Festo Sanga: TANESCO imezidiwa, kuwepo na taasisi/wakala tatu (3) zinazosimamia suala la umeme nchini

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
87
103

Nimechangia Bungeni namna mahitaji na matumizi ya Umeme yalivyoongezeka nchini, wakati TANESCO inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa ndogo, usambazaji wa umeme ulikuwa kwa kiwango kidogo.
Tunapozungumza leo, uwekezaji uliopo nchini wa viwanda na migodi (Mfano Mgodi wa Geita kwa siku moja unatumia umeme wa Mkoa mzima wa Njombe , huo ni mgodi mmoja tu je tuna migodi mingapi?, hapo hatujazungumzia Viwanda na matumizi binafsi).Vilevile namna serikali ilivyosambaza kwa ukubwa Umeme vijijini (REA) zaidi ya Vijiji elfu 11 vimefikiwa na umeme kati ya Vijiji elfu 12 vyote nchini, ni wazi TANESCO lazima izidiwe na isaidiwe.

Mapendekezo yangu ni kuwa, huu ni wakati sahihi wa kuwa na mamlaka/walaka ya Uzalishaji -Generation(kufua umeme),wakala/mamlaka ya kusafirisha (Transmission) umeme (Gridi ya Taifa na gridi zingine) na wakala/mamlaka ya Kusambaza umeme (Distribution).

Mitambo ikizimika, gridi ya Taifa ikipata shida, Mwananchi asipoingiziwa umeme, mita zisipopatikana kwa wakati, nguzo ikianguka, umeme ukiwa low voltage,Mzigo wote huu unaelekezwa TANESCO.

Ukiangalia nguvu kazi ya TANESCO, bajeti yao, uhaba wa ofisi na vitendea kazi kwenye ngazi ya wilaya n.k ni wazi muhimu kuangalia namna ya kuisaidia TANESCO.

Mfano mzuri wa Usambazaji (distribution) uliofanyika hivi karibuni na kuwafukiwa wananchi wengi ni uwe wa REA nchini, umeme umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Je hatuoni kufanya hivyo kwenye Uzalishaji na usafirishaji kuwa na shirika au mamlaka zinazohusika?.

Maoni yangu kwa Taifa langu Mama Tanzania🇹🇿

Festo Richard Sanga
Mb-Makete
 
TRA ipo moja tu na inakusanya mapato nchi nzima, isiwe sababu ya kuweka mitaasisi chungu mzima zenye wakurugenzi na bodi za menejimenti

Hapo ni kuweka idara na Kurugenzi ili zishughulikie masuala hayo ila utendaji uwe mmoja kutokea juu
 
Kwa muktadha huu nadhani kwakuwa nchi yetu ni kubwa sana tuwe na maraisi wa nchi walau watatu
 
Back
Top Bottom