyo ni jukumu la nchi kuweka mipango ya kusonga mbele na sio kuwa na maridhiano kwa sasa.

Amesema uchaguzi wa 2020 umesababisha vifo vya watu wengi kuliko chaguzi nyingine zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania. Amevitaka vyama kusimamia ilani zao ili kuepuka fujo. Amesisitiza Upendo haki na amani.
 
Yeye Huyo father ameshuhudia vifo vingapi na amezika watu wangapi?

Chaguzi zote ukiacha za mwalimu hakuna hata moja isiyokuwa na dosari za kuibwa kura.

Acheni chuki binafsi walioshindwa 2020 walishindwa kama wagombea wengine kura zao hazikutosha wagombee 2025 mbona nafasi zote zipo wazi hata ya Urais
 
Father Kitima japo ni Padre wangu lakini naona kakosa msimamo ni huyu huyu wakati wa JPM alikuwa akisifia kila kitu leo ameguka tena kuwa mkosoaji je kwa nini huo ukosoaji hakuuweka wazi tangu mwanzo Kiongozi wa dini msimamo wake unapaswa kuwa thabiti siku zote sio kubadilikabadilika.
 
Jamani uchaguzi 2020 ulikuwa na vifo vingi? Kweli?

Lisu alikuja akafanya kampeni bila watu kuuana! Huyu askofu anachuki zake za kipumbavu tu!

Nasikia ni home boy wa Lisu! Hivo vifo aliviona yeye tu? Ujinga kabisa!
 
Yeye Huyo father ameshuhudia vifo vingapi na amezika watu wangapi? Chaguzi zote ukiacha za mwalimu hakuna hata moja isiyokuwa na dosari za kuibwa kura acheni chuki binafsi walioshindwa 2020 walishindwa kama wagombea wengine kura zao hazikutosha wagombee 2025 mbona nafasi zote zipo wazi hata ya Urais
Wewe mwenyewe unajipinga katika andishi fupi namna hii bila ya kujitambua!

Kama unasema "chaguzi zote, hakuna hata moja isiyokuwa na dosar za kuibwa kura...", sasa itakuwaje "...walioshindwa 2020 kura zao hazikutosha"? Huoni kuwa "dosari" unazozisema hapa ndizo zilizosababisha "kura zao kutotosha"?
 
Zanzibar uko Karume alizamisha watu kwenye mashua wengine wakapigwa risasi na jeshi. Lakini watakwambia nchi hii hakujawai tokea mauaji kama kipindi cha Magufuli.
Kwa hiyo wewe unasemaje, kwa vile kuna hadithi za kusimliwa juu ya Karume ndizo tuzilinganishe na hizi zilizoshuhudiwa hivi karibuni wakati wa Magufuli. Halafu watu waseme Magufuli alikuwa malaika?
 
Jamani uchaguzi 2020 ulikuwa na vifo vingi? Kweli? Lisu alikuja akafanya kampeni bila watu kuuana! Huyu askofu anachuki zake za kipumbavu tu! Nasikia ni home boy wa Lisu! Hivo vifo aliviona yeye tu? Ujinga kabisa!
Wewe hapa unayapayuka , kwa msukumo wa unazi juu ya mtu au chama bila ya kuwa na takwimu zozote.

Usitegemee mtu kama huyo anaweza kusema maneno kama hayo, tena kwenye hadhara ya aina ile bila ya kuwa na ushahidi anaoutegemea.
 
Wewe hapa unayapayuka , kwa msukumo wa unazi juu ya mtu au chama bila ya kuwa na takwimu zozote. Usitegemee mtu kama huyo anaweza kusema maneno kama hayo, tena kwenye hadhara ya aina ile bila ya kuwa na ushahidi anaoutegemea.
akina Mdee tuliona wakituonyesha makaratasi tu ya kura bandia, hao watu wengi Kitima aliosema wamekufa, walikufa mkoa upi?

Huyu padre naye ndio maana Kagame anawafunga, kanisa katoliki liliusika sana na mauaji ya Kimbali nchi Rwanda.
 
Jamani uchaguzi 2020 ulikuwa na vifo vingi? Kweli? Lisu alikuja akafanya kampeni bila watu kuuana! Huyu askofu anachuki zake za kipumbavu tu! Nasikia ni home boy wa Lisu! Hivo vifo aliviona yeye tu? Ujinga kabisa!
Nenda kule Zanzibar ukaongee hivyo. Watu waliawa kweupe, watu wakiona, halafu wewe unaleta kejeli!
 
Yeye Huyo father ameshuhudia vifo vingapi na amezika watu wangapi? Chaguzi zote ukiacha za mwalimu h

Acha unafiki. Nikweli Kura ziliibiwa. Kwa mfano Jimbo la Tabora Mjini Hawa Mwaifunga alinyanganywa ushindi mchana kweupe. Alishinda kata nyingi na mgombea wa ccm alishinda kata mbili tu.

Kukataa mabaya ya nyuma na kuyafunika ndio chanzo Cha mgogoro. Ni Bora kukubali makosa na kusameheana ndipo amani ya kweli itakuja.
 
Amesahau vifo vya uchaguzi wa 2000 Zanzibar? Au damu za Wazanzibari hazina thamani?

Unajaribu kukataa ukweli kwa kutafuta visingizio vya zamani?. Ni wapi amesema 2000 Watu hawakufa? Kasema uchaguzi wa mwaka 2020 Watu wengi walikufa kuliko uchaguzi wowote ule, ukiwemo wa 2000.
 
Wewe hapa unayapayuka , kwa msukumo wa unazi juu ya mtu au chama bila ya kuwa na takwimu zozote. Usitegemee mtu kama huyo anaweza kusema maneno kama hayo, tena kwenye hadhara ya aina ile bila ya kuwa na ushahidi anaoutegemea.
Hakina mdee tuliona wakituonyesha makaratasi tu ya kura bandia, hao watu wengi Kitima aliosema wamekufa, walikufa mkoa hupi? ndio maana Kagame anawafunga kanisa katoriki, liliusika sana na mauaji ya Kimbali nchi Rwanda,hatuletee takwimu za chaguzi zilizo pita hadi 2020 tupime,msomi gani huyu anayeongea bila takwimu? Padre hovo kabisa
 
Back
Top Bottom