SoC02 Fahamu haya mambo mawili kabla ya kuamua kufanya biashara

Stories of Change - 2022 Competition

IFAC

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
3,658
9,264
Nipo sehemu kwenye mgundi wangu wa kila siku nimekaa, nikitafakari mambo mbalimbali katika maisha ila likubwa tambua biashara inakulazimisha kutambua haya mambo mawili ili uweze kufanikiwa:

Uhitaji Uchawi wala Ndumba ila inatakiwa ujue kuzihimili hizi sababu kuu mbili ili uweze kufanikiwa kwenye biashara uliyopanga kufanya.

Asilimia Tisini(90) ya biashara zilizoanzishwa hufa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, tangu kuanzishwa.

Asilimia Tano(5) hufa ndani ya miaka mitano toka ianzishwe.

Ile asilimia tano (5) iliyobakia mara nyingi ni biashara zinazoishi ili kukutengenezea heshima badala ya faida, yaani haitengenezi faida ya maana ila pia haitengenezi hasara ya kiwango Cha juu ili ife.

Hivyo unagundua kufanya biashara sio jambo jepesi kama wengi wanavyodhani, na sio sehemu ya kwenda kwa watu waliokata tamaa au kuwa na tamaa ya kupata utajiri kwa kipindi kifupi.

Kufanya biashara kwa mazingira ya kiafrika ni jambo lisilo gumu ila linalohitaji kujuwa kanuni mbili ili ufanikiwe au ufeli, kabla ya kuanza kupambana na Kodi mgandamizo toka serikarini.

Sababu zenyewe sio mpya, unazihitaji kila mahali ili uweze kuwa mahiri na kufanikiwa , kwenye kila jambo, ila kwa Leo tutaziangalia upande huu wa biashara.

(1) MUDA
Kijana nakuibia Siri hii, biashara yoyote inahitaji muda wako ili uweze kufanikiwa,
Kumbuka inahitaji rasilimali muda ili uweze kuijua biashara yako.

Usipoipa muda wa kutosha wa kuisimamia biashara, huwezi kujua kiwango cha changamoto, madhila, faida wala hasara, nje ya namna ya maboresho yanayotakiwa ili uweze kuvutia wateja zaidi.

Kumbuka watu hupenda kuwekeza mitaji, ila kinachowakwamisha kikubwa ni muda.

Mfano: Bwana Mwembe alipata Milioni 20 baada ya kuuza shamba lake lilipo Mjimwema kutokana na mradi mpya wa makazi kigamboni, Hivyo kutamani kuingia kwenye biashara.

Biashara aliyoona inamfaa ni kununua Mitumbwi ili kuwapa Vijana waweze kuvua bahari kuu, halafu samaki watakao patikana walete faida baada ya kuuzwa.

Kumbuka hajui kuvua, wala hajui kuogelea hivyo shughuli nzima ilisimamiwa na Vijana ambao uhaminifu wao ni wa kutilia mashaka.
Je, Atapata faida? Atazijua changamoto za uvuvi? Hali iliyopelekea biashara kumshinda.

Ukitaka kufanikiwa kwenye biashara wekeza muda, muda utakupa mawindo mazuri kwenye biashara yako.

Hali hii huwakuta wafanyabiashara wengi ambao Wana ajira zinazotumia au kula muda wao mwingi hivyo kujikuta biashara kwao hazina faida bali zinawaletea sifa tu kwenye jamii.
Wengine huenda mpaka wanatoa pesa Toka vyanzo vingine ili tu biashara isianguke.

Tafadhali unapoanzisha biashara hakikisha una muda wa kutosha kuisimamia lisije likakukuta ukalia kama mbwa mkiwa.

(2) MTAJI
Nani asiyejua mtaji ndio sababu kuu, ya wafanyabiashara wengi na wajasiriamali wenye mawazo chanya kushindwa kutoboa kwenye biashara.

Ndio biashara nyingi zinakwama miaka kwa miaka kisa hakuna mtaji wa ziada ili iweze kuongeza kiwango Cha pesa ingiza( cash inflow) hivyo kupelekea biashara kuwa mbilikimo yaani biashara isiyokuwa.

Hii ndiyo sababu inayofanya Vijana kushindwa pata mitaji wezeshi hivyo kupelekea wengi kukata tamaa.

Wakitaka waombe mikopo hawana, vitu vinavyotakiwa na benki au taasisi za kifedha hivyo kupelekea wengi kushindwa na kuingia kwenye mbio za panya.

Mfano:Mfanyabiashara mchanga ambaye hana Mali shikika inamuwia vigumu kupata mkopo kwenye taasisi za fedha.

NINI KIFANYIKE?
unahitaji muda na mtaji kwa pamoja ili uweze kukamilisha ndoto zako katika biashara, kinyume cha hapo jiandae kuanguka.
 
Unafanya biashara gani mkuu

Kwangu mimi masoko ndo kitu muhimu sana katika biashara. Unapofungua biashara, unategemea kumuuzia nani? Tabia ya ununuzi wake ipoje? Wateja wako wanataka nini kutoka kwako? Ukiweza kulitambua soko lako na kulihudumia ipasavyo na kuwashinda wapinzani wako ambao wanauza bidhaa kama yako basi utakuwa umeshida vita ya kibiashara
 
Nice post.!
 
True this
Screenshot_20220909-182213.jpg
 
Back
Top Bottom