Gerald .M Magembe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,496
- 1,797
Ila elimu ya Mbowe haitii mashaka. Kilaza oyeeeeeeeeeeee.Nimekuwa napata shida sana kutokana na elimu ya Gwajima . Tokea kipindi akitangazia umma na akiliamsha dude pale Kanisani kwake, basi ,nikawa napata shida kutokana na matamshi yake.
Kila kazi ina miiko yake. Askofu hatakiwi kutoa siri za muumini wake hata kama huyo muumini amelihama kanisa lake. Hapa niliona kwenye YouTube Gwajima akisema mambo ya siri ya mke wa Dkt. Slaa.
Leo nimeangalia tovuti ya kanisa la Gwajima. Katika hii tovuti ambayo ameandaa yeye mwenyewe nimeona mambo yafuatayo:
References
- Gwajima amezaliwa mwaka 1970
- Amemaliza shule ya msingi mwaka 1985
- Amemaliza shule ya sekondari Olevel mwaka 1993. Alichelewa kumaliza secondary sababu ya maradhi.
- Alimaliza Advanced Diploma in Bible and Theology mwaka 1994 mjini Nairobi Kenya. Hapa ndo pana ufisadi wa elimu. Yaani alisoma stashahada ya juu kwa mwaka mmoja tena baada ya kumaliza olevel. Kwa maoni yangu, huyu alichosoma ni level ya certificate. Matatizo ya Gwajima it yanaanzia hapa.
- Baada ya hiyo Advanced Diploma yake ambayo ni magumashi, alijiunga na chuo kinaiitwa Japan Bible Institute na kusomea Master’s degree in Christian Missions June 2006 mpaka February 2008. Hapa nilitaka kujua ni kwanini hiyo institute ilikubali kumpa admission mwanafunzi ambaye ambaye ana only post secondary study ya mwaka mmoja tu, nikakuta hiyo institute yenyewe nayo ni ya kimagumashi. Hiyo institute haina hata physical address . Ni Chuo cha kwenye mtandao na pia kinatoa degree by experience. Yaani waweza pewa hata degree kwa kuwa una uzoefu. Hii masters degree yake kumbe ni utata mtupu na achilia mbali kwamba hana sifa za kujoin hata kozi ya degree ya kwanza.
- Mwaka 2015 alipewa PhD na chuo cha kidini cha Afrika ya Kusini kinaitwa Omega Global University. Kwenye tovuti ya chuo hiki pana maelezo kwamba kinatoa honorary PhD. Gwajima haoneshi kwenye tovuti yake ni mwaka gani alijoin hiki chuo wala lini alimaliza. Pia, hiyo miaka, Gwajima alishakuwa na kanisa la misukule huko Ubungo na baadae kuhahmia Kawe. Tena ni mwaka ambao alikuwa mshenga wa kumleta Lowassa Chadema na baadaye kututobolea siri ya vyeti vya mkuu wa mkoa aitwaye Bashite. Hivyo basi, PhD hii ni ya heshima.
- Mwisho, kwa maoni yangu, elimu ya Gwajima ambayo haina mashaka kabisa ni ile ya form four mwaka 1993.
UNATAKA KUVUSHWA NA KILAZA.