#COVID19 Fizikia katikati ya COVID-19

onea 22

Member
Jul 31, 2020
34
20
Katikati ya mwezi wa tano mwaka 2020, dunia ilikuwa katika sintofahamu kubwa iliyoletwa kutokana na janga la corona. Ni kipindi ambacho ratiba pamoja mienendo mingi ya wanaaajamii duniani kote ilipaswa kubadilika ili kuendana na nyakati zile.

Watu walipaswa kukaa mbali mbali(angalau mita moja) ,kuvaa barakoa(I never heard this word before covid), kunawa mikono mara kwa mara, kutumia vitakasa mikono (sanitisers), kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima, kutengwa (quaranteen) na ilipobidi watu wa mji mzima walifungiwa ndani (lock down).

Siku moja (wakati janga bado la moto) nilikwenda dukani kupata huduma za msingi. Kutokana na maelekezo ya kipindi hicho nilikuta kumewekwa ndoo yenye maji tiririka na sabuni.(kwamba ni lazima unawe mikono ndio uhudumiwe).

Mteja aliyekuwa mbele yangu alinawa vizuri akasogea kuhudumiwa. Ilipofika zamu yangu nikafungua koki lakini maji hayakutoka. Nikamshirikisha muuzaji ili aweke maji mengine huduma ziendelee. Muuzaji akaniambia kuwa mimi ni mteja watatu pale tangu ajaze maji, inakuwaje yawe yameisha?

Mteja aliyekuwa mbele yangu akaniambia kuwa “kama maji yapo kwenye ndoo, na unafungua koki hayatoki, inabidi inabidi ufungue mfuniko wa juu maji yatatoka”. Kweli bhana, kufanya kama nilivyoelekezwa na jamaa maji yakatoka. Nikafanya yangu nikamaliza. Lakini bado nilikuwa na maswali like how could that happen? Majibu sikuwa nayo wakati huo, nikamuuliza Yule jamaa kwa nini imekuwa hivyo? Jamaa pia hakuwa na jibu..(to me how, what, when,why= life) so I question every thing hata kiwe minor kiasi gani..

Niliporudi nyumbani nilifungua madesa na kuanza kuchimba ni kitu gani hasa kilipelekea maji kutokutoka kwenye ndoo ya corona?(mbali na kuwa maji yalikuwepo na koki ilikuwa on) jibu likaja kupatikana kwenye presha. Unapokaza mfuniko wan doo ya corona juu, unapunguza presha ndani ya ndoo..wakti huo huo nje ya ndoo kuna presha inayosababishwa na mgandamizo wa hewa. Presha kuwa ndogo ndani ya ndoo kunazua maji kutoka nje kupitia koki..(hata wewe kama uko zako ndani halafu ukasikia nje kuna mtiti ,,let say bokoharam wanakichafua nje utatoka au utabaki ndani??je utafanyaje mtiti ukihamia ndani pia?yaani ndani mtiti nje mtiti…..ni lazima utoke nje angalau kuna nafasi ya kukinmbia). Kutokana na presha ndogo ndani ya ndoo hata gravity inaweza kuwa denied…kinyume chake , pindi unapofungua ndoo, presha ya ndani na nje ya ndoo zinabalansi na kupelekea mgandamizo juu ya maji kuongezeka na kulazimisha maji kutoka in response to gravity.

Joke!!

Tuachane na mambo magumu kuelezeka, je ni jinsi gani hii observation inaweza kuwa applied katika maisha ya kwaida??

1.kwenye ndoa, kwenye mahusiano ukitaka mwanaume asitoke nje ya mahusiano basi punguza presha ndani..un necessary makelele yanapelekea mwanaume kuflow out mahusiano naturally.(though viseversa can be true)

2. in a positive ,pressure ikiongezeka ndani financially , mwanaume ataflow out naturally kwenda kutafuta..so next time ukiona boy wako amekaa kizembe ongeza presha ndani,,beba mimba,omba hela za kusuka,,umwa umwa hovyo, anza vikoba etc..trust me atatoka tuuuu,,kwenda kutafuta au la siwezi kukuguarantee,,na kwenye kutafuta kupata , kukosa pia siwezi kuguarantee..ila all I know ni kwamba ATATOKA.
 
Back
Top Bottom