Fahamu jinsi ya kuchagua TV nzuri itakayokufaa kabla hujanunua

Issuna

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,168
7,523
1.jpg

Kwanza kabisa tufahamu tupo mwaka 2019 na teknolojia imebadilika kwa kiasi kikubwa na watu wanaamia kwenye ulimwengu wa flat panel (maarufu kama flat screen) kama kuna watu wenye zile za zamani a.k.a vichogo basi naamini ni wachache ambao watakuwa wanasoma post hii kama wapo, basi bila kupoteza muda twende kwenye maelezo zaidi.
  • TV GANI UNATAKIWA KUNUNUA
Kuna makampuni mengi hivi sasa yanayotengeneza aina mbalimbali za Tv kama vile Samsung, LG, Hisense, Sharp , TLC, Philips na kadhalika.

Kila kampuni ina aina yake ya utengenezaji wa bidhaa zao na sifa za kipekee ila sote tunatambua kuwa LG, SONY na Samsung ndio wameliteka soko la Tv kwa sasa ingawa unaweza kupata Tv nzuri kutoka katika makampuni mengine bila shaka lolote.

Kwa hiyo kwa kujibu swali hili ningeweza kukujibu kwa kusema kwamba usiangalie kampuni ili ununue Tv nzuri bali angalia budget uliyo nayo, ubora wa bidhaa, size ya kioo ukipendacho, kwa mfano; mimi nina laki tano (500,000 Tzs) nataka nipate flat iliyo smart ambayo pia ni inch 32, sasa tukiangalia katika makampuni kama SONY au LG au Samsung kamwe kupata Tv ya namna hiyo hutoweza kupata labda iwe used.

Ila ukichukua uamuzi wa kutembelea makampuni mengine unaweza walau kupata Tv kama hiyo kwa mfano Sharp au TLC, kwahiyo mwisho wa siku nafahamu wengine hawawezi kutumia kitu kutoka tofauti na kampuni fulani kwasababu pengine wanaona kuwa labda ndio zina dumu nk.

Kitu hicho si cha kweli na labda tu niwafahamishe kuwa makampuni yote yanafanya biashara na mara nyingi makampuni makubwa huwa wanatoa bidhaa zenye bei kubwa huku wakiongeza kitu kidogo tu katika bidhaa yao.

Kwahiyo cha kufanya ni kuangalia ni sifa gani unazotaka kwa ajili ya Tv yako ili uweze kuridhika bila kugharamia pesa nyingi ila kama una hela unamwaga tu hiyo mipesa.
  • FAHAMU RESOLUTION GANI ITAKUFAA KATIKA TV
Resolution ni suala muhimu sana katika Tv na ninaamini watu wengi sana huwa hawafuatilii swala hili na baadhi yetu sidhan kama tunafahamu hata maana yake, sasa kama ushawahi kupita dukani ukaulizia Tv basi lazima watakuambia "Hii ni HD" sasa watu wanafahamu kuwa HD ni kwamba Quality ya picha katika Tv yako ni nzuri well ni kweli lakini hizo hizo HD huwa zinatofautiana.

Nitaorodhesha kama ifuatavyo:

HD: Ukiona HD huwa inawakilishwa na 1280x720 Pixels au huitwa 720p (soma hapa kuelewa maana ya Pixels) na hii sasa ndio ile ukienda Kariakoo watakuambia hi ni HD hii ni HD lakini hawatoi maelezo ya kutosha sasa ngoja niwaonyeshe utofauti wake

2.jpg

Ningekuwa nimeweka HD peke yake usingeweza kutofautisha lakini ukiangalia hapo utaona kiji utofauti kidogo hapo na hiyo ndio maana ya pixels na umuhimu wake katika Tv unapata kitu chenye detals nzuri. Lakini mwisho wa siku HD iko poa ila tu ukiamia daraja linalofuata uataona HD ilikuwa ya kawaida tu.

FULL HD (FHD): Hii sasa inawakilishwa na 1920x1080 Pixels maarufu kama 1080P, unaweza ukapita kwa sasa kwenye baadhi ya maduka ukakuta stika zimebandikwa kwenye baadhi ya TV ukitizama utaona kimeandikwa (FHD) lakini pia wauzaji wengi huwa hawaelezei utofauti wake. Kwa ufupi hii ndio wengi wanatakiwa wawe nayo kama ukitaka uzuri wa content katika Tv yako ingawa kuna 4K lakini kiukweli kitanzania bado sana. Angalia picha hapa chini:

3.jpg

Angalia na hii ya bundi hapa chini

4.jpg

Kama uanavyo hapo picha za 4K zina details kwa wingi na ziko very sharp lakini still hauwezi kusema kuwa 1080P ni mbaya iko very good na inaonyesha vizuri sema 4K ni vizuri zaidi.

4K: Hii inawakilishwa na 3840 × 2160 Pixels maarufu kama 4K. Siku hizi watu wengi wengi wanaziongelea lakini naamini uwelewa ni mdogo juu ya hili suala kwasababu kwanza tangu mwaka 2015 mapinduzi ya 4K yalipoingia kwa wale watu wafuatiliaji wa dunia ya kiteknolojia, contents nyingi kama vile movies, music, videos etc zinapatikana kwenye 1080P kwa sana na baadhi ambazo nimeziona zinapatikana ni gharama sana kibongo bongo ila natumaini huko tunapoenda natumaini mambo yatabadilika.

Kama ni mpenzi wa quality katika Tv kwa sasa Youtube ina support kuplay hadi 8K kwa hiyo kama utakuwa na Tv yako ambayo ni Smart unaweza kuenjoy hapa kuangalia contents zenye 4K kupitia Youtube. Huu ni mfano wa 4K:

5.jpg

Hilo ni game (Assasin Creed) lilikuwa linachezwa katika PC ambayo imeunganishwa na Tv na kutestiwa utofauti kati ya 4K na 1080P, na kama unavyoona hapo utofauti unaonekana moja picha inaonesha details vizuri na nyingine ina kama blur hivi ila mwisho wa siku nashauri kama unaona hauna ulazima wa 4K just baki kwenye 1080P ila kama mpenzi wa teknolojia sana haya 4K ipo kwa ajili yako.

4K AU 1080P AU 720P: Kwa sasa hata nchi zilizoendelea bado hawajakomaa katika matumizi ya 4K na ndio kwanza kwa mfano mwaka 2016 ndio deki zinazoplay 4K zimetoka lakini zina bei kubwa sana, kama 600,000 hivi na ukirudi kwa wale wazee wa consoles pia binafsi sidhani PS5 ikitoka au hiyo Xbox mpya itakayotoka kama itasupport 4K na hata zikitoka bei yake itakuwa sio ya kitoto kwahiyo kati ya hivyo vitatu ningeshauri bora kukaa kwenye Tv yenye 1080P kwacsababu mwisho wa siku utachukua 4K halafu itakuwa ni kituko kama hivi

7.jpg

Ukiona hapo hiyo ni Tv ambayo ni 4K na ndani video inayoplay ni 720p hebu ona nafasi inayobaki pembeni labda Tv ikiwa na uwezo wa kufanya Upscaling ndio ikuze hiyo video ienee kwa screen lakini ikikuza kumbuka Quality itapotea.

BAKI KWENYE 1080P ila kama una kiherehere kama mimi haya nunua 4K for the future!
  • UKUBWA GANI WA TV UTAKUFAA
Nitarudi palepale kwamba ununuzi wa Tv ni chaguo la mtu binafsi, ninacho kifanya ni kutoa ushauri tu ili mtu aweze kupata Tv nzuri ya kuangalia na kuenjoy.

Kwa size za Tv nafahamu zipo nyingi mpaka inch 126 ila size ambayo itamfanya mtu aenjoy kuangalia kionekanacho katika Tv ni kuanzia inch 40 kwenda juu, najua lazima utajifikiria sana ukubwachuo utapatikana kwa bei gani?

Kiukweli kwa Tv hizo kama LG au Samsung au Sony lazima upate kuanzia 1,000,000 mpaka milioni 1.5 mpaka milioni mbili lakini makampuni kama Hisense wanatoa Tv zao zenye inch 40 kwa Tzs 500,000 mpaka 700,00 inaweza kuwa kubwa lakini still ni bei nafuu ukilinganisha na hao wengine.
  • JE NI MUHIMU KUWA NA SMART TV
Smart Tvs binafsi naona sawa ni feature moja nzuri kwasababu unaweza uka browse google ukaingia YouTube na kadhalika lakini sidhani kama ukikosa utakuwa umekosa kitu kikubwa sana na kwa sababu hii basi makampuni ya Tv yanatumia nafasi hiyo kutuuzia Tv za Smart kwa bei ya juu sana, kwa mfano juzi nilienda Mlimani City katika store ya Game pale dada wa pale akaniambia Hio 1080p smart ni shilingi 1.9milioni na hiyo 1080P ambayo sio smart ni 1.2 milioni

Sasa nikajiuliza kuwa na Smart ndio laki saba nzima inaongezeka jamani? Kwahiyo kama unavyoona wakiongeza kakitu kadogo tu basi bei wanaongeza pia like really bruuh?

Kama ingetokea nimesimamia zoezi la kutengeneza Tv ningeiita Smart lakini ningetoa vitu ambavyo havina umuhimu kivile kwa mfano SmartCast ni kitu kizuri sana katika Tv ambayo inakuwezesha kuplay kitu kwenye simu yako na ku display kule kwenye Tv.

Kitu kama Wi-Fi ni muhimu sana kwenye Tv kwa ajili ya kustream ingawa kwa bongo Netflix au Hulu au Amazon ambazo ni huduma za kustream zinazoonyesha Movies au Series etc bahati mbaya kwa nchi kama Tanzania hatuna services hizo ila nimeona Netflix wamezindua Tanzania inapatikana, ila hebu imagine unastream episode moja ya Game Of Thrones ambayo ina dakika 50 halafu network zetu na bando zetu hizi khaa kwakweli inahitaji pumzi ya kutosha na hela ya kutosha.

Ila tunapoelekea natumai teknolojia itanyooka tu.Kwahiyo tukiongelea Smart Tv ufahamu kuwa utakachoenjoy ni Youtube labda na browser. Sasa ukiangalia hapo si wanatuuzia Youtube na browser kwe laki saba ndugu zangu? Anyways mwisho wa siku ni mfuko wa mtu.

Kwa kumaliza kabisa ndugu zangu mimi napenda kutoa ushauri mkubwa kabisa wa kuangali sifa za Tv kabla hujanunua iwe mtumba au mpya dukani usije ukanunua kitu ambacho kuenjoy huwezi.

Kuna sifa nyingi sana ambazo zipo katika Tv zetu kwa hiyo natumaini walau mambo haya machache yatakupa ufahamu na kufanya uamuzi mzuri katika kununua Tv.

Cheers..

Maoni ya wadau:
Zipo technology za kuscale na TV ya 4K yenye HDR10 ama Dolby vision (Tv nyingi zina hizi technology) zitaonyesha vizuri video ya HDR bila kujali resolution compare na Tv ya kawaida. Pia Kuna Tv/simu ambazo zina convert video ya kawaida kwenda HDR.

Tatizo watu wengi wanaodisplay hizo TV za 4K hawatafuti content zake badala yake wanajichukulia tu video za kawaida na kuweka kwenye flash.

Tembelea hata site ya torrent search video yoyote ya 10bit resolution unayotaka wewe then iplay kwenye Tv ya 4K na 720p utaona utofauti.
Pia kwa mwaka 2019 kwenda mbele ni vizuri kuzingatia vitu kama:

- Display Technology, hapa inaweza kuwa Oled, Qled etc

- Pia view angle ya Tv ni nzuri sana kwa seat arrangement hii depend na chumba chako kikoje, maana kuna Tv ukikaa pembeni ya kochi tu unaona kama ukungu (Star X nyingi na michina mingine hii view angle kwao shida)

- Contrasts ratio, HDR compatibility hapa utapata picha moja kali sana hasa ukiwa na Dolby version HDR, input and output pia la kuzingatia hili.
Mkuu hapa pia sio asilimia 100 kwamba mtu atapata anachotamani.

Kitu nimegundua katika hizi Tv za kisasa, zina video zake. Ukiiwekea video ya ubora tofauti ni 1, isionyeshe au 2, ionyeshe ugoro.

Mfano HD tunaanzia 480P, hii picha haichezi katika deki zetu za wakina lufufu, ukiweka mpg katika hii deki ukawa unaangalia kwa flat 32inch hata ungetumia HDM bado ni upuuzi tu kuangalia. Hiyo video ya 480P ina detail ndogo sana lakini ubora wake ni mzuri.

Kama kuna watu wanatumia king'amuzi cha Azam watanielewa linapokuja suala la TBC 1 na HDM cable, ni vitu visivyo na ushirikiano kabisa.
Ninavyojua ama nilivyokariri Tv nzuri ni brand zifuatazo:
1. Sony
2. LG
3. Samsung
4. Hisense
5. TCL
 
Natamani kujua zile Curve Tv zina nini? Mkuu, Tv yangu Ina HDMI, pal- srcam, DBT-T / TNT, FHD 1080, standing by power<1W, Usb 2.0, eco,Atv,dtv, DVB(T) terrestrial.

Kuna label pembeni vingine sijui hata kazi zake.
Unajua Port za Tv zinaongezwa kutokana na vifaa vipya vinavyotumika. HDMI ni kutokana vifaa vingi vilikua vinatumia HDMI, kadhalika VGA nk kadri miaka inavyoenda port zitaongezeka na nyingine hutoweza hata zitumia kutokana na hauna vifaa vya ku connect na Tv yako.
 
Asante umetoa elimu nzuri sana kwenye hili suala. Binafsi nilikuwa sijajua hasa 4k ni nini na hata wauzaji wengi wanakwambia tu hii ina 4K lakini ukimuuliza hawezi kutoa haya maelezo. Nimefaidika na nimeweka kwa matumizi ya baadae.
 
Back
Top Bottom