Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Tanesco. Nimefungiwa mita ya peke angu dukani kuepusha usumbufu na wapangaji wengine ila naona kama units napewa ndogo yani mfano sh elfu 10 ni units 14.1???? hii iko sawa kweli au niende ofisini wanijuze zaidi
 
Mita ina deni hiyo hivyo wanakata Nusu unapewa Umeme Nusu
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
Je Wateja wanao tumia umeme chini ya Units 75 kwa mwezi bado wanasajiliwa?
 
Tanesco oye!!!!!

Sasa tanesco naombeni mnisaidie kwenye upande wa luku nyumbani kwangu daah sasa imepita wiki moja ,nimetumia taarifa ya kuja kufungiwa nyingine (ukiacha na hii ya zamani iliyofeli) lakini naona kama wanaipuuzia

Nateseka nafadhaika umeme hamna biashara haiendi ndo nini sasa tunafanyiana hiviii

Mimi nipo Mbezi mwisho nomewatumia taarifa(kupitia huduma Kwa wateja) lakini sioni matokeo Hadi kweli....hivi ingekuwa ni nyie kwenu ingekuwaje mngeweza vumilia Kwa wiki bila umeme ?

Anyway simu inaisha chaji subiri niipeleke Kwa jirani ijae tuje kuendelea
 
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hio, tafadhali tupatie namba ya taarifa kwa hatua zaidi ^EB
 
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hio, tafadhali tupatie namba ya taarifa kwa hatua zaidi ^EB
3496310-namba ya taarifa

Naombeni tuu jamani hata leo mkiweza mje daah napata shida sana kwenye hii dunia daaah kitendo Cha kubadilisha luku tuuh nakaa na giza wiki sasa inaelekea ya pili

Natumaini ombi langu limekubaliwa nitakuja kutoa ushuhuda hapa hapa

Mimi nipo dar es salaam,katika wilaya ya ubungo ,eneo ni kibanda Cha mkaa ,nyuma ya stand ya malori

Tanesco wetu niwasikivu naombeni muweze nifanyia wepesi
 
Namba ya simu nimewapa Kila kitu mnachokihitaji nimewapatia sasa imeshapita wiki sasa ,hamjatokea tatizo sijajua ni nini sasa wakuu wangu wa umeme

Sasa natumai solar (unaniumiza sana) na hapa simu chaji ishaisha biashara yangu ya maziwa Kwa sasa nimesimama (nimeingiza hasara ya shilingi laki tatu hadi sasa ),wateja wanagoma kununua maji ya moto dukani kwangu daaah

Naombeni tuumje leo kama ikiwezekana naona nawapigua simu lakini hamna majibu daah naumia sana jinsi siku zinavyoenda

Naombeni
 
3496310-namba ya taarifa

Naombeni tuu jamani hata leo mkiweza mje daah napata shida sana kwenye hii dunia daaah kitendo Cha kubadilisha luku tuuh nakaa na giza wiki sasa inaelekea ya pili

Natumaini ombi langu limekubaliwa nitakuja kutoa ushuhuda hapa hapa

Mimi nipo dar es salaam,katika wilaya ya ubungo ,eneo ni kibanda Cha mkaa ,nyuma ya stand ya malori

Tanesco wetu niwasikivu naombeni muweze nifanyia wepesi

Wanakuzungusha kukuletea huduma (ambayo unailipia) halafu bado unawaita 'wasikivu'?!!!

Hili shirika ni cancer, nchi nzima kote ni kero kero kero!

-Kaveli-
 
Sawa Ila huu Mgao wa umeme alafu mnasingizia matengenezo madogo madogo acheni.Semeni ukweli tununue Solar na gensets
 
Vip kama nimehama kutoka nyumba nyingine kwenda nyingine lakini nyumba ya kwanza ilikuwa na Mita yangu na nimeiuza hio nyumba nikanunua nyumba ingine yenye Mita ingine..je ninaeza kuchukua Mita yangu ya mwanzo nikahamia nayo nyumba ya Sasa Kwa maana inajina langu..?
 
Back
Top Bottom