UZUSHI Fiston Kalala Mayele amesaini miaka 3 Kaizer Chiefs

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kwa mujibu wa vyanzo , Mwana habari Nuhu Adam amevujisha habari ya Mchezaji Fiston Mayele kusaini kandarasi mpya na club ya Kaizer Chief ya S.A.

fiston ed_0.jpg
 
Tunachokijua
Mnamo Julai 30, 2022 mwandishi wa habari za michezo Nuhu Adam kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha kuwa klabu ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi kuu ya Supersport Afrika Kusini tayari wameinasa saini ya mchezaji wa Yanga, Fiston Mayele kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu. Taarifa hiyo ilieleza:

Timu kubwa ya Afrika Kusini @kcfcofficial 🇿🇦 imemaliza kumsajili mshambuliaji wa @yangasc 🇹🇿 Fiston Kalala Mayele (28) kwa mkataba wa miaka mitatu, tangazo linakuja hivi karibuni. Mayele alikuwa mfungaji wa pili bora katika Ligi Kuu ya Tanzania msimu huu akiwa na magoli 16.

Taarifa hiyo ilipelekea gumzo kwa mashabiki na wadau wa soka ndani na nje ya Tanzania kutoelewa hatima ya mchezaji huyo kutokana na mchango wake mkubwa kwa kufanikisha kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Hersi Ally Said alikanusha madai hayo na kusema ni uongo wala hawajapokea ofa yoyote kutoka klabu ya Kaizer Chiefs na kusema Fiston Mayele bado ni mchezaji wa Yanga.

Alisisitiza kuwa Mayele hauzwi pia aliendelea kusema kuwa ni uzushi uliotengenezwa ili kuvuruga klabu hiyo kutokana na ukali alionesha mchezaji huyo kwa kufunga magori 16 katika ligi kuu ndani ya msimu wake wa kwanza.

Kwa upande wa Kaizer Chiefs mfungaji na mchezaji wa zamani Shaun Permall alikanusha habari hiyo kuwa timu haina mpango wa kusajili mchezaji atakayesimama nafasi ya ufungaji kutokana na timu kuwa na idadi kubwa ya wafungaji.

Hivyo, kutokana na taarifa hizo kutoka Wahusika wa Vilabu hivyo, JamiiForums inaona kuwa hoja ya Mayele kusajiliwa na Keiza Chiefs inawea kuwa ni tetesi na hakuna uthibitisho mpaka sasa.

UPDATE:
Dirisha la usajili limefungwa na Mshambuliaji wa Fiston Kalala Mayele ameendelea kubaki Yanga. Hivyo, taarifa iliyomuhusisha mchezaji huyo kusajiliwa na Klabu ya Keiza Chiefs ya Afrika Kusini haina ukweli.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom